Maofisa wawili wa TRA mbaroni kwa tuhuma za uhujumu uchumi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Maofisa wawili wa Mamlaka ya mapato Tanzania, TRA, kituo cha Tunduma wamefikishwa katika hamakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mbeya na kuunganishwa na watuhumiwa wengine saba katika kesi ya uhujumu uchumi, wakituhumiwa kushirikiana kula njama za kuagiza na kuingiza nchini samaki kutoka nchina bila kibali wala kuwalipia ushuru.

Watuhumiwa hao, Ibarahim James na Lugano Mwakapala wote wakiwa ni maofisa wa TRA katika kituo cha Tunduma mkoani Songwe wamepandishwa kimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mbeya na kuunganishwa na watuhumiwa wengine saba kisha kusomewa mawili ya kuagiza na kuingiza nchini samaki bila kibali na pia kuingiza samaki hao nchini bila kuwalipia ushuru.

Watuhumiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Joseph Mushi ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa samaki jijini Mbeya, Said Omary Sisige,Agripina Benjamin, Andrew Ngachango, Pius joseph, Said Swed Ramadhan na Shaaban Sankwa.

Watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi na badala yake wakili wa utetezi, Ladslaus Rwekaza akaiomba mahakama hiyo kuharakisha mchakato wa kupeleka jalada la watuhumiwa hao mahakama kuu ili maombi yao ya dhamana yaweze kufanyiwa kazi.

Wakili mwingine wa utetezi, Victor Mkumbe akaieleza mahakama kuwa anaishangaa serikali kwa kuwafungulia kesi nyingine wateja wake wakati kesi hiyo ilikwisha tangu Januari 24, mwaka huu baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kutumia sheria ya forodha kutaifisha magari matatu ya watuhumiwa sambamba na kuwatoza faini ya zaidi ya shilingi milioni 3.97.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Michael Mteite amesema jalada la watuhumiwa litafikishwa mahakama kuu siku ya Ijumaa ya Februari 24, mwaka huu kwa ajili ya utaratibu wa dhamana na akaahilisha kesi hiyo hadi machi 7, mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo.

Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom