HABARI Kijana mmoja rika la Morani wa kabila la Maasai, wilayami Kiteto mkoani Manyara aliyejulikana kwa jina la Sabaya Isaskar (31)mkazi wa Njaniodo, amekatisha maisha yake kwa kujinyonga hadi kufa akitumia kamba aina ya manila.
Kifo cha kijana huyu wa kifuaji Maasai kimevuta hisia kwa jamii huku ikielezwa kwa kabila la kimaasai mtu kujinyonga huwa ni nadra kwao.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Partimbo amethibitisha tukio la kijana huyo Morani wa Kimaasai kujinyonga, "Toka tulivyopata taarifa kuwa hili tukio limetokea tulipata mshtuko lakini niwashukuru walioshiriki toka mwanzo marehemu alipoonekana maeneo yale ya tukio hadi kumfikisha hospitalini"amesema Kimirei