Maofisa Usalama wauaji, yawakuta

Maofisa Usalama wauaji, yawakuta

Simba321

Member
Joined
May 19, 2017
Posts
22
Reaction score
84
Tarehe 16 January 2017 Mahakama Kuu nchini Bangladesh ilitoa hukumu kwa maafisa ujasusi 26 wa nchi hiyo kunyongwa mpaka kufa,. Adhabu hiyo kwa wafanyakazi 26 wa usalama wa taifa nchini Bangladesh ya kunyongwa mpaka kufa inatokana na kuhusika kuwatesa, kuteka, kutia vilema na kufanya mauaji ya kutisha kwa wanasiasa wa "upinzani" wa nchi hiyo mwaka 2014 .

Mahakama ilielezwa kuwa wafanyakzi hao wa idara ya usalama wa Taifa nchini Bangladesh hasa kitengo cha ulinzi wa Rais (National Intelligence) na kitengo binafsi cha ulinzi wa rais (State Intelligence) walishirikiana na wanasiasa wa chama tawala kufanya mauaji ya kutisha kwa wanasiasa wa upinzani... Maafisa hao wanatoka vitengo vya Ujasusi vya nchi hiyo ambavyo ni National Security Intelligence (NSI), Directorate General of Forces Intelligence (DGFI), Criminal Investigation Department (CID), Detective Branch (DB),Special Branch (SB), Police Bureau of Investigation (PBI)

Hili liwe funzo muhimu kwa maafisa usalama binafsi maana muda wa kujibu tuhuma mahakamani utasimama pekee yako sio aliyekupa amri, pia iwe fundisho kwa vyama tawala barani Afrika. Hakuna aijuaye kesho, na hakuna aliyejuu ya sheria, utatenda uhalifu na mauaji leo, utajiona upo salama, lakini wanaokufanya ujione upo salama watoka madarakani nawe utafika mbel ya sheria... .

Kwa bahati nzuri ulimwengu ni waajabu sana, wananchi popote pale kwa tukio lolote lile hata ufanyie gizani uamini hakuna aliyeona zaidi ya wewe na shetani wako, wao hutunza ushahidi, haijalishi ni miaka mingapi itapita, lakini subiri siku ukifikishwa mahakamani utashuhudia ushahudi wa kila aina, kuanzia maandishi, picha, sauti, video na wa ana kwa ana... Dunia haina siri...
Mahakama zilezile zilizoonekana kuwabeba watawala na majaji wale wale utashangaa siku hiyo zinaposimama kwenye haki (umma), na kuhakikisha udhalimu unaadhibiwa kwa haki.
 
Acha nao waionje ladha ya kile walichokuwa wanawafanyia wenzao
 
Tukiwajua waliomjeruhi Lissu moja kwa moja tutawapasua kama samaki anayeandaliwa kubanikwa, tunajuwa walitumwa na sizonje
 
Back
Top Bottom