Interesting
Kwanza kama Kichwa cha familia, ukiona baba mwenye nyumba analalamika namna hii, ni dhahiri kabisa kwamba familia imeanza kumshinda kuiendesha.
Nategemea na wife atakuwa anafahamu kwamba husband ndio kiongozi wa familia na hivyo maamuzi na mashauri yake ni lazima yasikilizwe, hasa na yeye wife. Kama Mwanamke hana ufahamu huu wa msingi kabisa basi misingi ya familia inakuwa legevu na hapo ndio chanzo cha matatizo.
Na kama hali iko namna hiyo, basi tatizo zio kazi ya wife hata kidogo, tatizo ni uelewa wa misingi ya familia hasa katika swala la maamuzi ya mwisho.
Mwanamke ni lazima atambue kwamba maamuzi anayofanya mwanamme ni kwa faida ya familia, na mwanamme ni lazima afanye maamuzi katika misingi hiyo, kwa faida ya familia nzima akiwamo wife pia, na sio maamuzi yaliyojikita katika fikra za wivu.
Umezungumzia juu ya mtoto ambaye tayari ameshindwa kupata chakula kutoka mama, hii ni ishara kwamba mama au wote wawili hamuelewi majukumu yenu kwa mtoto,
cha msingi ni kwamba, maamuzi sahihi katika situations za namna hii huwa sio ya kibabe, by the way unaweza kukuta mama ndio mhemeaji mkuu wa chakula nyumbani, hapo panakuwa patamu kweli kweli.