Ngalikivembu
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,959
- 874
Hakika nchi hii ya JK ina mambo mengi kutoka ndani ya serikali yake.Mamlaka ya hali ya hewa ni wakala wa serikali kama zilivyo TRA,TCAA,TAA na nyingine nyingi tu.Kwa kawaida serikali au wakala wake huwa wana utaratibu wa kuwa na kitengo cha mafunzo kwa wafanyakazi wake.Lengo kuu ni kuwaendeleza wafanyakazi kielimu.Sasa TMA nayo ina utaratibu huo huo japo hapa kuna usiri mkubwa sana juu ya kusomesha wafanyakazi wake.
Hivi sasa mamlaka imekuwa ikisomesha wafanyakazi hewa.Hawa wanalipiwa na mamlaka.Wengi wao wanaaminika kuwa wanasoma OPEN UNIVERSITY.Wafanyakazi hao wamekuwa wakitumiwa pesa ya ada na stationery.Lakini list wanayoleta haipo kabisa.Utakuta wafanyakazi walioko vituoni wanatumiwa pesa hizo kwa maelezo kuwa wanasoma OUT,lakini undani wake ni kuwa hawajawahi kujisajili huko kama wanafunzi na hata wale waliojisajili awali kwa sasa wengi wao walikwisha acha kusoma,lakini pesa yao bado inamiminika kuja.Swali ni hili inakuwaje umsomeshe mfanyakazi halafu asikuletee maendeleo yake ya kila semester?Unaridhika na nini?Pengine alisha pata DISCO?Na wengi wao kutokana na ugumu wa masomo hayo ya sayansi wali drop mapema kabisa.
Je huu ni mradi wa wakubwa?Tazama hapa wafanyakazi wenye nia ya kusoma na ambao wanaomba msaada wa kusomeshwa wanakataliwa.Kubwa linalotafuna mamlaka hii ni kuendeshwa kikabila zaidi na kwa upande mwingine kuna element za udini.Ona mfano huu kuthibitisha,wafanyakazi wawili waliomba kusoma kozi moja inayokubalika sana TMA.Mmoja akaambiwa kozi hii haina kipaumbele kwetu.Mwingine akajibiwa tutakusomesha.Huyu wa pili ukitazama sana ni kwa sababu HR manager ni mtu wake toka eneo hilo hilo na dini ile ile.(Msini hukumu kwa hili lakini ugonjwa upo toka zamani).Ushahidi wa kusomesha wafanyakazi hewa upo.