Manispaa ya Kigoma uozo mtupu

Haludzedzele

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,468
529
Kweli ualimu wito sio ajira mana watu wanafanya wanavyotaka tuu, nakatishwa tamaa sana na hii kada ya ualimu kimsingi Walimu wa kigoma manispaa tulioajiriwa 2012 hatujapewa barua za kupanda madaraja mpaka sasa ijapokuwa wenzetu wa halmashauri zingine wameshapew barua za kupanda daraja kuanzia Kigoma vijijini,Kasulu na Kibondo ukiachilia mbali mikoa mingine mingi kama Geita waliopandishwa mwaka jana Kahama mapema mwaka huu Makete nk.

Kuona hivyo tukashtuka na kuanza mikakati ya kufahamu ni kwanini sisi tuu manispaa tukaenda tsd wakasema mwaka 2015/16 hatumo kwenye bajeti hiyo ambayo kimsingi ndio bajeti yetu kwenda kwa Afisa utumishi majibu hayo hayo mmmmm kwenda kwa Mkurugenzi nae majibu hayo hayo tena kwa nyodo tumeona huko kote kumegota leo tumeenda kwa Afisa Elimu Mkoa nae anasema hana majawabu labda tumsubiri Katibu tawala mkoa ambae yupo kwenye uwashaji Mwenge Morogoro hivyo mtetezi hasa ni nani iwapo walimu hawapati stahiki zao? nimepata kizungumkuti sana leo hasa nchi ni moja mwaka wa kuajiriwa ni mmoja iweje kuwe na mambo kama haya?

kimbilio letu hasa ni wapi? tumesimama kidete kuhakikisha hatuendelei kuchezewa kama wanavyotaka kwa kufahamu haki haiombwi bali hutafutwa na ikibidi hulazimishwa kupatikana. Kwakweli wanajamvi naomba tupeane ujanja ni namna gani tunaweza kwenda sawa na waajiri wasiotambua stahiki za watumishi wao japo kwa Kigoma Manispaa mmmmm sidhani mana pameoza sana hawana utu kabisa. Mwenye namba ya Waziri Tamisemi naomba pamoja na Naibu wake labda baada ya ngazi zote ni kunyooka tuu kwa hawa kazi tuu inaweza saidia kwa kiasi fulani.

Tushikane mikono jamaani haya ni maisha yetu sote ahsanteeni na poleni kwa kusoma andiko lefu baada ya hapa mtasikia tuu kinachoendelea! KARIBUNI KWA MAWAZO
 
Kufanya kazi Kigoma ni kujimaliza,sio idara ya elimu tuu kotee ni majipu yaliyogeuka kansa
aiseee upo sahihi kabisa yani maisha yake ni magumu lakini pia hata stahiki za watumishi majamaaa yanakaza tuu sijui kunani ngoja nifanye mchakato niinuke tuu
 
aiseee upo sahihi kabisa yani maisha yake ni magumu lakini pia hata stahiki za watumishi majamaaa yanakaza tuu sijui kunani ngoja nifanye mchakato niinuke tuu
Andaa vile wanavyoangalia wakija kukagua,toa notes za kutosha,kusanya madaftari ya wanafunzi weka tick za kutosha
Ingia mtaani kusaka pesa hadi mambo yakiwa sawa
 
Kweli ualimu wito sio ajira mana watu wanafanya wanavyotaka tuu, nakatishwa tamaa sana na hii kada ya ualimu kimsingi Walimu wa kigoma manispaa tulioajiriwa 2012 hatujapewa barua za kupanda madaraja mpaka sasa ijapokuwa wenzetu wa halmashauri zingine wameshapew barua za kupanda daraja kuanzia Kigoma vijijini,Kasulu na Kibondo ukiachilia mbali mikoa mingine mingi kama Geita waliopandishwa mwaka jana Kahama mapema mwaka huu Makete nk.Kuona hivyo tukashtuka na kuanza mikakati ya kufahamu ni kwanini sisi tuu manispaa tukaenda tsd wakasema mwaka 2015/16 hatumo kwenye bajeti hiyo ambayo kimsingi ndio bajeti yetu kwenda kwa Afisa utumishi majibu hayo hayo mmmmm kwenda kwa Mkurugenzi nae majibu hayo hayo tena kwa nyodo tumeona huko kote kumegota leo tumeenda kwa Afisa Elimu Mkoa nae anasema hana majawabu labda tumsubiri Katibu tawala mkoa ambae yupo kwenye uwashaji Mwenge Morogoro hivyo mtetezi hasa ni nani iwapo walimu hawapati stahiki zao? nimepata kizungumkuti sana leo hasa nchi ni moja mwaka wa kuajiriwa ni mmoja iweje kuwe na mambo kama haya? kimbilio letu hasa ni wapi? tumesimama kidete kuhakikisha hatuendelei kuchezewa kama wanavyotaka kwa kufahamu haki haiombwi bali hutafutwa na ikibidi hulazimishwa kupatikana. Kwakweli wanajamvi naomba tupeane ujanja ni namna gani tunaweza kwenda sawa na waajiri wasiotambua stahiki za watumishi wao japo kwa Kigoma Manispaa mmmmm sidhani mana pameoza sana hawana utu kabisa. Mwenye namba ya Waziri Tamisemi naomba pamoja na Naibu wake labda baada ya ngazi zote ni kunyooka tuu kwa hawa kazi tuu inaweza saidia kwa kiasi fulani. Tushikane mikono jamaani haya ni maisha yetu sote ahsanteeni na poleni kwa kusoma andiko lefu baada ya hapa mtasikia tuu kinachoendelea! KARIBUNI KWA MAWAZO
Cc:MOTOCHINI
Cc:mcubic
 
aiseee upo sahihi kabisa yani maisha yake ni magumu lakini pia hata stahiki za watumishi majamaaa yanakaza tuu sijui kunani ngoja nifanye mchakato niinuke tuu
Wewe huna haja ya kutoka huko subiri mbunge wetu ana mpango wa kuyaboersha maisha ya wana wa kigoma
Cc:mcubic
Cc:MOTOCHINI
 
Andaa vile wanavyoangalia wakija kukagua,toa notes za kutosha,kusanya madaftari ya wanafunzi weka tick za kutosha
Ingia mtaani kusaka pesa hadi mambo yakiwa sawa
Akauze mawese na kayoga hizo ndio biashara zisizo hitaji mtaji mkubwa na hazina complication
 
Wewe huna haja ya kutoka huko subiri mbunge wetu ana mpango wa kuyaboersha maisha ya wana wa kigoma
Cc:mcubic
Cc:MOTOCHINI
utasubiri sana kama unadhani maisha yanaboreshwa na mtu wa nje badala ya juhudi zako pole! ahsante kwa ushauri
 
utasubiri sana kama unadhani maisha yanaboreshwa na mtu wa nje badala ya juhudi zako pole! ahsante kwa ushauri
Hata hao matajiri wanao miliki magari na maduka hapo kigoma walianzia kwenye kuuza migebuka na kayoga
 
Back
Top Bottom