Maneno haya yanasisimua


princetx

princetx

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Messages
581
Likes
76
Points
45
princetx

princetx

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2012
581 76 45
Kama tungejua yanayosemwa juu yetu tukiwa hatupo,hakika tusingetabasamu kwenye nyingi ya nyuso za watu!!
(ukweli ni huo)

Aliulizwa mwenye hekima kwa nini mbingu ni safi?
akatabasamu na akajibu:kwa sababu wanadamu hawaishi huko!!

Maji kidogo yanakuokoa,na maji mengi yanaweza kukugharikisha!!
jifunze daima kutosheka na unachomiliki.

Ili ufaulu katika maisha unahitaji mambo mawili:
🔸kujiamini
🔸kupuuza

Ujinga ni upungufu,kujifanya mjinga ni ukamilifu.Kughafilika ni upotevu,kujighafilisha ni hekima!

dhiki usizozijua????
huenda ni dhambi zinakutaka uombe maghfira..

Ibada
inamfanya mtu aweze kudhibiti zaidi matendo yake yenye hisia
amesema Mwenyezi Mungu:(Kwa hakika binadamu ameumbwa hali ya kuwa mwenye papatiko.Inapomgusa shari huwa mwenye fazaa.Na inapomgusa kheri huwa anaizuilia.

Hasidi daima anakuona unaringa,na anayekupenda anakuona mzuri!

Usiumie anapokanusha mmoja wa watu wema uliomfanyia! kwani taa za barabarani zinasahauliwa mchana!!

Ulianguka mti na wakasikia wote sauti ya muanguko wake!
wakati ambapo msitu mzima unamea wala husikii kelele zozote!
watu hawatazami mafanikio yako bali anguko lako

Baadhi ya mabadiliko ni magumu!
lakini ni ya lazima ili kuendelea na maisha!!

Jifunzeni kuwaongoza kwenye mwangaza walio karibu yenu,hata ikiwa yaliyojificha kwenu ni giza totoro

Siku zote kinacholeta nuksi siyo bahati mbaya!! hakika ni madhambi yaliyorundikana na ambayo mengi yao tumeyasahau!!
[HAKIKA MAASI YANAONDOA NEEMA]

Nimevutiwa na nayo...
nikaona niwazawadie,
Wanajf wenzangu

TUAMRISHANE
MEMA
 
Patrickn

Patrickn

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Messages
8,330
Likes
5,087
Points
280
Patrickn

Patrickn

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2010
8,330 5,087 280
umetisha mkuu.....hii ni chakula ya akili na roho
 

Forum statistics

Threads 1,252,214
Members 482,048
Posts 29,800,701