Manispaa ya Moshi msiwaumize zaidi wafanyabiashara soko la Mbuyuni

Manispaa ya Moshi msiwaumize zaidi wafanyabiashara soko la Mbuyuni

Ndagullachrles

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
198
Reaction score
209
Manispaa ya Moshi msiwaumize zaidi wafanyabiashara soko la Mbuyuni

Februari 6 mwaka huu,wafanyabiashara katika soko la Mbuyuni Manispaa ya moshi walikumbwa na janga la moto ulioteketeza eneo kubwa soko hilo na kuwaacha wafanyabiashara hao mikono mitupu baada ya mali zao kuteketezwa na moto.

Huo ulikuwa ni moto wa pili baada ya ule wa Februari pili 2022 kuteketeza pia mali zao na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya soko hilo na bahati mbaya sana mpaka sasa taarifa za matukio haya mawili hazijawekwa wazi ni nini hasa chanzo cha matukio hayo.

Baada ya tukio hilo la februari 6 mwaka huu,manispaa ya moshi ilifanya jitihada za kulifanyia ukarabati mkubwa soko hilo lenye mkusanyiko wa watu wengi kwa kutumia mapato ya ndani ya manispaa na hatimaye hivi karibuni lilikamilika na kupima vizimba zaidi ya 700 pamoja na frem kwa wafanyabiashara wa nafaka na wale wa nyama.

Nimeamua kuandika uzi huu baada ya kilio cha wafanyabiashara wa nafaka na wale wa nyama(bucha)kuiomba manispaa ya moshi kuangalia upya kodi mpya iliyowekwa ya sh,300,000 kwa kila frem kwa mwezi kutoka sh,40,000 iliyokua ikilipwa na wafanyabiashara hao kabla ya kuungua kwa soko.

Wafanyabiashara hawa wanadai tangu kuungua kwa soko hilo hawajafanyabiashara yoyote na kibaya zaidi Taasisi za fedha zinawasumbua ili warejeshe mikopo waliyokopa kabla ya soko kuungua.

Kwenye barua yao ya Mei 19 mwaka huu kwenda kwa mkurugenzi wa manispaa ya moshi,Mwajuma Nasombe ,wafanyabiasara hao wanaiomba manispaa kuangalia upya mpango wake wa kuwatoza kodi kubwa bila kuangalia athari kubwa walizozipata kutokana na tukio moto huo.

Cha kushangaza manispaa ya moshi imeziba masikio na imetoa kitisho kwa wafanyabiashara hao kuwa kama hawako tayari kulipa kodi hiyo mpya basi waachie huizo frem ili kupisha maombi mapya 100 ya wafanyabiashara wanaozitaka frem hizo.

Hii imekaaje,watu wametoka kwenye mkasa mkubwa wa kupoteza mali zao,leo wanaambiwa kodi ni laki 3 kwa mwezi na kama hutaki pisha wengine,kaaazi kweli kweli
 
Back
Top Bottom