Mapenzi Yana Viwango?

Companero

Platinum Member
Joined
Jul 12, 2008
Posts
5,609
Reaction score
1,738
Je, ni sahihi/haki kutoka au kuolewa na mtu ama kuoa mtu ambaye unampenda ila humpendi kwa kiwango kile kile (ama zaidi) ulichompenda mtu wako wa zamani?
 
Duh! Hii ni tricky ila nadhani ipo ingawa mi haijawahi kunitokea.
 
Wee unata ndoa unataka kupenda kwa kiwango cha zamani?
 
Kwa hiyo wewe kiwango kinapanda tu kadri unavyosonga mbele ( N > M > K) ?

Hahaahahaaa hukuweza kujizuia hadi uwataje hao eeeh?

Unajua bana, love is a phenomenon, i.e. it is difficult to understand or explain fully its workings.

Ni vigumu kusema kiwango kinapanda tu kadri ninavyosonga mbele kwa sababu kila mtu ana unique qualities zake. Sasa ukitaka kulinganisha kila mmoja wao ni sawa na kulinganisha matufaha na machungwa.

Matufaha na machungwa yote ni matunda lakini yako tofauti.
 
Je, ni sahihi/haki kutoka au kuolewa na mtu ama kuoa mtu ambaye unampenda ila humpendi kwa kiwango kile kile (ama zaidi) ulichompenda mtu wako wa zamani?

Penzi halina kiwango.kuwa na mtu unaempenda kwa ukweli.life is too short,utakapokufa uwe na mtu anaekulilia kiukweli .ukitaka kujua mtu anakupenda msisimko wa damu unavyokuwa kila umwonapo.Pray for wisdom
 
hebu dadavua hapo kwenye nyekundu - yaani mimi nikisisimkwa na damu ndio kipimo kuwa yeye ananipenda kiukweli, sayansi gani hii?
 
Je, ni sahihi/haki kutoka au kuolewa na mtu ama kuoa mtu ambaye unampenda ila humpendi kwa kiwango kile kile (ama zaidi) ulichompenda mtu wako wa zamani?

mapenzi hayana viwango, kupenda nikupenda tu haijarishi kwa mpenziwazamani au wasasa tofauti ni jinsi mtakavyo yaishi hayo mapenzi yenu.
 
- Kwa hiyo hakuna kiwango kati ya kupenda chungwa, dalanzi na chenza? Au embe dodo, nyonyo na bolibo?

- Hivyo kuna kupanda na kushuka kwa viwango i.e. N ulimpenda sana, M ukampenda kiasi, K unampenda sana?
 
- Yaani kuwe na hisia kali na hisia zisizo kali sana halafu bado kusiwe na tofauti ya viwango katika kupenda?

- Hata tukiweka hisia pembeni si kuna kujali sana na kujali kiasi, sasa hiyo si tofauti ya viwango vya kujali?
 
- Kwa hiyo hakuna kiwango kati ya kupenda chungwa, dalanzi na chenza? Au embe dodo, nyonyo na bolibo?

- Hivyo kuna kupanda na kushuka kwa viwango i.e. N ulimpenda sana, M ukampenda kiasi, K unampenda sana?

Standards lazima ziwepo bana la sivyo hata wewe mwenyewe basi utakuwa si mtu wa standards.

Muhimu ni kuzifanyia tu marekesho hapa na pale ili ziendane na uliye naye kwa wakati huo bila ku-compromise core principles.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…