Mamelod Sundown ni daraja la kuipa Yanga sc hadhi ya ukubwa Afrika

mwehu ndama

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
543
1,837
Huwezi kuwa bora, bila kushindanishwa kisha kushinda dhidi ya walio bora kuliko wewe, naam, kuelekea mchezo wa Yanga afrika dhidi ya masandawana, tathmini yangu fupi ya kina kabisa imeleta mrejesho kuwa mechi hii ndio tanuru la moto litakalo kwenda kuisafisha Yanga sc, na kisha kusimikwa rasmi kama moja ya timu dume na wababe wa kubumbumbu la ngazi ya vilabu barani Afrika kwa kipindi hiki.

Bila kuwakosea heshima wanayostahili mamelod sundown, nasema wazi kuwa wamekutana na mpinzani waliemtaka katika nyakati mbaya.Inafahimika kuwa mashabiki wa mamelod huko south afrika na wale wa kukodi toka kolozidad wanafikiri yanga sc ni timu itakayowapa ahueni ya kuingia nusu fainali. Ila wasichokijua ni kwamba yanga sc iko njiani kuelekea kilele cha ubora wake, Yanga sc inawachezaji wenye njaa kali na quality ya kimataifa yakucheza na timu yoyote ile barani Afrika nakupata matokeo iwe home au away.

Ubora wa timu katika soka unaendana na nyakati sababu ni mchezo jumuishi, unategemea kikundi cha watu chenye muunganiko sahihi kiuchezaji ili kuwa tishio na sio pesa pekee itakufanya uwe na timu bora uwanjani, na ndio maana hadi Leo timu kama psg pamoja nakuwa na mastaa wote wakubwa bado walikuwa wanakandwa uefa, man utd na Chelsea pamoja navikosi vya gharama bado Liverpool na arsenal zinawahenyesha sababu hawana muunganiko sahihi wa wachezaji. Tp mazembe alikadharika.

binafsi sijawahi kuona muunganiko bora wa timu yoyote ile ya Tanzania kiuchezaji kama ilivyo Yanga sc ya sasa chini ya mchawi Gamondi, na itakuwa ni dhambi kubwa kwa wanandinga hao kutoka mitaa ya twiga na jangwani kushindwa kuwafurumusha mabwanyenye masandawana nje ya mashindano hayaaa.

Naiona aibu ya mamelod baada ya mechi zote mbili dhidi ya Yanga, ila natazama mbali nakuziona hoja za aibu na kufedheheka za mchambuzi wa kimakonde jemedari saidi huku akili na kwa maumivu ya ushindi wa Yanga, Wakati huhuo pembeni yake nyuso za aibu za mashabiki toka mbumbumbu efusii zikipaza sauti ya maumivu kushiriki katika mateso hayo.
 
Kwa uwezo wa Mungu naamini Yanga atashinda na kusonga mbele na mwisho ataishangaza dunia from zero to hero.

Kila la kheri niitakie Yanga!
 
Mpira ni serious Uwekezaji.

Sio mdomo.
Kelele na siasa.


HAWA AKINA MO NI WAONGO WAJANJA NA MATAPELI WA WA SIMBA NA YANGA.

MIMI BINAFSI NAAMINI UKISHABIKIA SANA SIMBA NA YANGA KICHWANI ZINAANZA KUPUNGUA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom