Maandiko ya Mwalimu ni ya kipekee. Watawala na watawaliwa wengi kwa sasa hawayataki kwa sababu yanawaumbua. Mimi maandiko ya Mwalimu ndiyo dira yangu ya maendeleo. Ukiyasoma maneno ya Mwalimu lazima utakuwa mtu muungwana na mpenda binadamu wenzako na pia mazingira yanayokuzunguka.