Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,157
Hii ni kero kubwa hapa Morogoro mjini. Kwa takribani mwezi mmoja sasa sisi wakazi wa Morogoro majumbani mwetu tunapata maji machafu na yenye harufu kali mithili ya maji ya kwenye chemba za chooni!!
Hali hii inasikitisha sana. Na kibaya zaidi swala hili limechukua muda mrefu sana kinyume na matumaini tuliyopewa na baadhi ya wafanyakazi wa idara hiyo tulipo hoji mwanzoni kabisa
Tunaomba idara na mamlaka husika mlimulike swala hili kwa uzito kwani sisi wakaazi wa Manispaa hususani mitaa ya Mafiga na Misufini tunateseka sana!
Haya maji hayafai kwa matumizi ya binadamu lakini kwa sababu ya shida na kukosa mbadala tunalazimika kuyatumia hivyo hivyo kwa kutegemea kudra za mwenyezi Mungu kitu ambacho ni cha hatari sana tena sana.
Nisisi wakaazi wa Morogoro kutoka mitaa ya Mafiga na Misufini, tunaomba vyombo vya habari mtusaidie kupaza sauti kwa hili ili wahusika watuondolee kero hii kwani sisi tumeongea hadi tumechoka