Maofisa wa Urusi wapingana na kauli ya Trump kuhusiana na Iran,wasema Iran ni wasafi

mcomunisti halisi

Senior Member
Jan 17, 2017
103
328
Siku ya jumatatu Kremlin walitoa taarifa rasmi kupingana na kauli ya Rais wa US Donald Trump aliyoitoa hivi karibuni kuhusiana na Iran kwamba ni nchi namba 1 duniani kwa ugaidi.

''Hatukubaliani na maana hiyo,''msemaji wa Rais wa Urusi alinukuliwa Dmitry Peskov

''Nyie nyote mnajua kwamba Urusi wanafurahia mahusiano mazuri na Iran,tunashirikiana kwenye masuala mbalimbali na tunashukuru kwa mahusiano yetu thabiti ya kiuchumi,tunategemea yataenda mbali zaidi.

Mkutano baina ya Rais wa Urusi Vladimir Putin na rais wa Iran Hassan Rouhani unategemea kufanyika hivi karibuni.

''Mawasiliano kati ya Rais Putin na Rais Rouhani yanaandaliwa,tutawajulisha tarehe kamili katika muda muafaka.''alisema Peskov

''katika maongezi hayo na uongozi wa Urusi pande zote mbili watajadili vipengele muhimu kuhusiana na siasa,biashara na sekta za uchumi.Ukiachana na haya,mambo yatakayopewa kipaumbele zaidi ni kuhusiana na ajenda ya kanda ya mashariki ya kati kama vile hali ndani ya Afghanistan ,matatizo ya bahari ya caspian na ugomvi wa Nagorno-Karabakh pamoja na hali nchini Syria.

pia balozi wa Urusi anayewakilisha UN Churkin amemtaka Rais wa US Donald Trump kutenganisha hisia zake na masuala ya kimataifa na amemtaka asiendeshwe na hisia zake za chuki dhidi ya China na Iran,.

''Katika masuala ya kimataifa ,unatakiwa utenganishe hisia zako,kile unachotaka kukiona na yale unayotegemea kuyaona kutoka nchi nyingine.''alisema Churkin

'Hizi vilio kuhusiana na jaribio lililofanywa na Iran la kurusha Balistic Missile ,hakika nimeshangaa sana nilivyosikia hata wataalamu wa USA walizungumza kwenye chombo cha habari cha CNN na kuyaita ni ya ukiukwaji wa maazimio ya baraza la usalama la umoja wa mataifa.

''UNSC wameitaka/wito Iran na hawajawakataza Iran kutorusha Ballistic missiles na hata kama wangerusha makombora yenye uwezo wa kubeba vichwa vya nyuklia kwanza inabidi yathibitishwe na siyo kuanza kupiga makelele''-Churkin Balozi wa Urusi UN

'' Hivyo ni wito tu na siyo katazo,Kitaalamu na kisheria huwezi kusema walikiuka makatazo yoyote yale' ya UNSC-balozi wa urusi UN
 
Iran anawezaje kuwa Msafi? Alishasema anampango wa kuifuta kwenye ramani Israel,Amesema anafadhiri vikundi vyote vya kigaidi vyenye nia ya kupigana na Israel, Anaiba tech nyingi na kudai ni local made raia wake wameshikwa na wana kesi karibu dunia nzima za kusafirisha mali zilizokatazwa au kuzuiliwa na vikwazo... Usuri anasema nini huku anapokea mshiko takrima kutoka kwa iran.. Iran amefadhiri magaidi waliolipua mabomu katika nchi zenye waumini wa Sunni karibu Dunia nzima.. Me Nachopenda Iran Iishi kama Nchi zingine tu za Kiislam sioni tatizo dunia ikiwa na amani yake tu... Tatizo lao maadhimio yao hayaishi Wananchi wanapata Shida sana huko Iran na pamoja na vikwazo kupunguzwa ambapo wananchi walifurahia sana vilipopinguzwa ila bado wamebanwa maisha yao ni duni mno wanalalamika... Kama Wananchi wanalalamika iweje Russia awasemee?
83360.adapt.470.1.jpg

"To Live in Tehran You Have to Lie": Revealing Hidden Lives in Iran
 
Tuliwaambia mashabiki wa Obama kuwa mkataba na Iran ulikuwa mbovu hawasikii,
Sasa unaona Iran wana cheza na maneno tuu, eti ule ulikuwa "wito" sasa mkataba gani una base kwenye wito na si makubaliano? na kutengeneza nyukilia hawata acha.
Hahahaha, that was dumb deal.
 
Us anaijua sana mashariki ya kati kuipa nguvu iran baada ya vikwazo vya muda mrefu ni kutaka kuvunja influence ya sunni. Maana wasunn ndio tishio kubwa kwa US nakupa mafano uzao wa alqaeda,muslim brotherhood na isis ni chimbuko la sect ya sunni tena power za kina qatar na saudi ndio financers wakubwa sasa hii inawatisha america wakaona wampe nguvu iran ili ideology ya shia ipate nguvu na msunni aanze kupambana na mshia. Na hilo wamefanikiwa emagine vita ya yemen etc sasa ndio ujue kuondolewa vikwazo iram stratrgy ni kuivuruga middle east
 
Ehehehe
Wakati unasema hivo wameruhusu Iran ashikilie affairs za middle east Iran huyo huyo hawasaidii Us ana wasidia Urusi, angalia ishu ya Syria angalia biashara ya silaha kati ya urusi na Iran,
Bado Us wali imburse mabilioni ya pesa na bado lengo la kupinguza nuclear halija fikiwa
Yaan wana mu empower mtu ambaye hawawezi ku m control.

Ukisoma ule mkataba, Iran ka gain na Us kapoteza
 
Iran anawezaje kuwa Msafi? Alishasema anampango wa kuifuta kwenye ramani Israel,Amesema anafadhiri vikundi vyote vya kigaidi vyenye nia ya kupigana na Israel, Anaiba tech nyingi na kudai ni local made raia wake wameshikwa na wana kesi karibu dunia nzima za kusafirisha mali zilizokatazwa au kuzuiliwa na vikwazo... Usuri anasema nini huku anapokea mshiko takrima kutoka kwa iran.. Iran amefadhiri magaidi waliolipua mabomu katika nchi zenye waumini wa Sunni karibu Dunia nzima.. Me Nachopenda Iran Iishi kama Nchi zingine tu za Kiislam sioni tatizo dunia ikiwa na amani yake tu... Tatizo lao maadhimio yao hayaishi Wananchi wanapata Shida sana huko Iran na pamoja na vikwazo kupunguzwa ambapo wananchi walifurahia sana vilipopinguzwa ila bado wamebanwa maisha yao ni duni mno wanalalamika... Kama Wananchi wanalalamika iweje Russia awasemee?
83360.adapt.470.1.jpg

"To Live in Tehran You Have to Lie": Revealing Hidden Lives in Iran
Unaweza kusema Israel ni msafi?mauaji anayofanya huko Palestine,alikuwa mfadhili mkuu wa Isis,hata uundwaji wa vikundi vingi vya kigaidi mfadhili ni israel
,una uhakika wa Irani wanapata shida kama wapalestine wa Gaza waliozingirwa na waisrael? Au wanaishi maisha kama tunayoishi tanzania?au ulishawahi kusikia wanakufa njaa?tuache mihemko .
 
Mkuu Mgogolo wa Israel na Palestina nadhani huujui hata kidogo... Israel ilipounda Taifa lao Waarabu hawakutaka walitaka wale Wayahudi wenyeji waliokuwepo tokea enzi na enzi ambo walijaribu kuwaondoa lakini walishindwa... Waingereleza walipoondoka Israel baada ya Azimio la League of Nation kwa sasa ni United Nation. Kulikuwa na Waarabu original from Egypt,Jordan na Saudia na hao watu wana asili kabisa ya sehemu hizo hata Majina fuatilia Asili ya Wapalestina utaamini. na wengi zaidi ni from Misri..

Waarabu wengi waliwauzia Wayahudi ardhi its same kama Dar Es Salaam Wazaramu walivyouza maeneo yao ati waamue waweke kikao na kuondosha Wavisiwani,wabara,waarabu na wahindi kuwa wanataka ardhi za Mababu zao.. Kwa upande wa wayahudi waliona hiyo haiwezekana wakawalipa pesa na kupishwa... Kuna Sheria wapalestina wamewekeana sasa Muarabu yeyete asize ardhi kwa Myahudi the issue Myahudi ana pesa ndefu na wengi waliuza na kukimbilia nje ya nchi kwa pesa ndefu waliyoipata... ila wajinga bado hudai Ardhi ni ya Muarabu je Israel angechukua bila fedha sijui ingekuwaje? ila kuna sehemu za kiusalama amezizuia kimabavu kwani tishio ni kubwa sana na Matamko ya Waarabu hayaishi... Mgogolo ni mkubwa sana ndio maana kuna wakati Misri alitaka awape Sinai wahamie wote wajengewe kila kitu na Israel wakagoma na kuendelea na vitisho vyao mbuzi kuwa wanataka Israel yote...

Waziri Mkuu Yitzak Rabin aliamua awape waarabu Gaza ili waache kelele na Ugaidi waishi vizuri lakini Matokeo yake yalikuwa ni mabaya zaidi Gaza ikawa kama kitovu free cha kuisumbua Israel kwa kila namna ya Ugaidi Utawala wa umoja wa Wapalestina ukafa ukawa Utawala wa Hamas unaofadhiliwa asilimia nyingi na Iran, NaIran lengo lao kuu ni Ugaidi tu dhidi ya Israel na hilo halina ubishi.

Sasa Linapokuja jambo la kigaidi limetokea Israel ilikuwa ikitoa Onyo tu ikafikia wakati ugaidi ukazidi ikaanza kuwawekea vikwazo ili kuwafanya watulie lakini wapi wakazidi uchochezi Israel subra ikawashinda ikawachapa wakaongeza jeuri ati wanaweza kupigana the Issue wakawa wanajificha kwa raia wao Israel akaona hamna Jinsi akawachapa tu maana vita haina mtoto as if amebeba silaha... kama Vita ya Hamas huijui ni bora tu Unyamaze last one walikuwa wanatumia propaganda tu na picha za zamani na media hadi Israel ikastopisha lakini lengo ilikuwa ni kuirejesha Gaza katika Ramani ya Israel kimakazi. So Kuhusu Gaza watu wote wanaopewa kusuluhisha wanaona Hamas ni Tatizo... na wewe kama hutambui fuatilia uelewe usisikie tu juu juu bila kuchunguza Watoto mbona hata Israel walikufa kwa rocket zisizo na Shabaha za Hamas.! UN yenyewe ikifika suala hilo inafyata.

Kuhusu ISIS Ukisema inafadhiliwa na Israel haiwezekani ikawa 100% unapokuwa mpakani na jirani yako yupo vitani unakila sababu ya kuwa Neutral problem Syria yupo upande wa Iran na Hezbollah unafikiri Israel atashika upande upi? au ungekuwa wewe ungekaa upande upi? huyo Isis hana Ugomvi na Israel na anayepigana nae ni Adui wa Israel. so take my point and ishi
 
Mkuu hebu soma historia ya George habbash na wadie haddad ni kwanini waliingia katika harakati na mambo yepi yaliwachagiza wakaingia kwenye harakati ndio utajua

Kuhusu Syria/Isis ,Israel hataki Assad ashinde sababu ushindi wa Assad ni ushindi wa Iran na kati ya Isis na Iran Israel yupo kwa Isis sababu Iran ndiye adui yake mkubwa

Kuna taarifa zinasema Israel alikuwa anachelewesha vita Syria ndio maana USA licha ya kuisema Isis lkn walikuwa wanawaacha wajitanue
 
Back
Top Bottom