yello masai
JF-Expert Member
- Jan 8, 2016
- 3,635
- 3,658
Salaam wakuu.
Nijuavyo mimi watu huingia kwenye mahusiano ya kimapenzi ili kupata faraja, hivyo hutegemea kupata furaha na kuwapa furaha wenza wao. Wengine wamekuwa wakifanikiwa katika hilo na wengine mambo yanaenda kombo.
Kuna mahusiano mengine ukiwemo unakuwa unahisi kama unaidhurumu nafsi maana nafsi inaeza kuwa inakwambia hapa si sahihi au kuna udanganyifu lakini bado wang'ang'ania tu na kujikuta unaishi kama mlinzi wa mwenzio.
Nitatoa mfano kidogo wa jamaa yangu ambaye naona anaishi kama mtumwa sababu anatumia muda mwingi kumchunga mwenzie zaidi ya muda anaotumia katika mambo ya msingi.
**Huyu jamaa anamchukua demu anayetoka katika familia duni ambako kwao mlo mmoja ni jambo la kawaida. Lakini demu anaishi na mama ake wa kambo katika nyumba yao ya urithi ambako wamewapangisha na watu wengine.
* Sasa tatizo linakuja hivi: Jamaa kila akipiga simu anasikia sauti za kiume maana ile nyumba vyumba vipo ndani kwa ndani. Sasa ugomvi wao hauishi maana kila jamaa anapopiga simu na kusikia hizo sauti humaind sana na ndo ugomvi huanzia hapo.
Jamaa hatulii amekuwa mtumwa wa simu, anashinda anachat na simu ukimuuliza anakwambia anataka asimpe demu wake chance ya kuongea na hao wapangaji wa kiume.
** Kitu kingine, huyu jamaa alipoanzisha mahusiano na huyu demu alimkuta akiwa na jamaa mwingine, akafight kuvunja mahusiano hayo alijitahidi kwa kiasi flan kama kumbadilishia demu namba za simu na kumwambia ampigie simu jamaa kumueleza kuwa hamuhitaji tena.
* Lakini jamaa hakuishia hapo akataka huyu demu ampeleke kwa yule X wake amweleze kuwa hamuhitaji tena na amtambulishe mchumba wake mpya maana jamaa anadai hakuwa na uthibitisho zaidi kuwa yale mahusiano yamevunjika kweli. Lakini demu amekataa kata kata kuwakutanisha anadai yule X wake ni mkorofi sana. Anamwambia jamaa eti we niamini tuu mi siwezi kuendelea naye, jambo ambalo linamuumiza sana jamaa.
** Kitu kingine kinachomuumiza jamaa ni kwamba demu huwa hataki kumtembelea wala kutoka na jamaa kwenda katika matembezi. Lakini akimuita kumgegeda hapo fastaa anakuja na mara nyingi demu anaomba mwenyewe mgegedo. Hili jambo linampa walakini jamaa yangu maana hutamani sana kujiachia na demu wake. Lakini huyu demu sio expensive sana yaani si mpiga mizinga.
Sasa nikiangalia maisha anayoishi rafiki yangu, anaishi kwa wasi wasi sana. Saa sita usiku anapiga simu kuangalia kama kweli demu kalala au anajiachia na wapangaji au yuko nje anapunga upepo maana wana tabia ya kutoka nje usiku kupunga upepo kwa sababu hawana umeme.
Huwa najiuliza haya ni mapenzi au ni karaha? Kuna raha yoyote hapo au ni kuidhurumu nafsi? Je ushawahi kuwa na uhusiano na mtu anayeishi mazingira magumu kama hayo na je ilikuaje? Je ni sahihi kuendeleza uhusiano wa kuchungana kama mbuzi na kuishi bila amani kwa kuwaza mwenzako anafanya nini kila dakika ipitapo?
Nimeamua kuvaa viatu vya rafiki yangu sababu amenichosha kwa kuomba ushauri. Naamini hapa nitapata madini ya maana nimpelekee kama yalivyo.