Mapendekezo ya Kuboresha Mfumo Mpya wa Ajira Portal

Mapendekezo ya Kuboresha Mfumo Mpya wa Ajira Portal

Cybercurex

Member
Joined
Jan 19, 2023
Posts
98
Reaction score
238
Hivi karibuni kumefanyika maboresho ya mfumo wa kuomba ajira , Ajira Portal.
Pamoja na maboresho haya, kuna baadhi ya feature muhimu ambazo zimeondolewa na kusababisha changamoto kwa watumiaji. Maeneo ya kuzingatia ni kama ifuatavyo:

1. Job Categories
Zamani kulikuwa na job categories ambazo zilifanya iwe rahisi kwa mtu kuchagua nafasi za kazi zinazomhusu.
Mfumo mpya unaorodhesha nafasi zote kwa pamoja, jambo linalofanya kutafuta kazi maalum kuwa gumu zaidi.
Vilevile, job categories zilisaidia kujua ni nafasi mpya zipi zimeongezwa kwenye kila kundi.

2. Kurudi kwenye Ukurasa Navigation Issue
Wakati unavinjari(browse) nafasi za kazi, mfano ukiwa kwenye ukurasa wa 50, ukirudi nyuma mfumo unakurudisha ukurasa wa kwanza kabisa.
Hii inalazimisha mtumiaji kutafuta tena ukurasa alioacha, jambo linalopoteza muda na kurudisha nyuma ufanisi.

Tunaomba wahusika waangalie changamoto hizi ili kuboresha zaidi mfumo na kufanya uzoefu wa mtumiaji kuwa bora.
 
Kwenye job categories umeongea point sana kiufupi wameharibu sana hicho kipande
 
Back
Top Bottom