Mapenzi yananitatiza

Pendaneni

Senior Member
Joined
Feb 12, 2014
Posts
134
Reaction score
108
Jamani mapenzi, yananitatiza, Kulala siwezi, kusema siwezi
Chakula sitaki, nakiiona sumu, Mapenzi yamenivaa, nami ugenini
Akili imenipaa, hata njia siioni, Mapenzi yana hadaa, ya kweli nawambieni

Haiba imepotea, uzuri umenitoka, mali imeangamia, maradhi hayakutoka,
Mwenzenu nimepotea, muokozi kanitoka, Enyi wenye ukarimu, siri nawatobolea
Moyo umepata sumu, madawa hayakufaa, Kupenda kitu adimu, nawambia kuna baa

Ya kweli nawambieni, myatie akilini msipende ugenini, mtaingia hatiani
Mtalala majiani , wazimu tele vichwani🙂
 
kama yanakutatiza achana nayo
 
Miss Chagga wahenga walisema 'mapenzi ni utumwa' na kupenda ni maradhi omba sana yasikukute! Maana hayo maradhi hayana tiba asilani.......
Mafikizolo sasa unanishauri niachane na mapenzi nifanye nini zaidi!! Siwezi kuukataa uasilia jamani!
 
Mkuu unajua umekua ukicomplain sana kuusu mapenzi kukutesa, sasa jamani kama kitu unaona unafanya chakunyima raha,amani achana nacho,hata mfanya biashara akianzisha biashara akaona haimlipi huachana nao,unafanya vitu vingine,Ongea na Mungu muombe sana haya yataisha
Miss Chagga wahenga walisema 'mapenzi ni utumwa' na kupenda ni maradhi omba sana yasikukute! Maana hayo maradhi hayana tiba asilani.......
Mafikizolo sasa unanishauri niachane na mapenzi nifanye nini zaidi!! Siwezi kuukataa uasilia jamani!
 


HATA MAREHEMU MBARAKA mwishehe Mwaruka aliimba hivyo hivyo, hayo ni marudio tuuu.
 
Shyeeeh! movie hizi ona sa' binti anawaza kifilipino.
 
Bila shaka unamiaka kati ya 15 - 20 au kama umezidi miaka hiyo basi ulichelewa kuanza mapenzi.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…