Tangu ile ripoti ya kwanza na hii ya leo, Kamati zote mbili zimewasaidia watanzania kubaini kuwa CCM si ya kuaminika, haifai kuongoza nchi, haina dhamira ya dhati ya kusaidia taifa hili, na viongozi wengi wa CCM ni wapiga dili.
Serikali ya CCM ndiyo iliyoileta kampuni ya Accacia nchini, wakaipa mgodi bila kusajiliwa BRELA, CCM ikatumia idadi kubwa ya wabunge wake bungeni kuruhusu wawekezaji wa madini (including Accacia) kuchukua 96% ya gross income na taifa kuambulia 4% tu.
Mambo haya yaliyoongelewa kwenye kamati leo na ile kamati ya kwanza, yamekua yakiongelewa na vyama vya upinzani kwa miaka mingi lakini CCM na wafuasi wake wakiwabeza wapinzani. Leo Kamati hizi zinaongea lugha ileile iliyoongelewa na upinzani kwa miaka mingi, wafuasi walewale wa CCM waliobeza ndio wako mstari wa mbele kushangilia. Upuuzi wa kiwango cha shahada ya uzamivu.!!
Labda niwaambie tu kuwa chanzo cha yote haya si makinikia, wala si Accacia kutokusajiliwa. Chanzo cha yote haya ni mikataba ya hovyo iliyopitishwa na wabunge wa CCM kwa wingi wao bungeni. Kwa hiyo kama tunataka kusaidia taifa hili dawa si kukenua meno kumsifia Rais, dawa ni kurudisha mikataba yote bungeni, ikafumuliwe na kusukwa upya kwa maslahi ya taifa. Vinginevyo tunapoteza muda kusikiliza vitu visivyotoa promising future.
[HASHTAG]#NiniKifanyike[/HASHTAG]:
1. CCM na serikali yake wanapaswa kuwaomba radhi watanzania kwa kushiriki kuiba au kusaidia wezi wa kimataifa kuiba rasilimali za nchi (madini ni kielelezo tu, lakini CCM wameuza rasilimali nyingi kuliko madini. Sekta ya utalii, uvuvi, gesi huko balaa ni kubwa zaidi).
2. Serikali ya CCM wakubali kubeba lawama zote zinazotokana na hasara hii kubwa kwa taifa.
3. Mikataba yote ya madini na mikataba mingine inayohusu rasilimali za taifa (kama utalii, gesi, vitalu vya uwindaji, Uvuvi, nishati etc) irudishwe bungeni ikafumuliwe na kusukwa upya kwa kulinda maslahi ya taifa.
4. Naibu Waziri wa Madini Dr.Medard Kalemani (ambaye alibakizwa baada ya Waziri Muhongo na Katibu Mkuu kuondolewa) nae aondolewe. Ikumbukwe Kalemani alikua wizara ya nishati na madini tangu mwaka 1999 akishika nafasi mbalimbali wizarani hapo. Amekuwa Afisa Mwandamizi wa Sheria (Seniour Legal Officer), Mkurugenzi wa sheria kwa nyakati tofauti. Maana yake ni kwamba alihusika kwa namna moja au nyingine na mikataba hii mibovu iliyotuingizia hasara kama taifa.
5. Mwaka 2020 CCM waamue wenyewe kuondoka madarakani kwa kutosimamisha mgombea Urais, maana wamepoteza uhalali wa kuendelea kuongoza. Vinginevyo wananchi wawaondoe madarakani kwa nguvu ya kura.!
Malisa GJ