Kama miezi minne iliyoita tulitangaziwa kuwa mvua kubwa itanyesha maeneo mengi ya nchi hasa Kanda ya Ziwa. Kwa kawaida mvua kwenye maeneo ya Kanda ya Ziwa huanza kunyesha mwishoni mwa mwezi Septemba lakini mpaka sasa hakuna mvua zinazonyesha licha ya manyunyu manyunyu ya hapa na pale. Inavyoelekea mwaka huu kutakuwa na njaa kali hasa katika Kanda hii. Ule uamuzi wa Serikali wa kutouza vyakula nje yanchi ibaki palepale. Katika Kanda hii kama mwaka ungekuwa mzuri mahindi yangeanza kubeba lakini hata kupanda mazao bado kutokana na kukosekana kwa mvua ya vuli.