Mzalendowadamu
JF-Expert Member
- Jul 10, 2016
- 218
- 318
Kulingana na ukaribu tulio nao amekua akinisimulia kila kitu kuhusu maisha yake. Picha lilianzia wakati akiwa Sekondari ikatokea kukosana na mwalimu wake kwa kumgombania mdada mmoja ambae alikua dem wa jamaa. Mwalimu alitengeneza uadui na kumsimaisha shule huku akiandaa mpango wa kumfukuzisha shule. Jamaa ikabidi awaeleze kaka zake mtaani wakamuibukia ticha na kumfanyia kifinyo na vitisho vikali.
Katika mtafaluku huo wapo maticha kadhaa walishuhudia jambao hilo na walimshawishi kuwa jambo hili alifikisha katika uongozi wa shule. Baada ya kuona jambo likiwa kubwa dada mmoja mtaani hapo akamchukua jamaa mpaka kwa sangoma, Sangoma kafanya yake ilikuwa siku ya Jumapili usiku ndipo mitego ikawekwa njiani ili kesho yake ticha akipita basi mzigo umshike.
Ilipofika J3 asubuhi jamaa alijificha sehemu ili kupata uhakika kuwa ticha amepita hapo mtegoni na kama alivyo tarajia ticha alifika kazini kwa kupitia hapo. Kila kengele jamaa alidhani ni dharula na kifuatacho anafukuzwa,lakini haikuwa hivyo na hakuna lililo tokea mpaka time ikafika kwenda home. Baada ya kutawanyika alipata taarifa kuwa ticha amelazimishwa azungumze kilicho tokea alakini anasema hakumbuki na wenzake wanamuona zuzu na kumcheka.
Jamaa alifurahi sana na hapo ndipo safari ya kuelekea kwa shetani ikakolea.
Baada ya miaka mingi kupita, Jamaa alipata mkasa wa kutendwa na mpenzi wake. Huyu alikuwa mdada ambae jamaa walipendana wakati mdada akiwa katika mafunzo ofisini kwetu, na baada ya kuhitimu alikaa home bila kazi na kwakuwa jamaa alikuwa anammega kisela akamfanyia mchakato kulingana na connection na ushawishi wa jamaa msichana akapata kazi na wakaishi kama mke na mume. Baada ya kupita miezi kama sita dem akaanza kuzingua, akawa anatoka na kibabu kimoja chenye pesa zake tena mbele ya jamaa bila kuficha na wafanyakazi wote wakajua, kwakweli jambo lile kila mtu aliyekuwa anajua aliumia sana. Jamaa alidhoofu sana na baada miezi kadhaa dem akapatapata ujauzito ambao alimwambia sio wake bali ni wa kibabu.
Hali ya jamaa ailikuwa mbaya mpaka akapewa likizo ili akapumzisha nafsi. Mdada Yule kila mtu alimchukia kwa vitendo vya dharau alivo kuwa anamfanyia jamaa, jambo moja lililo muumiza ni kuambiwa kuwa avumilie tu yeye atamzalia mtoto wa pili ila huyu ni wa kibabu. Jamaa akiwa likizo alitafakari sana safari yake ya maisha, ndipo akakumbuka mkasa wa ticha na solution ilikuwaje, na kwakuwa asingeweza kupambana na kibabu kwa pesa ikabidi azirejelee zama za sangoma kama ukombozi pekee wa wanyonge, alikwenda chimbo flani kwa mzee mmoja wa kutoka Congo na kumuelezea.
Baada ya kutoa maelezo mzee kamuuliza sasa unatakaje!? Hapo ukawa mtihani mwingine kwa jamaa kwani bado alikuwa anampenda dem na hataki kumuona na mimba ya jamaa, alitamani lifanyike jambo ili mpenzi wake awe kama zamani yaani bila kibabu wala mimba.Baada ya jamaa kumueleza mzee matamanio yake Yule mzee akamuomba malipo ya kazi na kumwabia aende kusibiri majibu.
Baada ya siku tatu yule msichana alipata maumivu ya tumbo ghafla na kukimbiza hospitali, akiwa bado yupo mapokezi alianza kutokwa damu na baada ya uchunguzi aliambiwa mimba imeharibika. Wakati akiwa hapo hospitali Yule kibabu akiwa njiani kuelekea hospitali kwa dem gafla gari yake ikapata ajali na kuanguka katika mtaro na kukatika mguu na kiganja cha mkono wa kulia.
ITAENDELEA …. ( stori ni ndefu)