Wakuu salaam..
.
Hivi inawezekanaje mtu kuota ndoto ndefu ndani ya muda mfupi sana?hii inanitokea sana,kwa mfano leo mida ya saa 5 asubuhi wakati nasikiliza taarifa ya habari bbc,nikasinzia.Ile taarifa ya habari huwa inachukua kama dk 5 hivi,basi nikaanza kuota niko kijijini,tunatoka mimi na kaka tunaenda porini kukata miti ya kujengea choo.Tunakata ya kutosha tunaibeba kuisombelea nyumbani.Tunajenga choo kinaktwa tayari kwa matumizi na mzee anatupongeza.Ghafla nikashtuka usingizini nikakuta ile taarifa ya habari ndio inaishia!sasa swali ni je,yaani kweli mishemishe zote za kwenda porini kukata miti,kuibeba,kujenga choo hadi kinakamilika ndio zimetumika dk 5 tu??