Halafu waliongeza bila kutoa taarifa sijui tatizo nini, huduma muhimu kama ya maji kupandisha bei ghafla hivi mpaka sasa sijajua lengo lao nini, au ni gharama za uzalishaji zimeongezeka? Au ndio wanapima upepo? Kwa kweli wametuumiza sana sisi wananchi hasa sisi wa hali ya chini. Ziwa victoria lipo hapahapa halifu tuuziwe maji kama tupo jangwani, wasije wakasababisha mlipuko wa magonjwa sababu maji na usafi ni vitu vinavyoendana.