Mamlaka za maji zitupe mwongozo wa matumizi ya maji kuzalisha chakula

Mahandeiboho

Member
Dec 27, 2016
94
43
Ni wakati sasa wa kuwauliza wahusika wa maji katika maeneo yote watupe muelekeo wa kunusuru nchi kutokana na baadhi ya maeneo kuwa na njaa inayotishia uhai wa watanzania wengi hasa vijijini.

Skimu za umwagiliaji zote nchini zitupe mkakati wa kutumia maji ya mito yetu mikuu kwa ufanisi tupate chakula.

Maziwa Victoria, Tanganyika, Nyasa, Eyasi, Natron, Rukwa, Manyara na Jipe yatakuwa na mchango gani. Maji yanayovutwa kwa pump toka ardhini yatasaidiaje. Je walio na maji ya bomba majumbani wataendelea kukatazwa wasiyatumie kuotesha mchicha na nyanya na vitunguu katika compound zao. Ni vipi mifugo itapata maji isiendelee kufa?

Naomba tuchangie uzi huu kwa nia ya kujenga msingi wa matumizi ya rasilimali kiuchumi na sio kutuambia inaruhusiwa kutumia maji kuoga na kufua ila kumwagia karoti zangu za kula na watoto hairuhusiwi.
 
Ni wakati sasa wa kuwauliza wahusika wa maji katika maeneo yote watupe muelekeo wa kunusuru nchi kutokana na njaa inayotishia uhai wa watanzania wengi hasa vijijini. Skimu za umwagiliaji zote nchini zitupe mkakati wa kutumia maji ya mito yetu mikuu kwa ufanisi tupate chakula. Maziwa Victoria, Tanganyika, Nyasa, Eyasi, Natron, Rukwa, Manyara na Jipe yatakuwa na mchango gani. Maji yanayovutwa kwa pump toka ardhini yatasaidiaje. Je walio na maji ya bomba majumbani wataendelea kukatazwa wasiyatumie kuotesha mchicha na nyanya na vitunguu katika compound zao. Ni vipi mifugo itapata maji isiendelee kufa? Naomba tuchangie uzi huu kwa nia ya kujenga msingi wa matumizi ya rasilmali kiuchumi na sio kutuambia inaruhusiwa kutumia maji kuoga na kufua ila kumwagia karoti zangu za kula na watoto hairuhusiwi.
It is ok. Go ahead.
 
Je, Katika hali ya tishio la njaa tulilo nalo kuendelea kuweka masharti ya matumizi ya maji kunatusaidia? Wanaohusika wakifanya hivyo hata sehemu ambazo watu wangezalisha chakula cha kutosha familia hawataweza tena.
 
Back
Top Bottom