Maoni: Chaguzi za Marudio zifutwe

Maoni: Chaguzi za Marudio zifutwe

Toosweet

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2012
Posts
2,140
Reaction score
1,982
Kwenu,

Inapotokea mbunge au diwani amefariki tunafanya uchaguzi wa marudio. Hii ni gharama ambayo pengine haina bajeti.

Kwa upande mwingine, akitokea mbunge au diwani 'ameenda kumuunga mkono' Rais Magufuli kwa kukimbilia CCM, tunafanya uchaguzi pia.

Hivi kuna lazima gani kuitisha uchaguzi mdogo ambao kwa kawaida hugharimu fedha na maisha ya watu na hasa wanachama na viongozi wa upinzani? Sijawahi kuona au kusikia mtu yeyote anayemuua mwanachama na kiongozi wa upinzani akikamatwa.

Mauaji na utekaji hufanywa kwa kupangwa lakini wahusika hawakamatwi. Wanaokamatwa ni upande wa wanaouawa. Sasa tuna raia first class na wengine third class. First class hawakamatwi wala kufungwa

Serikali ilete muswada au marekebisho ya sheria ili mbunge au diwani kutoka chama chochote akihama chama wakati bado anahudumu, aapishwe mbunge au diwani aliyefuatia kwa wingi wa kura na kusiwe na haja ya marudio ya uchaguzi.

Tabia zinazoendelea kwa sasa za hama hama, zinasababisha wapigakura kutokuona umuhimu wa kupiga kura.

Ni mawazo yangu tu.
 
Paka akiongea panya wananyamaza ama kukimbia na kupotea kabisa.
 
Kwa upande mwingine, akitokea mbunge au diwani 'ameenda kumuunga mkono' Rais Magufuli kwa kukimbilia CCM, tunafanya uchaguzi pia.
Na hata akienda upinzani tunafanya pia uchaguzi vilevile,sasa jenga hoja yako...
 
Laleni ni mda wangu huu..
unnamed (2).jpg
 
Ni upuuzi wa kiwango cha juu kushiriki uchaguzi unaowaacha na vilema vya kudumu na udhalilishaji wapinzani eti kuungopea umma na dunia kwamba ccm inakubalika. Sioni haja ya wapinzani wa kweli kuendelea kushiriki chaguzi zinazowaachia jinamizi la kudumu maishani. Ni muda sasa kuwaachia ccm wafanye uchaguzi wenyewe, na huko mbeleni wataishia kwenye chaguzi za kikabila na kikanda.
 
Mkuu hauoni kuwa kwa kusema mbunge au diwani akifariki mshindi wa pili ashike nafasi automatically kutasababisha wimbi la washindi wa pili kuwaua viongozi hawa ili wao watawazwe?
 
Mkuu hauoni kuwa kwa kusema mbunge au diwani akifariki mshindi wa pili ashike nafasi automatically kutasababisha wimbi la washindi wa pili kuwaua viongozi hawa ili wao watawazwe?
Hiyo ni nadharia zaidi inawezekana
 
Hakika kuanzia Leo sina imani na mbunge yoyote ile pale atakapojinadi kuwa atanipigania kutuletea maendeleo.Wabunge wametufanya wanyonge Wa nchi kama mtaji wao wakulipwa mabilioni ya FEDHA ambazo ni kodi za watanzania masikini Kwa KUKUBALI KUJIUZULU ili walipwe Mabilioni ya kodi zetu.Heko ccm Kwa yote hayo.
 
Mkuu tena Hilo la kulipwa Wajiuzulu ata lisikuumize sana kwa vile halina uhakika, Vuta picha Huo mkwanja wa Kuandaa Chaguzi mpya Kwa majimbo yanayokuwa Wazi, Mimi nasema ivi Usalama wa Taifa waingilie kati kuchagua hawa viongozi haswa ktk nomination
Huu ni Ulimbukenu mkubwa kabisa wa Wabunge wakitegemee kubebwa na Mkuu aliepo, Ivi huwezi Kumuunga mkono Rais mpaka Uhame na chama na kujivua ubunge? Huu ujinga hauvumiliki kabisa mimi sipo Chama chochote ila Hawa washezi Hawajui uchungu wa Kodi zetu sisi wavuja Jasho.
 
Namchek tu diwani niliyemchagua, kabla ya kutangazwa tulivyopigwa mitama na polis afanye huo ujinga. Sitakubali, sitakubali.
 
Wimbi al kuhama kutokana chama kimoja kwenda kwingine limezoeleka wakati wa uchaguzi.Wimbi hili la sasa ambalo limekikumba chama kikuu cha upinzani ni la aina yake.
Kwanza wanaohama karibu wote wanatoa sababu ileile.
Jambo la pili,pamoja na vyuma kukaza wanaohama wanaacha mishahara minene ya ubunge,posho na marupurupu kibao.
CDM na UKAWA wamegoma kushiriki uchaguzi wa marudio na kinachotokea watu wanajiuzulu kutoka katika ngome zao.Je hii haiwezi kuwa hesabu ya kuwafanya wafute uamuzi wao wa awali?
Ni kweli wanaoondoka hawaoni hasara wanayosababisha kwa Taifa?
 
Ukiona mtu baki kaukana ubunge alioenyea tena kwa mapambano makali na dola anaamua kuwatelekeza wananchi waliomchagua wakikesha kulinda kura,pia kuacha marupurupu yote ya ubunge sababu eti anamuunga mkono raisi ujue kuwa jua limechomoza kutokea magharibi kuelekea mashariki.
Wabunge hao wajue wamegeuzwa manamba,changudoa wa kisiasa,wamekosea wananchi na taifa kwa ujumla na kuizika demokrasia ya kweli.
Lakini historia itawahukumu,sitashangaa makaburi yao kuzungushiwa minyororo ya jela hata ahera.
 
Kwa haya yanayoendelea ya kununua wanasiasa na kisha kuingiza nchi kwenye uchaguzi,yataka moyo sana kwa wafadhili kutoa hela za walipa kodi wao kusaidia watu wasiojitsmbua.

Yaani ni sawa na wewe umkute ombamba barabarani ukampa chochote kumsaidia alafu baadae unamkuta baa kalewa chakari kisha kesho yake upite maeneo yale yale umkute akuombe tena hela na bado uwe na moyo wa kumpa.

Nina hakika hawa watu wanatudharau sana sema sheria na taratibu haziruhusu wao kuingilia mambo yetu ya ndani.

Ikifika mahali mkaona wanapunguza misaada au hawatimizi ahadi zao basi tusiwalamu maana hata katika nchi zao masikini wapo.
 
Back
Top Bottom