Manahodha waliopita wamfunda Cannavaro

News TZ

Senior Member
Jun 17, 2015
127
69
nadir-haroub-cannavaro_210_120.png


WACHEZAJI mbalimbali wa soka waliopata kuwa manahodha wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ wamezungumzia hatua ya nahodha wa timu hiyo Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kujiuzulu kuchezea timu hiyo, huku baadhi wakimshauri afute uamuzi wake. Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime amemtaka Cannavaro kufuta uamuzi wake wa kujiuzulu Taifa Stars kwani mchango wake unahitajika. Maxime ambaye aliwahi pia kuwa nahodha wa Stars wakati ikiwa chini ya Mbrazil, Marcio Maximo, alisema alichofanya beki huyo si sahihi. Hivi karibuni kocha wa Stars, Charles Mkwasa alimpa unahodha mchezaji wa TP Mazembe ya Congo DR Mbwana Samatta na kusema Haroub atabaki kuwa nahodha kwenye timu inayoshiriki michuano ya ndani ya Afrika (Chan).

Akizungumza na gazeti hili jana, Maxime alisema suala la unahodha mwenye uamuzi ni kocha, hivyo Cannavaro hana budi kukubaliana na maamuzi hayo na kwa nafasi anayocheza kwa sasa timu ya taifa bado anahitajika. “Kwa nafasi ya mabeki wetu, Cannavaro bado anahitajika sana kwenye timu, arudi tu mchango wake bado unahitajika sana ingawa kujiuzulu ni utashi wake mwenyewe, lakini anahitajika bado ana uwezo na ana nidhamu nzuri,” alisema. Akifafanua zaidi suala la nafasi ya nahodha, Maxime alisema: “Suala la kocha kumnyang’anya unahodha Cannavaro inaweza kuwa si sahihi au sahihi, yote kwa yote. “Sahihi kwasababu kocha ndio anaamua nani awe nahodha, kwani wachezaji wake anawafahamu vizuri, lakini pia unahodha hauna barua unajua maana hayo ni maamuzi ya kocha, mimi nadhani Cannavaro aelewe tu na si kweli kwamba amedharaulika,” alisema.

Naye nahodha mwingine wa zamani wa Taifa Stars, Peter Manyika ameungana na Maxime kwamba mchezaji huyo wa Yanga anapaswa kufanya kazi yake kwani uamuzi wa kuteua nahodha ni wa kocha. “Kocha ndio anateua nahodha kwa sababu ndio bosi kwa hiyo kama ameamua basi atakuwa na sababu za msingi na hatuwezi kumuingilia sababu zake,” alisema. Kuhusu kujiuzulu kwa Cannavaro, Manyika alisema hilo ni jambo la utashi wa mtu ingawa upande wake anaamini bado alistahili kuwepo kwenye timu.

“Kujiuzulu kila mtu ana upeo wake, unahodha unajua ni kitu kizito labda sababu za kuvuliwa kwake hazijamridhisha hatuwezi kujua kinachotakiwa hapo ni suluhisho ambalo naamini litafanywa na kocha na mchezaji mwenyewe,” alisema Manyika. Tangu kufanyika kwa maamuzi hayo Cannavaro amekuwa akilalamika kwenye vyombo vya habari kwamba hakutendewa haki kwa namna alivyovuliwa unahodha. Lakini Mkwasa akizungumza na gazeti hili, alisema hajamvua unahodha Cannavaro bali alichokifanya ni mabadiliko ya kawaida kwenye timu. “Sikuwa na sababu ya kumuondoa kwenye unahodha, namheshimu sana Cannavaro (Haroub) na ametoa mchango mkubwa kwa taifa hili na bado namhitaji, kwa nini nimuondoe,” alisema.

“Nilichokifanya ni mabadiliko kidogo tu kwenye kazi ni kama nyinyi huko kuna Mhariri wa Habari na Mhariri wa Michezo, ndivyo nilivyofanya mimi na hili lipo duniani kote, hata ukiangalia wenzetu Ivory Coast, Cameroon Zambia, Uganda na hata Rwanda… “Sasa hivi kuna mashindano ya Chan yanaendelea lazima utakuta nahodha wa Afcon sio yule wa Chan,” alisema. Beki huyo ametangaza kujiondoa Taifa Stars kutokana sababu mbalimbali lakini mojawapo ikiwa ni kuvuliwa unahodha bila kupewa taarifa, ingawa kocha alisema alimjulisha.

Chanzo: darwaya.com
 
Nimependa apo kocha aliposema sijamvua unahodha Canavaro ila nilichofanya ni mabadiliko tu…!! Unaelewa nn apa mdau?
 
Nadhani cannavaro kaonyesha ubinafsi uliotukuka katika jili la unahodha...yeye ni nani hata afikilie kuwa nafasi hiyo haitakiwi kuchukuliwa na mwingine...upuuzi mtupu asema kitu kingine si cha unahodha
 
Nadir Haroub analilia barua ya kuondolewa kwenye Unahodha wakati hata barua ya kuteuliwa unahodha hana. Cheo chochote unachopewa bila ya Maandishi ukakubali usiombe barua ck ukitolewa
 
View attachment 318221
WACHEZAJI mbalimbali wa soka waliopata kuwa manahodha wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ wamezungumzia hatua ya nahodha wa timu hiyo Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kujiuzulu kuchezea timu hiyo, huku baadhi wakimshauri afute uamuzi wake. Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime amemtaka Cannavaro kufuta uamuzi wake wa kujiuzulu Taifa Stars kwani mchango wake unahitajika. Maxime ambaye aliwahi pia kuwa nahodha wa Stars wakati ikiwa chini ya Mbrazil, Marcio Maximo, alisema alichofanya beki huyo si sahihi. Hivi karibuni kocha wa Stars, Charles Mkwasa alimpa unahodha mchezaji wa TP Mazembe ya Congo DR Mbwana Samatta na kusema Haroub atabaki kuwa nahodha kwenye timu inayoshiriki michuano ya ndani ya Afrika (Chan). Akizungumza na gazeti hili jana, Maxime alisema suala la unahodha mwenye uamuzi ni kocha, hivyo Cannavaro hana budi kukubaliana na maamuzi hayo na kwa nafasi anayocheza kwa sasa timu ya taifa bado anahitajika. “Kwa nafasi ya mabeki wetu, Cannavaro bado anahitajika sana kwenye timu, arudi tu mchango wake bado unahitajika sana ingawa kujiuzulu ni utashi wake mwenyewe, lakini anahitajika bado ana uwezo na ana nidhamu nzuri,” alisema. Akifafanua zaidi suala la nafasi ya nahodha, Maxime alisema: “Suala la kocha kumnyang’anya unahodha Cannavaro inaweza kuwa si sahihi au sahihi, yote kwa yote. “Sahihi kwasababu kocha ndio anaamua nani awe nahodha, kwani wachezaji wake anawafahamu vizuri, lakini pia unahodha hauna barua unajua maana hayo ni maamuzi ya kocha, mimi nadhani Cannavaro aelewe tu na si kweli kwamba amedharaulika,” alisema. Naye nahodha mwingine wa zamani wa Taifa Stars, Peter Manyika ameungana na Maxime kwamba mchezaji huyo wa Yanga anapaswa kufanya kazi yake kwani uamuzi wa kuteua nahodha ni wa kocha. “Kocha ndio anateua nahodha kwa sababu ndio bosi kwa hiyo kama ameamua basi atakuwa na sababu za msingi na hatuwezi kumuingilia sababu zake,” alisema. Kuhusu kujiuzulu kwa Cannavaro, Manyika alisema hilo ni jambo la utashi wa mtu ingawa upande wake anaamini bado alistahili kuwepo kwenye timu. “Kujiuzulu kila mtu ana upeo wake, unahodha unajua ni kitu kizito labda sababu za kuvuliwa kwake hazijamridhisha hatuwezi kujua kinachotakiwa hapo ni suluhisho ambalo naamini litafanywa na kocha na mchezaji mwenyewe,” alisema Manyika. Tangu kufanyika kwa maamuzi hayo Cannavaro amekuwa akilalamika kwenye vyombo vya habari kwamba hakutendewa haki kwa namna alivyovuliwa unahodha. Lakini Mkwasa akizungumza na gazeti hili, alisema hajamvua unahodha Cannavaro bali alichokifanya ni mabadiliko ya kawaida kwenye timu. “Sikuwa na sababu ya kumuondoa kwenye unahodha, namheshimu sana Cannavaro (Haroub) na ametoa mchango mkubwa kwa taifa hili na bado namhitaji, kwa nini nimuondoe,” alisema. “Nilichokifanya ni mabadiliko kidogo tu kwenye kazi ni kama nyinyi huko kuna Mhariri wa Habari na Mhariri wa Michezo, ndivyo nilivyofanya mimi na hili lipo duniani kote, hata ukiangalia wenzetu Ivory Coast, Cameroon Zambia, Uganda na hata Rwanda… “Sasa hivi kuna mashindano ya Chan yanaendelea lazima utakuta nahodha wa Afcon sio yule wa Chan,” alisema. Beki huyo ametangaza kujiondoa Taifa Stars kutokana sababu mbalimbali lakini mojawapo ikiwa ni kuvuliwa unahodha bila kupewa taarifa, ingawa kocha alisema alimjulisha.

SOURCE: darwaya.com
Tatizo si unahodha bali ni jinsi Mkwasa alivochukua uamuzi wa mabadiliko. Mie naamini kabisa Mkwasa hatufikishi popote kisoka kwani upeo wake haufanani kabisa na hao akina Mbwana na Tomas. Namuumga mkono Haroub kwa utovu wa uungwana aliofanyiwa.
 
Uamuzi wa Canavarro ni sahihi kabisa. Tatizo ni namna alivyovuliwa unahodha. Lazima iwepo heshima kwa mchezaji kama huyo. Angepewa taarifa kabla ya kumtangaza Samatta.

Kwa vile waliona hawana haja ya kumpa taarifa, kwa nini aendelee na watu hao hao? Uamuzi wake unalinda heshima yake na kuonyesha jinsi kocha na viongozi wa TFF walivyo kosa staha
 
Uamuzi wa Canavarro ni sahihi kabisa. Tatizo ni namna alivyovuliwa unahodha. Lazima iwepo heshima kwa mchezaji kama huyo. Angepewa taarifa kabla ya kumtangaza Samatta.

Kwa vile waliona hawana haja ya kumpa taarifa, kwa nini aendelee na watu hao hao? Uamuzi wake unalinda heshima yake na kuonyesha jinsi kocha na viongozi wa TFF walivyo kosa staha
lakini kocha anasema alimpa taarifa kabla!!
 
Kanavaro, El Kapatain, Nahodha, Jitu Jeusi, Jitu la Misimamo! Ami yuko sahihi, alichofanya Mkwassa ni kama Malaya wa Baa, kukaa kwenye meza yenye bia nyingi... Alikuwa anatafuta huruma ya wakubwa na washabiki kwa kumpa unahodha kipenzi chao, haipendezi hata kidogo.
Huyo Samatta timu ya taifa ana skendo ya kucheza bila kujituma na kusingizia majeraha, hafai kuwa nahodha!
 
Nadhani cannavaro kaonyesha ubinafsi uliotukuka katika jili la unahodha...yeye ni nani hata afikilie kuwa nafasi hiyo haitakiwi kuchukuliwa na mwingine...upuuzi mtupu asema kitu kingine si cha unahodha
alichokuwa anacomplain yeye ni kutopewa taarifa hata kwa simu tu, yaani kakaa sebuleni anaangalia habari ndo anashtuka, baadaye ndo wakampigia
 
Tatizo si unahodha bali ni jinsi Mkwasa alivochukua uamuzi wa mabadiliko. Mie naamini kabisa Mkwasa hatufikishi popote kisoka kwani upeo wake haufanani kabisa na hao akina Mbwana na Tomas. Namuumga mkono Haroub kwa utovu wa uungwana aliofanyiwa.
Ni kweli ila afkilie yeye anatakiwa awe mzalendo kwa taifa lake..Kwa uamuzi huoo hamkomoi mkwasa anaikomoa nchi yake ya tanzania..uamuzi kam huo waufanyie kwnye simba na yanga..hvi mbna tunakosa uzalendo hvi
Uamuzi wa Canavarro ni sahihi kabisa. Tatizo ni namna alivyovuliwa unahodha. Lazima iwepo heshima kwa mchezaji kama huyo. Angepewa taarifa kabla ya kumtangaza Samatta.

Kwa vile waliona hawana haja ya kumpa taarifa, kwa nini aendelee na watu hao hao? Uamuzi wake unalinda heshima yake na kuonyesha jinsi kocha na viongozi wa TFF walivyo kosa staha
 
lakini kocha anasema alimpa taarifa kabla!!

Mkuu, nadhani Mkwassa anajikosha tu. Amegundua kosa lake hataki kujishusha na kusema ukweli.

Kwenye sakata hili kuna nafuu moja tu. Fikiria kocha angekuwa damu ya Simba. Zingekuja tafsiri nyingine mpya! Bahati nzuri mchezaji na kocha wote damu ya Yanga. Mkwassa na TFF wamelikoroga.
 
Kama ni hilo la kupewa barua tu basi Mkwasa na benchi lake la ufundi wanatakiwa wajirudi.

Lakini tuwe wakweli wachezaji wa timu zetu za taifa wanapoteuliwa na kocha mkuu pamoja na kutangaza manahodha wa timu huwa wanapewa barua kweli kabla ya kutangazwa au hata kupigiwa simu? Si ndiyo mila na desturi zetu kocha anaitisha mkutano na waandishi wa habari baada ya hapo anatiririka majina ya walioteuliwa. Muungwana kama kilio chake kimesikika ni kusamehe na kurudi kulitumikia Taifa.

Tena hilo la unahodha wa CHAN kutenganishwa na ya kimataifa ndiyo mahale pake haswaa. Maana timu zetu taifa zina michezo mingi ya ndani kuliko ya kimataifa.

Na hivi ambapo tumeshatolewa kwenye michuano ya kombe la dunia na ambapo mara nyingi hata AFCON huwa tunaishia huku michezo ya awali huyo Mbwana Samatta akifanikiwa kwenda Genk ~Ubelgiji au Nantes~Ufaransa atakuwa anaonekana kwa nadra sana kwenye timu yetu ya taifa, maana hata michezo ya kimataifa ya kirafiki vilabu vikubwa hutunga uongo uliotukuka ili wachezaji wa Kiafrika wasirudi kutumikia timu zao za taifa. Msisitizo huwa ni kwenye madhindano ya kimataifa yanayotambuliwa na FIFA ambayo mara nyingi ni kombe la dunia na AFCON ambako huwa hatushiriki!

Hilo la kujituma timu ya taifa siyo kwa kina Sammata limekuwa tatizo sugu kwa nyota wa Kiafrika wanaokipiga Ulaya, lakini tusemezane ukweli tuu nani anaweza kubambika mguu wake kwenye mechi ambazo ukiumia unaishiwa kukandikwa barafu tu bila matibabu ya maana na pole? Halafu ukose mamilioni ya pesa kwa wiki kwenye klabu yako na upokwe namba. Money talks kubambika mguu bila pesa loooh!
 
Nadir Haroub analilia barua ya kuondolewa kwenye Unahodha wakati hata barua ya kuteuliwa unahodha hana. Cheo chochote unachopewa bila ya Maandishi ukakubali usiombe barua ck ukitolewa
Lakini nina hakika Unahodha hakupewa kupitia kipindi cha michezo redioni!
 
TFF hawabadiliki kabisa kapteni wa timu ni mtu mkubwa hawatakiwi wamchukulie kama walivyofanya mchezaji amejituma na amekua mzalendo kwa miaka yake yoote kwa timu yetu mbona woote sawa tuu.. Mkwasa anakuwa kama hakuwaona wakina Gaga,marsha,george lukas,Athuman China,Kizota na wale wataalamu waliopita..
 
alichokuwa anacomplain yeye ni kutopewa taarifa hata kwa simu tu, yaani kakaa sebuleni anaangalia habari ndo anashtuka, baadaye ndo wakampigia
kwa style hiyo hata mimi ningechukia kwa kweli...ila basi ampuuze Mkwasa na alifikilie taifa katika maamzi yake!
 
Yeye, Yondani, Erasto Nyoni wapumzike tu na vijana wengine wapewe nafasi timu ya Taifa. Tumekuwa tunafungwa magoli ya kipuuzi sababu ya uzembe wa hawa mabeki.

Nchi hii ina wachezaji wengi vijana, mbona John Terry aliondolewa England na Chris Smalling aka emerge kuwa beki mzuri sasa hivi?! Na wanampa nafasi kinda mwingine anaitwa John Stones akiwa na miaka 20 tu! Tuwape nafasi vijana bhana, hakuna haja ya kuwalilia hawa wazee.
 
Back
Top Bottom