MAPENZI YA MUNGU

Nicodemas Tambo Mwikozi

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2016
Posts
663
Reaction score
1,047
MAPENZI YA MUNGU

Ukijilaza na kupata usingizi, ujue ni mapenzi ya Mungu, lakini ukiamka asubuhi mzima wa afya, tambua kuwa ni mapenzi ya Mungu pia

Ukiweza kula na kumeza, jua kuwa ni mapenzi ya mapenzi ya Mungu. Lakini wakati mwingine hata unapokosa chakula ni mapenzi ya Mungu

Ukipata ajali na kunusurika kufa jua kuwa ni mapenzi ya Mungu. Lakini tambua kuwa hata wanaokufa ni mapenzi ya Mungu

Ukipata kazi nzuri au kupanda cheo kazini, ni mapenzi ya Mungu. Lakini hata kama bado hujapata kazi au kupanda cheo, tambua kuwa ni mapenzi ya Mungu

Ukifanyaa zinaa bila kupata ukimwi, ni mapenzi ya Mungu. Lakini hata siku utakayoambiwa umepata Ukimwi, tambua kuwa ni mapenzi ya Mungu

Ukimsaliti mwenzako bila kugundulika, ni mapenzi ya Mungu. Lakini hata siku utakapofumaniwa tambua kuwa ni mapenzi ya Mungu

Ukipata mali ya unyang'anyi bila kukamatwa, ni mapenzi ya Mungu. Lakini hata siku ya kukamatwa ukumbuke kuwa ni mapenzi ya Mungu

Mambo yakikuendea vizuri usisahau kuwa ni mapenzi ya Mungu, lakini hata yakigeuka mrama elewa kuwa ni mapenzi ya Mungu

Mwisho wa siku lazima Mapenzi ya Mungu yatimizwe.

Je, wewe unatimiza mapenzi ya Mungu?
 
Ni watakatifu tuu ndio waliotimiza mapenzi ya Mungu
 
kuandika mada na ikachangiwa pia ni mapenzi ya mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…