Nahitaji ushauri wenu wana JF, mimi nina rafiki ambaye tulifahamiana toka niko sekondari kama family friend. Tulipoteana kwa muda wa miaka 8 hivi kisha tukaaza kuwasiliana tena mwaka huu (family friendship) tukaaza kuwa na mawasilanao ya kimapenzi ingawa tuko mabara tofauti tukitafuta elimu. Tunapendana sana na ameamua kuniomba afanye taratibu za kuoana ili tukirudi tu Tanzania tuoane.
Niliamua kuuliza nyumbani (Aunt yangu) kama tunaweza kuoana na huyo kijana nikajibiwa kuwa huyo kijana ndo awaulize wakubwa wa kwao. Tatizo ni kwamba inasemekana kwa mila zetu, haturuhusiwi kuoana watu tunaotokea eneo moja nami hizo mila sizijui, naye anasisitiza kuwa inawezekana, sasa ooooooh hata sijui nifanyeje hapa make sijampata mwingine ila yeye.
Msaada tafadhali
nahitaji ushauri wenu wana jf, mimi nina rafiki ambaye tulifahamiana toka niko sekondari kama family friend. Tulipoteana kwa muda wa miaka 8 hivi kisha tukaaza kuwasiliana tena mwaka huu (family friendship) tukaaza kuwa na mawasilanao ya kimapenzi ingawa tuko mabara tofauti tukitafuta elimu. Tunapendana sana na ameamua kuniomba afanye taratibu za kuoana ili tukirudi tu tanzania tuoane.
Niliamua kuuliza nyumbani (aunt yangu) kama tunaweza kuoana na huyo kijana nikajibiwa kuwa huyo kijana ndo awaulize wakubwa wa kwao. Tatizo ni kwamba inasemekana kwa mila zetu, haturuhusiwi kuoana watu tunaotokea eneo moja nami hizo mila sizijui, naye anasisitiza kuwa inawezekana, sasa ooooooh hata sijui nifanyeje hapa make sijampata mwingine ila yeye.
Msaada tafadhali
Kwa kuwa mila yenyewe huijui sana (maelezo yake na sababu zake), jaribu jkuulizia kule nyumbani wakueleze sababu ya katazo hilo: yawezekana ni sababu nzuri na nzito kabisa, huwezi kujua. Wakishakueleza - ukiona ni sababu isiyo na uzito - unaweza pia kuwaelimisha wazazi na wana-ukoo juu ya kilicho cha kweli: kwamba kutoka sehemu moja si kizuizi cha ndoa kama si undugu wa damu. Wakikuelewa utakuwa umepata pasi ya kuingia ndoa bila bughudha au kuwatia simanzi wazazi wako. Huenda katazo hilo linasababishwa na kutaka kuzuia tabia fulani mbovu au ugonjwa fulani wa kurithi ambao eneo lenu upo. Kwa hiyo kwa kutaka kutomeza polepole tatizo hilo wazee wakaweka katazo hilo ili kuwafnya watu wa eneno lenu waende mbali kuoa na kuchanganya damu na watu wengine wasio na athari hizo mbaya za eneo lenu. Huu ni mfano tu.
Kama inawezekana au haiwezekani kwa mujibu wa mila zenu, mimi ushauri wangu kwako ni zitupilie mbali hizo mila zisizo na kichwa wala miguu. Kama ninyi si ndugu wa damu na mmefikiana sioni ubaya wowote wa ninyi kutokufanya kile ambacho mioyo yenu inataka.
Haya mamila ya Kiafrika bana aaaah....wewe watu wanaoana na mabinamu zao huko Mashariki ya kati sembuse ninyi mliotoka eneo moja?
Fuata mila zilizo na maana. Za kipuuzi zipuuze.
MAra waseme kwanza kijana mwenyewe anamaringo, mara mweusi.... wakati mimi hayo hata siyaoni kwa huyu kijana.
Ndo maana watu wana-bleach ngozi cku hzi. Yaani huwezi amini watu ujinga umewajaa vichwani unaweza kubaki mdomo wazi halafu sasa unakuta ni mtu ana madigirii kama 100 hvi.Sasa hii ya kuwa "mweusi" wanapitiliza. Imekaa kiubaguzi baguzi wa rangi.
Ndo maana watu wana-bleach ngozi cku hzi. Yaani huwezi amini watu ujinga umewajaa vichwani unaweza kubaki mdomo wazi halafu sasa unakuta ni mtu ana madigirii kama 100 hvi.
Asante NN
Nitajitaidi ili niweze kukabiliana na hiyo hali kwa maana wamekuwa wakijaribu kunikatisha tamaa sana juu ya huyu kijana.
MAra waseme kwanza kijana mwenyewe anamaringo, mara mweusi.... wakati mimi hayo hata siyaoni kwa huyu kijana.
Wanataka tu kuumiza roho yangu make toka nimeambiwa hayo maisha yangu yamekuwa ni magumu sana.