Mansour Yussuf Himid ajiunga rasmi CUF (UKAWA)

Mansour Yussuf Himid ajiunga rasmi CUF (UKAWA)

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
MA1.JPG

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akimpongeza Mhe. Mansour Yussuf Himid baada ya kuamua kujiunga na chama hicho na kumkabidhi rasmi kadi ya CUF katika viwanja vya Paje, Wilaya ya Kusini Unguja.

Mansour alikua Mwakilishi wa Kiembesamaki Kabla ya kuvuliwa Uwakilishi na CCM. Mwaka 2000 hadi mwaka 2004, alikuwa Naibu Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, na kati ya mwaka 2004 hadi mwaka 2010 alikuwa waziri kamili katika wizara hiyo na baadaye mwaka 2010 hadi mwaka 2012, alikuwa Waziri wa Kilimo na Rasilimali. Kwa habari zaidi kumuhusu, soma=> CCM yamvua uanachama Mwakilishi wa Kiembesamaki, Mansoor Yussuf Himid
 
Another reinforcement combatant into UKAWA structure!
 
tunamkaribisha kwenye ukombozi UKAWA ni mwendo mdundo
 
Na ile kesi ya kumbambikia risasi iliyotungwa na magaidi ya ccm imeishia wapi?
 
Na ile kesi ya kumbambikia risasi iliyotungwa na magaidi ya ccm imeishia wapi?

ccm wameshashindwa siku zote njama za chafu chafu za shetani haziwezi kufanikiwa ccm walijua wanamkomoa kumbe ndo wamezidi kumwinua juu.
 
Na ile kesi ya kumbambikia risasi iliyotungwa na magaidi ya ccm imeishia wapi?

Serikali ya CCM haina akili, wanapofanya mambo hua hawajui kama baadae yatawaathiri. Hile kesi ilikua ni kama kesi nyengine wanazobambikiziwa watu bila ya (CCM) mwiaho wa siku kuthibitisha ukweli wa kesi hizo

Hii kesi ya Mansour ni kama ilivyo kesi ya Mashehe wa UAMSHO (Walikua wanataka Muungano wenye kukubalika na pande zote mbili bila ya kila upande kulalamika) lakini wakabambikiziwa kesi ya UGAIDI

Kesi ya Mansour pia inafanana na ile ya fundi seremala aliyembiwa amempiga risasi Padri Mushi na mwisho wa siku MaCCM wakashindwa kuthibitisha

Mansour alikua amefunga CCTV Camera katka nyumba yake na baadae mchezo wote umekuja kujuilikana na kesi yake imezimwa kimya kimya

Haya ndiyo mambo yanayowamaliza CCM
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom