Mamlaka husika, ichunguzeni dispensary ya serikali ya Katoro hasa watumishi wake na utoaji wa huduma

GIPAMA

JF-Expert Member
May 21, 2016
1,103
541
Jamani, mamlaka husika mkoani geita, tafadhali sisi kama wananchi wa katoro, tunaomba watumishi wa dispensary hii wachunguzwe, wagonjwa wanazidiwa, bila huduma yeyote kupewa, waganga na manesi wanapiga story tu....

Fikiria mtu anafika asubuhi mpaka saa hizi hajaonana na mganga, wakati huo wapo wamejifungia wanapiga story tu.....

Enyi wauguzi na waganga wa dispensary ya katoro badilikeni, mnamuangusha rais wetu, kumbukeni kuna maelfu ya watu wanahtaji hizo nafasi za kazi.... Mnapozipata msijione miungu watu, mnahudumia wagonjwa kwa muda mnaotaka bila kujali hali za wagonjwa.

Mamlaka husika lichunguzeni hili jambo.
 
Back
Top Bottom