Mapenzi bwana

Sinoni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Posts
7,045
Reaction score
12,537
Kama penzi ni pepo aliyesema hakuzua,
Penzi kweli likiwepo maisha huwa muruwa,
Wawili wapendanapo dunia huwa maua,
Popote ulipo wewe moyoni sitakubagua ....


Ctrl+c = Ctr+v
 
mapenzi bila pesa ni sawa na kuotesha mbegu bila kumwagiliwa
 
Pesa ndio ufunguo malaya ( master key). Ukiwa nazi utafungua kila kitasa.
 
Mapenzi kitu ajabu,
yakutia bumbuwazi
Yakufanya uwe bubu,
kujibu huwa huwezi
Shubiri kwako zabibu,
na vitamu huviwezi.
 
Mapenzi ni kupendana
Sio kuvumiliana
Pasiwe kudanganyana
Kauli iwe mwanana
Usipige danadana
Uipokee amana
WEWE NDIWE WA PEKEE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…