Mamlaka ya bandari na TRA kubaini chanzo cha kupungua kwa shehena ya kontena

nanawoo

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
1,300
1,252

SERIKALI imeziagiza Mamlaka ya Bandari-TPA, na Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kufanya uchambuzi wa kina ili kubaini sababu za kupungua kwa shehena ya kontena zinazoingia nchini kupitia Bandari ya Dar es salaam kwenda nchi jirani.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dokta Philip Mpango, ameliambia Bunge mjini Dodoma, jana tarehe 30, Machi, 2016 kwamba taarifa zilizopo zinaonesha kwamba uingiaji wa mizigo inayopelekwa nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, Malawi na Zambia kupitia bandari hiyo, umeshuka.

Alisema katika kipindi cha mwezi Oktoba mwaka jana na Machi mwaka huu kontena zilizopelekwa nchini Congo zilishuka kutoka 5,529 hadi 4,092, wakati yale yaliyokuwa yakipelekwa nchini Malawi yalishuka kutoka kontena 337 hadi 265, huku yale ya Zambia yakishuka kutoka 6,859 hadi kufikia 4,448.

Hata hivyo, Dokta Mpango aliwahakikishia waheshimiwa wabunge kwamba kushuka kwa kiwango cha kontena ziendazo nchi jirani kupitia Bandari ya Dar es salaam, hakujaathiri malengo ya ukusanyaji wa mapato ya serikali.Alisema sababu mojawapo ya kushuka kwa idadi ya kontena zinazopitia bandari ya Dar es slaam zinachangiwa na kuporomoka kwa uchumi wa China ambao umeathiri nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania.

"lakini naziagiza Mamlaka ya Bandari Tanzania-TPA na Mamlaka ya Mapato-TRA, zichambue mwenendo huo ikilinganishwa na nchi nyingine" alisisitiza Dokta Mpango.Alilieleza Bunge pia kwamba, Tanzania haitozi kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa kontena zinazosafirishwa kutoka bandari hiyo kwenda nchi jirani hivyo hiyo haiwezi kuwa sababu ya kuzikwaza nchi jirani kutumia bandari ya Dar es salaam
 
Afadhali wamechukua hatua maana chanzo kinaeleweka wanajifanya hawajui wakaishia kulaumu wafanyabiashara. Siku zote mfanyabiashara anaangalia faida so kama kuna mwanya wa kukwepa kodi lazimaatautumia. Sasa tuangalie jinsi gani tutawatumia wafanyabiashara na tuache kuwatumana kama vile wao ndio walioifikisha hapa nchi hii na kuondoa lawama kwa wanasiasa.

Ni hatua njema I hope wadau wa bandari watatumia hii fursa vizuri kuishauri serikali ipunguze pupa sasa walidhani sifa kujitangaza kwamba bandari yetu ina wizi watu wamekimbia
 
Wakwepa kodi hawaleti mizigo. Bora hao wachache wanaolipa kodi.
 
SERIKALI YAIAGIZA MAMLAKA YA BANDARI NA TRA KUBAINI CHANZO CHA KUPUNGUA KWA SHEHENA YA KONTENA ZINAZOINGIA NCHINI SERIKALI YAIAGIZA MAMLAKA YA BANDARI NA TRA KUBAINI CHANZO CHA KUPUNGUA KWA SHEHENA YA KONTENA ZINAZOINGIA NCHINI ~ MUUNGWANA BLOG

Mi nadhani kuna shida kubwa sana kwenye uongozi wa nchi hii, sidhani kama kuna Sera rasmi ya nchi, naona kunakuwa na maamuzi binafsi, yaani mtu mmoja anaamua mustakabali wa nchi
Ndani ya miezi sita ya uongozi mpya tayari kuna kauli mbilimbili kwenye issue ya Sukari, kuna walakini kwenye upungufu wa Meli na mizigo Bandarini, bado hali sio nzuri mahospitalini pamoja na juhudi za kununua vitanda na kadharika

Kweli kazi ipo
 
Juzi nilipita mombasa nairobi kiukweli nilikukutana na gari nyingi za kontena zinatoka mombasa sijui zinaelekea wapi ni tofauti na miaka ya nyuma njia ile kukutana na semi zilikua chache sana laki siku hizi ni za kumwaga nahis itakua wamehamia nchi jiran
 
Back
Top Bottom