GE2025 Manara: Serikali ya CCM inajali elimu, awapatia wanafunzi elfu kumi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mgombea Udiwani wa Kata ya Kariakoo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Haji Sunday Manara, amesema kuwa Serikali ya CCM imeendelea kuthibitisha kujali elimu kwa vitendo, kwa kuwekeza kwenye misingi imara iliyopelekea kuzalisha wasomi wengi nchini.

Manara alitoa kauli hiyo leo aliposhiriki mkutano wa kampeni za kumnadi Mgombea Udiwani wa Kata ya Jangwani, Nassibu Hassan Kitabu, uliofanyika ndani ya kata hiyo, ambapo alipata nafasi ya kuuliza swali kwa mmoja wa wanafunzi waliokuwepo na kuonyesha umahiri wake kwa kujibu kikamilifu.

Akizungumza mbele ya wananchi waliohudhuria mkutano huo, Manara alisema kuwa kwa sasa watoto hawana tena hofu kuhusu kupata elimu bora, kwani Serikali ya Awamu ya Sita imefanya kazi kubwa kuhakikisha mazingira ya elimu yanaboreshwa na kuwa rafiki kwa mwanafunzi wa Kitanzania.
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…