Hiyo inakua kama mfano, hata kama alieleta mada sio muhusika mkuu, inakuwa ni mojawapo ya kuwaelimisha watu, wanaokutana na hali kama hiyo, pengine wengine wapo kwenye madhila kama hayo(kutokana na mada iliyowekwa) tatizo huwa wanashindwa kuyatoa yanayowapata au yaliyowapata, sasa mtu anapoleta mada ya uongo sioni kama kuna tatizo.
Ni moja ya kufikisha ujumbe, upo?
Tatizo lipo mkuu! baadhi ya members wanaghaili kutoa ushauri/michango wakishajua aliyewasilisha maada uhusika aliovaa hauna ukweli,(ushaidi upo hapa hapa mmu). Ushauri wangu ni kuwa kama unawasilisha maada hata kama haina ukweli iwe inahusiana na maada zako za nyuma ili iendane na ukweli kukuhusu wewe la sivyo tuelezane kuwa chochote kinachowasilishwa hapa ni kwa ajili ya kuelemishana no matter uhusika wa aliyewasilisha kwa sababu nimeshuhudia hapa hapa mmu mmoja akipewa za uso baada ya kuanzisha topics akiwa mhusika lakini watu wakasearch na kukuta uhusika wake kwenye hizo topics hausiani.