Maoni yangu kwa wanachadema na upinzani kwa ujumla

Mpunilevel

JF-Expert Member
Sep 14, 2015
3,140
1,871
Ndugu wanachadema na upinzani kwa ujumla salaam!

Toka mheshimiwa Rais Magufuli aingie madarakani, kasi yake ni kubwa katika kurudisha nidhamu ya watendaji serikalini.
Anapambana na kile kitu kinachoitwa business as usual ambacho kimepigiwa kelele kwa muda mrefu sana.
Hii ni dalili njema kwa taifa letu, kwani madhira yaliyokua kero kwa wananchi yanaelekea kupata tiba mujarabu.

Cha msingi sasa ni kumpa ushirkiano madhubuti na si kukwamisha juhudi hizi, kwani Ndio kilio chetu kwa miaka mingi. Kifupi upele umepata mkunaji, na sote tunajenga nchi moja, Tanzania.
Jana Arusha kongamano la wasomi na wafanyabiashara ni jambo jema kuhusu uchumi wetu. Nategemea litakuwepo kongamano lingine litakalohusisha wakulima /wafugaji na wafanyakazi.

Angalizo :
Nategemea mje na sera mbadala na zenye tija kwa taifa na si kama iliyokua jana kwa kushambulia juhudi za Rais Magufuli kwa kutaka kutengeneza tension kwa raia ambao asilimia karibu 80%wanakubaliana na kazi ya Rais Magufuli.
Naamini wasomi mnao wa kutosha, elekezeni jamii namna bora ya kilimo, utunzaji wa akiba, ufugaji wenye tija, umuhimu wa kulipa kodi, elimu ya uraia na mengineo mengi mazuri.
Kwa kufanya hivyo tutafikia malengo ya kuikwamua nchi haraka.
Suala la kukosoa na kuleta mawazo bora mbadala dhidi ya serikali, 100%inakubalika na si kubeza bila ya wazo chanya.

Ikumbukwe wananchi nao hupima kauri na matendo ya wanasiasa. Watanzania kwa sasa wanaelewa mbivu Na mbichi za wasiasa.
Si wa kudanganyika tena.

Rais Magufuli kaonyesha njia tuliohitaji, sasa tuunge mkono juhudi hizi. Siasa za matukio zinapitwa na wakati.

Mwisho nampongeza diwani na meya jacob wa kinondoni kwa kwenda sambamba na juhudi za Rais Magufuli kwa vitendo.
Huyu ni mfano wa kuigwa, na wakosoaji wengine ndani ya upinzani.
Ni mtizamo tu, nakaribibisha michango.
 
Back
Top Bottom