Mapenzi ya kuchuma

MpajiGiva

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2014
Posts
272
Reaction score
63
Katika ulimwengu huu ambapo UBINAFSI umetawala mioyoni mwa watu ambapo hata kwenye Mahusiano watu wanaangalia mwisho wa yote watajinufaisha vipi na Mahusiano hayo.Si wanawake si wanaume,wote wanazipigia hesabu nafsi zao kwanza.Imekuwa "Mimi kwanza,Yeye baadae".UBINAFSI huu umepelekea watu wengi kutoonja ladha ya Mapenzi badala yake wanaishia kuonja ladha ya Ngono.Kupata Mapenzi umekuwa mtihani,wengi huishia kupata Ngono.Inasikitisha kuona watu wanaingia kwenye taasisi nyeti kama Ndoa huku mioyoni wanajiwazia wao kwanza.Kwa mwendo huu,si ajabu kusikia Kukosa furaha ya kweli,Hofu ya kusalitiwa na Kuvunjika kwa Ndoa (Mahusiano) vikishika kasi.Wanawake wanaishi kwenye ndoa kwa dhamiri za kikahaba(kuchuma) ,Wanaume wanaishi kama wanaoishi kwa kununua Makahaba(Ngono).Yote hayo ni matokeo ya "Mimi kwanza,Yeye baadae".Na Yote ni kwa sababu Mahusiano mengi hayana chachu ya PENDO LA MUNGU.Pendo ambalo hukausha na kuutowesha UBINAFSI moyoni na kumfanya mtu asiwe mwenye kutafuta mambo yake mwenyewe.Pendo lisilo na chembe ya unafiki.Pendo lililojaa uvumilivu na ustahimilivu ktk hali zote.Hivyo uonapo ubinafsi unakithiri,haina haja ya kutaabika kutafuta nani mchawi,SABABU NI KWAMBA HAKUNA CHACHU YA PENDO LA MUNGU MIOYONI MWA WAHUSIKA HIVYO HALI YA UBINAFSI KUZITAWALA NAFSI ZAO NA KULETA UHARIBIFU.DHAMIRI YA MTU ISIYO NA CHACHU YA PENDO LA MUNGU HUGEUKA NA KUWA YA MNYAMA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…