Mambo unayohitaji kujua katika ndoto unazoota sehemu ya nne(jambo la 4) by Christopher Mwakasege

Principal Focus

JF-Expert Member
Jan 4, 2013
924
1,000
Bwana Yesu asifiwe milele!
Jambo la 4 kati ya “Mambo unayohitaji kuyajua kuhusu ndoto unazoota ili iwe vyepesi kufanikiwa kimaisha” ni hili:
“Ikiwa umeota ndoto ambayo tafsiri yake huijui ufanyeje?”
1. OMBA MUNGU AKUPE UFAHAMU JUU YA NDOTO! UFAHAMU HUU JUU YA NDOTO, UKIUPATA TOKA KWA MUNGU KATIKA KRISTO YESU, UTAKUSAIDIA WEWE NA WATU WENGINE PIA!
Biblia inatueleza ya kuwa: “Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto” (Daniel 1:17).
Kufuatana na Wakolosai 1:9, Mtume Paulo akiongozwa na Roho Mtakatifu aliwaombea wakristo waliokuwepo Kolosai wakati ule, wajazwe “maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni”.
Naamini hata katika nyakati za sasa, Roho Mtakatifu yupo tayari kutuongoza tujazwe “ufahamu wa rohoni”. Naamini ufahamu huu wa rohoni unahusu pia ufahamu juu ya ndoto!
2. USITAFUTE TAFSIRI YA NDOTO TOKA KWA MTU YE YOTE TU UNAYEDHANI ANAWEZA KUKUSAIDIA!
Kitabu cha Mwanzo 40:8 tunasoma swali hili: “Kufasiri si kazi ya Mungu” Hayo yalikuwa maneno ya Yusufu akiwahakikishia “Mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri”, juu ya upatikanaji wa tafsiri juu ya ndoto walizokuwa wameota!
Farao alipoota ndoto zake mbili mfululizo zilizofanana, tena kwa usiku mmoja (Mwanzo 41:1 – 7), alitafuta tafsiri ya ndoto zile mahali ambapo hakutakiwa kutafuta!
Farao alitafuta wapi kwanza juu ya tafsiri zake za ndoto alizoota usiku ule? Biblia inasema: “Farao akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko…akawahadithia ndoto zake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria…” (Mwanzo 41:8).
Ni mpaka alipotafutwa Yusufu aliyekuwa gerezani wakati ule, ili amtafsirie Farao ndoto zake. Yusufu akamwambia Farao: “Si mimi, Mungu atampa Farao majibu ya amani” (Mwanzo 41:16).
Ni wazi ufahamu aliokuwa nao Yusufu juu ya ndoto, ulikuwa mkubwa kuliko wa waganga na wachawi wote waliokuwa nchini Misri wakati ule!
Mfalme Nebukadreza aliona jambo kama hili kwa Danieli, alipomlinganisha na waganga na wachawi waliokuwa kwenye himaya yake alipokuwa anatawala.
Biblia inatueleza ya kuwa: “Danieli…alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto” na alifaa “mara kumi zaidi ya waganga na wachawi waliokuwa katika ufalme wake” (Danieli 1:17,20).
Ni kweli kuna mtu ambaye anaweza kukupa tafsiri ya ndoto yako, lakini asiweze kukupa ujumbe uliomo katika ndoto hiyo! Kupewa tafsiri ya ndoto, bila kupewa ujumbe unaoambatana na ndoto hiyo; ni sawa na kula chakula na ukashiba huku hakina virutubisho kwa afya yako.
3. OMBA MUNGU AKUPE KUJUA UJUMBE ULIOMO KWENYE NDOTO ULIYOOTA, ILI USIISHIE KUPATA TAFSIRI YA NDOTO BILA KUJUA UJUMBE WAKE!
Ukisoma kitabu cha Danieli 4:4 – 18, utaona ya kuwa kiu aliyokuwa nayo mfalme Nebukadreza, ilikuwa ni kujua tafsiri ya ndoto aliyoota, na si ujumbe uliokuwa ndani ya ndoto kwa ajili yake!
Lakini Danieli alimpa mfalme Nebukadreza vyote viwili – tafsiri ya ndoto (Danieli 4:20 – 26), na ujumbe uliokuwemo kwenye ndoto ile kwa ajili yake (Danieli 4:27).
Na kwa sababu mfalme Nebukadreza alitaka tafsiri ya ndoto, na si ujumbe wa ndoto, alijikuta akipuuzia na kutokutilia maanani ujumbe wa ndoto aliopewa, wala hakuufuatilia! Na matokeo yake ni maisha ya mateso ya miaka saba, kwa ajili yake, na kwa ajili ya familia yake, na kwa ajili ya serikali ya ufalme wake.
Unapoendelea kutafakari juu ya jambo hili, ni vizuri nikujulishe pia yafuatayo:
(i) Kuna ndoto ambazo zimebeba vitu vinavyohitaji tafsiri ili uweze kupata ujumbe uliomo ndani yake. Mfano wa ndoto kama hizi tunaupata katika Mwanzo 40:5 – 23
(ii) Kuna ndoto ambazo zimebeba vitu ambavyo maana yake iko wazi, na kwa ajili hiyo havihitaji tafsiri yake, ili kuupata ujumbe uliomo ndani yake. Soma mfano wake katika Mathayo 1:18 – 24.
(iii) Kuna ndoto ambazo zina ujumbe peke yake, bila kubeba vitu vyovyote zaidi ndani yake. Soma mfano wake katika Mathayo 2:12,22 na Mwanzo 31:24,29.
(iv) Mfasiri sahihi wa ndoto na ujumbe uliomo ndani yake ni Mungu tunayemwabudu katika Kristo Yesu; bila kujali chanzo cha ndoto uliyoota!
4. UWE NA NENO LA BIBLIA LA KUTOSHA NDANI YAKO – TENA KATIKA HEKIMA YOTE!
Wakolosai 3:16 inasema hivi: “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana…”
Kwa nini jambo hili ni la muhimu katika kutafsiri ndoto na kupata ujumbe uliomo ndani yake? Hii ni kwa sababu kufuatana na Ayubu 33:14,15 – ndoto ni neno katika picha!
Na kwa kuwa “kusikia huja kwa neno la Kristo” (Warumi 10:17), basi ujue bila neno la Kristo ndani yako huwezi “kusikia” ujumbe uliomo ndani ya ndoto – hata kama unajua tafsiri ya ndoto hiyo!
Hebu tuangalie mfano juu ya Biblia inasema nini kuhusu tafsiri ya ndoto zinazohusu madarasa, au kusoma, au kufanya mitihani; na ujumbe uliomo ndani yake.
Ukisoma kitabu cha Danieli 1: 3 – 20 unaweza kujifunza yafuatayo juu ya ndoto hizo:
(i) Maandalizi yanahitajika kwa ajili ya hatua iliyo mbele yako, au hatua unayotaka Mungu akupe unapoomba katika maombi yako.
(ii) Kuota “shule” au “chuo” maana yake maandalizi ya hatua fulani iliyo mbele yako yanahitaji utaratibu maalumu.
(iii) Kuota “shule” au “chuo” ulichowahi kusoma zamani, ina maana kwamba kuna jambo lililotokea hapo ulilotakiwa “kuvuka” – lakini hukuweza kuvuka, na kwa hiyo kuna eneo limekwama kwenye maisha yako.
(iv) Watu mlio nao darasani katika ndoto ina maana watu mlio ngazi moja ya kimaandalizi
(v) Kuota ndoto uko darasani na watu uliowahi kusoma nao zamani au unaota unarudia darasa, au unarudia mtihani – ina maana umekwama mahali kimaisha na unahitaji maandalizi ili kuvuka hapo.
(vi) Ukiota hukai darasani wakati wengine wako darasani; au hukai kwenye mtihani wakati wengine wanafanya mitihani – ina maana huna utulivu unaotakiwa uwe nao ili uweze kujiandaa vyema kwa hatua iliyo mbele yako
(vii) Ukiota unafanya mtihani – ujue: au unapita mahali kimaisha ambapo unapimwa kiwango chako ulichofikia kimaandalizi; au mbele yako kuna kuja kipimo kwa ajili ya kujua ikiwa umefikia kiwango kinachotakiwa kwa wewe kuingizwa hatua nyingine ya maisha
(viii) Ukiota unaota unasoma, na ukaona na somo unalosoma, au ukaota unafanya mtihani na ukaona somo la mtihani huo – ina maana unaonyeshwa aina ya, au eneo la – maandalizi unalotakiwa kulifuatilia kimaandalizi
Kumbuka – huu ni mfano tu wa kutafsiri ndoto na kupata ujumbe uliomo ndani yake kwa kutumia neno la biblia.
Mungu aendelee kukubariki unapoendelea kujifunza somo hili la ndoto.
 
Principal Focus

JF-Expert Member
Jan 4, 2013
924
1,000
Bwana Yesu asifiwe milele!
Ndani ya somo lililotangulia kabla ya hili, nilikuwa najibu swali hili: “Ikiwa umeota ndoto ambayo tafsiri yake huijui ufanyeje?”
Nilipokuwa nakupa majibu ya swali hilo, nilikufundisha vipengele vinne muhimu, katika kutafsiri ndoto. Leo – nataka nikufundishe kipengele cha tano, kitakachoweza kukusaidia katika kutafsiri ndoto unazoota, kipengele hicho ni hiki: “ANGALIA ULICHOKUWA UNAWAZA KUKIFANYA KABLA YA KUOTA NDOTO ULIYOOTA”
Waefeso 3:20 inatukumbusha ya kuwa, Mungu anaweza “kufanya mambo ya ajabu mno, kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo…”Kwa hiyo – ikiwa Mungu anatumia “ndoto” kama njia mojawapo ya kuwasiliana na watu (Ayubu 33:14,15) ina maana Mungu anaweza kutumia “ndoto” kujibu mawazo ya mtu, au kufikiri kwa mtu, au maombi ya mtu!
Ndiyo maana kwenye kipengele hiki cha tano, juu ya kutafsiri ndoto, nasisitizia umuhimu wa kuangalia ulichokuwa unawaza kukifanya kabla ya kuota ndoto uliyoota!
Hebu tujifunze jambo hili kwa mifano ifuatayo:
MFANO WA 1: YUSUFU ALIPOTAKA KUMKIMBIA MARIAMU.
Ukisoma habari iliyoandikwa katika Mathayo 1:18 – 20, utaona ya kwamba, kulikuwa na uhusiano wa kile ambacho Yusufu alikuwa anafikiria kukifanya, na ndoto aliyoota!Wakati huo Yusufu ambaye alikuwa anajiandaa kumwoa Mariamu – “akaazimu kumwacha kwa siri”, baada ya kusikia kwamba alikuwa mja mzito.
Biblia inasema; “Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema…usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu”.Ni dhahiri ndoto ile aliyoota Yusufu ilikuja ili kujibu alichokuwa anafikiri kukifanya – kumwonyesha ya kuwa hakikuwa sahihi!
Yusufu aliamua au aliazimu kumwacha Mariamu, kwa kuwa hakuwa na ufahamu wa kutosha juu ya mimba ya Mariamu. Ndoto ile ilimpa ufahamu, uliomsaidia kubadili kile alichokuwa anafikiria kukifanya.
MFANO WA 2: MAMAJUSI
Mamajusi waliombwa na Mfalme Herode, wampe taarifa ikiwa watajua Yesu alipozaliwa, ili naye aende kumsujudia
Ukisoma Mathayo 2:1 – 18 utajua ya kuwa si kweli kwamba Herode alitaka kujua Yesu alipozaliwa ili amsujudie – bali apate kumwua! Lakini Mamajusi hawakujua hila hizo za Herode! Kwa hiyo – walipomaliza kumsujudia Yesu na kumpa zawadi walizompelekea, wakawa wanajiandaa kurudi kwa Herode kumpa taarifa ya mahali Yesu alipokuwepo.
Ndipo biblia inasema; “Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine’ (Mathayo 2:12). Mungu aliingilia kati kwa njia ya ndoto, kuwazuia Mamajusi wasifanye kile walichokuwa wanafikiria kukufanya!
Tunaona tena katika mfano huu wa pili, umuhimu wa kufuatilia ulichokuwa unawaza – kama njia mojawapo ya kukusaidia kujua tafsiri ya ndoto uliyoota!
MFANO WA 3: KUHAMIA KANISA LINGINE
Kuna mtu aliyenishirikisha ndoto hii ifuatayo, baada ya kuamua moyoni mwake, kutaka kuhama toka Kanisa alilokuwa anasali, na kuhamia kanisa lingine – ambalo yeye aliona ni bora kuliko lile alilokuwa anasali wakati huo. Aliota ndoto ambayo ndani yake alimwona mchungaji wa Kanisa alilotaka kuhamia. Mchungaji huyo alikuwa anawaongoza waumini wake kuelekea porini – huku na yeye aliyeota ndoto hiyo akiwemo kwenye kundi hilo.
Na huko porini wakapotea njia na hawakujua pa kutokea – mchungaji wao na waumini wake. Na akaamka toka usingizini wakiwa wamepotea porini!
Mtu huyo alipoamka toka usingizini, na kuitafakari ndoto aliyoota – alijua Mungu alikuwa amemtumia ujumbe kwa njia ya ndoto aliyoota, ya kuwa uamuzi wa kuhamia kanisa alilotaka kuhamia, haukuwa sahihi! Na ikiwa ataamua kupuuza onyo lile, basi, angejikuta amepotea kiroho na kimaisha!
Yule mtu aliyeota ndoto ile, akanieleza ya kuwa aliamua kusitisha uamuzi wake wa kuhama kanisa kama alivyokuwa anataka kufanya!
Kumbuka: Njia mojawapo itakayokusaidia kutafsiri ndoto uliyoota, ni wewe kutathmini mawazo uliyokuwa unawaza kabla ya kuota ndoto uliyoota. Hii ni muhimu kwa sababu, ndoto hiyo inawezekana imeletwa kwako ili kujibu, au kurekebisha, au kuonya, au kuthibitisha - misimamo ya mawazo uliyokuwa unawaza, kabla ya kuota ndoto hiyo uliyoota!
Mungu aendelee kukubariki unapoendelea kujifunza somo hili pamoja nasi!
 
Principal Focus

JF-Expert Member
Jan 4, 2013
924
1,000
Jina la Yesu litukuzwe milele!
Jambo la 5 kati ya “Mambo unayohitaji kuyajua kuhusu ndoto unazoota ili iwe vyepesi kufanikiwa kimaisha” ni hili hapa:
“Omba Mungu akupe kujua muda uliomo katika ndoto, unaokupa kuomba na kujiandaa, au kubadili kuhusu uliyoota”.
Si ndoto zote zina kipengele cha “muda” wa namna hii, ingawa nyingi zinao, lakini wengi wanashindwa kuufuatilia!
Hebu tujifunze jambo hili kwa mifano ifuatayo:
Mfano wa 1: NDOTO ZA FARAO
Habari za ndoto hizi tunazipata tunaposoma Mwanzo 41:1 – 36. Ndoto zote mbili alizoota Farao katika usiku mmoja, zilikuwa na msisitizo mkubwa uliowekwa kwenye “muda”!
• Ndoto zote zilikuwa na matukio ya jumla ya “muda” wa miaka 14.
• Miaka 7 ya shibe ilihitajika kwa ajili ya kujiandaa, kwa ajili ya miaka 7 ya njaa.
• Sehemu ya 5 ya mavuno ya mwaka mmoja (1) wa shibe, ilihitajika kwa ajili ya mahitaji ya chakula ya mwaka mmoja (1) mzima wa njaa
• Maarifa yalihitajika kwa ajili ya kukusanya mavuno ya kila mwaka katika miaka 7 ya shibe; ili kupata na kutenga, na kulinda sehemu ya 5 kama akiba katika miji.
• Yusufu aliamua kutokuwa “mvivu” wa kuweka akiba kila mwaka. Kwa hiyo akaweka akiba ya chakula, kwa miaka 7 mfululizo, kwa ajili ya miaka 7 ya njaa iliyofuata.
• Wananchi wa Misri hawakuweka akiba ya nafaka bali waliweka akiba ya fedha na wanyama pekee – tena ya kutosha mwaka mmoja (1) tu. Mwaka wa 2 wa njaa walijiuza wao na ardhi yao kwa Farao ili kupata msaada ili wasife njaa.
Kumbuka: Ndoto zote mbili za Farao zilikuwa na msisitizo uliowekwa kwenye “muda”! Bila msisitizo huo wa muda, ujumbe uliokuwa kwenye ndoto zile, usingekuwa wa msaada kwa aliyeoteshwa ndoto!
Mfano wa 2: NDOTO ZA WAFANYAKAZI WA FARAO
Wafanyakazi hawa wawili wa Farao – mmoja alikuwa mkuu wa wanyweshaji na mwingine alikuwa mkuu wa waokaji. Biblia inasema "wakaota ndoto wote wawili kila mtu ndoto yake usiku mmoja, kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake…"(Mwanzo 40:5).
Yusufu aliyekuwa amefungwa nao gerezani – aliwapa tafsiri za ndoto zao…na kukuta zilikuwa na kipengele cha “muda”, kilichofanana katika ndoto zote mbili – za wale wafanyakazi wawili wa Farao!
Muda uliokuwepo kwenye ndoto zao ni “siku tatu” (Mwanzo 40:12,18) – zilikuwa na matukio mawili yaliyokuwa yatokee kwao “siku tatu” baada ya kuota ndoto zao!
Biblia inatupa habari ya kuwa “Ikawa siku ya tatu …Farao…akampandisha mkuu wa wanyweshaji katika kazi yake….Bali akamtundika mkuu wa waokaji, kama Yusufu alivyowafasiria” (Mwanzo 40:20 – 22).
Ndoto zile ziliwapa wahusika ujumbe wa kuwa kila mmoja wao alikuwa na “siku tatu” kabla ya matukio yaliyokuwa kwenye ndoto zile kutokea katika maisha yao!
Swali la msingi la kujiuliza ni kwa nini walipewa muda huo – ikiwa si kwamba walitakiwa kuzitumia kuhusiana na ujumbe uliokuwemo kwenye ndoto zile?
Mfano wa 3: NDOTO YA MKE WA PILATO
Kufuatana na Mathayo 28:19 – ndoto aliyoota mke wa Pilato, ilikuwa imebeba “muda” uliokuwa wa “usiku mmoja”, kama onyo na angalizo kwa mume wake, juu ya ushiriki wake katika maamuzi ya hukumu juu ya Yesu, iliyokuwa ifanyike kesho yake
Ni dhahiri familia ile ya Pilato ilishindwa kuutumia vizuri ule “muda” waliopewa katika ndoto ile!
Mfano wa 4: NDOTO YA NEBUKADREZA.
Hii ni ndoto tunayoipata katika Danieli 4:1 – 37. Ndani ya ndoto hii kulikuwa na “muda” wa aina mbili – na wenye kazi mbili tofauti.
“Muda” wa kwanza – na uliokuwa wazi, ni ule wa kipindi cha “adhabu” ya “nyakati 7” (Danieli 4:16, 23, 24), uliokuwa umekusudiwa kwa Nebukadreza – ikiwa hatabadili tabia zake.
“Muda” wa pili – na ambao haukuwa dhahiri sana, ni ule wa kipindi cha kuangalia ikiwa atafuata ushauri aliopewa – ili adhabu aliyopangiwa isimpate!
Danieli alimpa Nebukadreza ushauri huu: “Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kuwahurumia maskini, huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha” (Danieli 4:27).
Kufuatana na Danieli 4:28, mfalme Nebukadreza alipewa “miezi kumi na miwili” ili kufuata na kutekeleza ushauri wa Danieli. Lakini hakuufuata – na matokeo yake ni kuipata adhabu aliyoona imepangwa kwa ajili yake kwenye ndoto!
Pamoja na kwamba ndani ya ndoto hatujaona miezi 12 hiyo moja kwa moja – lakini ina maana ndoto ile iliendelea kukaa mawazoni mwake kwa mfululizo wa miezi kumi na mbili …ili asiipuuzie – lakini akaipuuzia!
Nakuombea ili Mungu akusaidie, ili ikiwa utaota ndoto yenye “muda” ndani yake – usije ukafanya kosa kama la mfalme Nebukadreza la kutojali ushauri ambao angeutekeleza – angeepuka adhabu iliyokuwa kwenye ndoto ile!
Mungu aendelee kukupa nafasi ya kulifuatilia somo hili kwa umakini kwa kadri ninavyokufundisha!
 
Principal Focus

JF-Expert Member
Jan 4, 2013
924
1,000
Bwana Yesu Asifiwe!
Leo nataka tuangalie sehemu ya 10 ya somo letu la ndoto, inayohusu;"uhusiano wa jina la Yesu na damu ya Yesu, ili uwe unapata ushindi juu ya mashambulizi ya shetani anayopitisha katika ndoto."
Hebu soma na kutafakari ndoto zifuatazo, halafu tuone tunajifunza nini ndani yake, juu ya mambo mawili hayo hapo juu.
Ndoto ya mtu wa 1: Mtu mmoja aliniandikia kuwa aliota yuko nyumbani kwao alikozaliwa. Na alipofika nyumbani kwao kwa wazazi wake, akatokea nyoka mbele akitaka kumuuma. Huyo mtu aliyeota ndoto hiyo, kwa kuwa alikuwa ameokoka, akamkemea yule nyoka mbele yake kwa jina la Yesu. Yule nyoka hakuondoka, badala yake akamrukia na kumuuma kwenye kidole cha mguu wake. Na alipoamka au alipozinduka toka usingizini, alikuta kile kidole alichoumwa na nyoka kwenye ndoto, kinauma na kutoa damu.
Ndoto za mtu wa 2: Mtu mwingine aliniandikia kuhusu ndoto zifuatazo alizoota: " Niliota kijana ameajiriwa kuniua na aliponiambia - nilikemea kwa jina la Yesu kwa nguvu zote - lakini alinizidi nguvu! Aliposogeza kisu ( kutaka kunichoma nacho), nikasema damu ya Yesu inenayo mema inishindie, aliniacha. Nikashtuka toka usingizini".
"Wiki iliyofuata nikatoka ndoto nyingine ya kuwa; niko msituni nimeshikwa na walinzi, halafu akaja mdada na kisu ili anichinje. Nikakumbuka kilichotokea kwenye ndoto ya wiki iliyopita, nikaita damu ya Yesu dhidi ya kile kisu, ghafla kikadondoka, na yule dada akaondoka hapo huku akikimbia. Nikashtuka toka usingizini".
Huyu mtu aliyeota ndoto hizo mbili kufuatana katika wiki mbili, alimalizia ujumbe huo alioniandikia kwa maneno yafuatayo:"Tangu kipindi hicho natafuta sana kujua juu ya damu ya Yesu. Asante kwa somo"
Ndani ya ndoto hizo za watu wawilu, tunajiuliza maswali ya msingi yafuatayo:
1. Kwa nini yule mtu wa kwanza alipotimia jina la Yesu kumkemea nyoka, hakuon ushindi, na badala yake akaumwa na yule nyoka?
2. Kwa nini yule mtu wa kwanza alishindwa kupata ushindi dhidi ya shetani, alipomshambulia kwenye ndoto, ingawa alikuwa ameokaka?
3. Kwa nini yule mtu wa pili aliona ushindi dhidi ya mashambulizi ya adui kwenye ndoto, kwa kutumia damu ya Yesu na si kwa kutumia jina la Yesu?
Je kuna uhusiano gani wa kimamlaka na wa kimatumizi, kati ya damu ya Yesu na jina la Yesu?
Kuna mambo ya msingi unayohitaji kuyafahamu, ikiwa unataka kupata majibu ya maswali hayo hapo juu.
Jina la Yesu ni jina lililofunuliwa na Mungu kwa wanadamu katika mazingira ya agano jipya. Hili tunalipata tunaposoma vitabu vya Waebrania 1:1 – 4, na Wafilipi 2:5 – 11, na Luka 1:30 – 35.
Kufuatana na maneno ya Waebrania 9:15 – 18, msingi na uhalali wa kutumika kwa agano jipya, ni kule kutumika kwa “damu” katika kuwepo kwake.
Na Yesu alipokuwa anashiriki chakula cha pasaka na wanafunzi wake kwa misingi ya agano alisema: “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu inayomwagika kwa ajili yenu” (Luka 22:20).
Kwa mantiki hii uhalali wa matumizi ya jina la Yesu, unategemea uhalali wa kimatumizi wa damu ya Yesu kwa mtumiaji wa jina la Yesu!
Ndiyo maana mahali ambapo damu ya Yesu inatakiwa itumike kwanza kabla ya kutumia jina la Yesu, utakuta jina la Yesu likitumika linakosa nguvu ya kimamlaka!
Ikitokea namna hii haina maana jina la Yesu halina nguvu – la hasha! Bali ina maana ya kuwa, mazingira ya kiroho ya jambo hilo, yanadai damu ya Yesu itumike kwanza kabla ya kutumia jina la Yesu! Kwa hiyo, ukiona kuna jambo unaloliombea kwa jina la Yesu, na huoni matokeo uliyotarajia – basi tumia damu ya Yesu, na utaona matokeo mazuri na ya ushindi.
Hili ndilo lililoweka tofauti ya kimatokeo katika matumizi ya jina la Yesu na damu ya Yesu kwenye ndoto nilizokushirikisha kwenye somo hili la leo.
Mazingira ya kiroho yanayodai matumizi ya jina la Yesu kwa msingi huu, ndiyo yaliyowafanya wana wa Skewa wasifanikiwe kutoa pepo kwa kutumia jina la Yesu.
Habari hii utaipata ukisoma Matendo ya Mitume 19:11 – 17. Jina la Yesu halikuwa na matokeo waliyoyataka, kwa sababu walikuwa hawajaitumia damu ya Yesu maishani mwao!
Kumbuka ya kuwa Damu ya Yesu ukiiamini na kuitumia kibiblia maishani mwako, inakupa uhalali wa kutumia jina la Yesu kwa mafanikio zaidi.
Ni vigumu kulitumia jina la Yesu kwa mafanikio, ikiwa kuna “lango” katika maisha yako ambalo shetani anatumia, au anaweza kulitumia kukushambulia.
Ni muhimu utumie damu ya Yesu KWANZA kuziba, au kulifunga hilo “lango” kwa damu ya Yesu, ndipo utaweza kuona matokeo mazuri hata utakapolitumia jina la Yesu!
Jambo jingine la kukumbuka kujiombea katika vita vinavyokujia kupitia kwenye ndoto – ni hili la kwamba Mungu akupe uwezo wa kushinda hivyo vita wakati unaota ndoto hiyo – ili kuondoa kwako madhara ya ndoto za vita vya kiroho katika maisha yako!
Nami nakuombea katika hilo wewe uliyesoma somo hili leo! Mungu azidi kukubariki sana!
 
mederii

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
801
500
Safi sana nimejifunza somo hili kupitia kwa mtumishi MWL Mwakasege
 
NANGA WA DEPO

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
657
1,000
USHAURI.
MKUU HAYA MASOMO UNGEYAWEKA YOTE KWENYE
THREAD MOJA TU...ITAKUWA NZURI ZAIDI,... ITATUPA URAHISI WA KUFUATILIA....

YAANI, SOMO LIKIONGEZEKA.....,,,,UNAPOST TU KAMA KOMENTI....KWENYE UZI MMOJA.

BARIKIWA.!!!
 
Inna

JF-Expert Member
Jan 13, 2017
10,946
2,000
USHAURI.
MKUU HAYA MASOMO UNGEYAWEKA YOTE KWENYE
THREAD MOJA TU...ITAKUWA NZURI ZAIDI,... ITATUPA URAHISI WA KUFUATILIA....

YAANI, SOMO LIKIONGEZEKA.....,,,,UNAPOST TU KAMA KOMENTI....KWENYE UZI MMOJA.

BARIKIWA.!!!
Kweli me sijaon ata hayo mengine yakowap?
 
EP PRO

JF-Expert Member
Nov 5, 2013
7,587
2,000
Labda niongeze kitu hapo.

Bible inasema na wote waliompokea amewapa huwezo wa kufanyika wana wa Mungu ,

pia alisema kwa Ombeni lolote kwa Jina langu namim nitafanya

Pia akasema nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na falme za giza.

lakin matukio yote lazima huwe na haki na jina hilo na uhalali. Ndio maana wale watu waliornda kutoa pepo kwa Jina la Yesu waliulizwa wao ni nan? maana hawakuwa na uhalali.

Huwezi kumuita Mungu ukiwa mchafu maan maombi ya mwenye dhambi ni kelele kwa Bwana, kwa hiyo lazima uoshwe huwe safi ,na tunaoshwa kwa damu ya Yesu then hapo utasikika vema sana kwa Mungu. Kuna baadhi ya matatizo chanzo chake au hukupata sababu ya dhambi tu, so ukioshwa n yenyewe yanatoka

( ndio maana kun wemgine Yesu alipo waponya alisema wasitende dhambi tena) ila kuna mengine yanatokan na mengi siwezi sema yote sasa.

ila hatua ni hizi, tafuta uhalali kwanza wa kulitumia Jina la Yesu kwa kuoshwa kwa damu yake then litumie

Note. kuna some cases Mungu hufanya ili ajitukuze tu.

Mungu anipe kibali kesho naweza kuja na somo la haki tutashare vitu kidogo.
 
Principal Focus

JF-Expert Member
Jan 4, 2013
924
1,000
[4/30, 8:30 AM] Principal Focus: Bwana Yesu asifiwe milele!
Leo nataka nianze kukufundisha juu ya: “Mambo unayohitaji kuyajua kuhusu ndoto unazoota ili iwe vyepesi kufanikiwa kimaisha”.
Jambo la 1: “Usiipuuzie ndoto uliyoota hata ikiwa hukijui chanzo cha ndoto hiyo!”
Mfano wa Kwanza: Unaposoma kitabu cha Mwanzo 41:1 – 7, unaona ndoto mbili alizoota Farao, kwa usiku mmoja, na kwa kufuatana. Ndoto zile mbili zilikuwa na tafsiri moja iliyofanana. Na zilikuwa na ujumbe mmoja uliofanana, uliokuwa unamjulisha ujio wa njaa nchini Misri miaka 7 baadaye – tokea wakati ule alipoota zile ndoto.
Farao alipoamka alijisemea moyoni mwake ya kuwa: “Kumbe ni ndoto tu” (Mwanzo 41:7). Hii ikiwa na maana ya kwamba wazo la kwanza lililomjia moyoni mwake, baada ya kuamka usiku ule, ni kuzipuuzia zile ndoto – na wala asiwe na mpango wa kuzifuatilia.
Lakini biblia inasema, “asubuhi roho yake ikafadhaika” (Mwanzo 41:8); ikiwa ni kiashiria chenye ujumbe toka kwa Roho Mtakatifu, kwamba asizipuuzie ndoto zile! Asante Yesu hakuzipuuzia, na akatafuta msaada, ili ajue tafsiri yake. Yusufu alimtafsiria zile ndoto na kumpa maelekezo yaliyoambatana na ndoto zile. Na Farao akatekeleza maelekezo aliyopewa. Na hata njaa ilipotokea miaka 7 baadaye haikuwasumbua – kwa kuwa ujumbe wa ndoto uliwapa kujiandaa.
Je, umewahi kujiuliza ingekuwaje kama Farao angezipuuzia zile ndoto? Ni dhahiri ya kwamba angezipuuzia – angeona tu baada ya miaka saba njaa kali yenye kudumu miaka saba – huku hajajiandaa nayo!Na kwa vile njaa ile ilikuwa ni ya “dunia yote” (Mwanzo 41:56,57), ina maana dunia yote ingekumbwa na njaa, kwa sababu tu ya Farao kuzipuuzia ndoto – ikiwa angeamua kuzipuuzia zile ndoto!
Mfano wa pili: Danieli 4:1 – 34 tunaelezwa madhara yaliyompata mfalme Nebukadreza, kwa sababu aliipuuzia ndoto aliyoota!
Ndoto ile – ilikuwa inampa onyo mfalme Nebukadreza, juu ya mwenendo wake aliokuwa nao wakati ule. Na ndoto ile ilimpa pia kujua adhabu atakayopewa asipobadili mwenendo wake. Lakini pia kwenye ndoto ile aliyoota, alipewa maelekezo ya mambo ya kufanya, ili aliyoyaona kwenye ndoto yasimpate – lakini alipuuzia! Soma Danieli 4:27. Tena – alipewa miezi 12 ya kujirekebisha – lakini alipuuzia – na wala hakuitumia nafasi hiyo – na matokeo yake yote aliyoyaona kwenye ndoto, yalimtokea katika maisha yake!Kwa kuipuuzia ile ndoto, Mfalme Nebukadreza aliingia kwenye adhabu ya maisha yake, na afya yake kuvurugika kwa nyakati saba au miaka 7! Na pia “nafasi” yake ilikosa uongozi kwa miaka 7!
Mfano wa tatu: Yusufu – yule aliyekuwa mume wa Mariamu, na mlezi wa Yesu wakati akiwa mtoto, aliota ndoto nne, ambazo angezipuuzia – historia ya ukristo isingekuwa ilivyo sasa!
Ndoto ya kwanza iliyoandikwa kwenye Mathayo 1:18 – 24 tunaona akihimizwa na “malaika wa Bwana”, kuwa asihofu kumchukua Mariamu akiwa na mimba. Na akajulishwa juu ya jina na kazi ya mtoto atakayezaliwa. Biblia inasema: “Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza;akamchukua mkewe” (Mathayo 1:24).
Ndoto ya pili iliyoandikwa kwenye Mathayo 2:13 – 18, Yusufu alionywa na Malaika wa Bwana, juu ya mipango ya mfalme Herode ya kutaka kumwua Yesu. Na akaelekezwa amchukue Yesu na mama yake awapeleke Misri – na akae kule Misri hadi malaika wa Bwana atakapompa maelekezo mengine!
Biblia inasema juu ya Yusufu baada ya kuota ndoto hiyo ya pili ya kuwa: “Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri” (Mathayo 2:14). Hata Herode alipotuma watu Bethlehemu kumtafuta Yesu na kumuua – wakakuta hayupo! Na kwa hasira aliua watoto wote wa kiume wa eneo lile; “tangu wenye miaka miwili na waliopungua” (Mathayo 2:16).
Ndoto ya tatu aliyoota Yusufu, iliyoandikwa katika Mathayo 2:19 – 21, ndiyo iliyomfanya aondoke Misri na familia yake, na kuanza kurudi nchini Israeli.
Ndoto ya nne aliyoota Yusufu, iliyoandikwa katika Mathayo 2:22 – 23, ndiyo iliyomfanya amchukue Yesu na mama yake, na kuwapeleka kuishi nao “katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazarayo” (Mathayo 2:23).
Huo ulikuwa ni utii wa hali ya juu sana kwa Yusufu! Hasa tukichukulia maanani ya kuwa Yesu hakuwa mtoto wake wa kumzaa; tena – maelezo ya kumtunza Yesu na hata kumwepusha na hatari zilizomkabili, alikuwa anapewa kwa njia ya ndoto – ambazo watu wengi wangeweza kuzipuuzia.
Lakini Yusufu hakuzipuuzia zile ndoto, na utii ule uliweka mwanzo mzuri wa Yesu, katika kumwandaa kwenye huduma, na kazi ya Mungu, aliyotumwa kuifanya duniani!
Je, wewe una kiwango gani cha utii kwa maelekezo ambayo Mungu anakuletea kwenye ndoto? Au kila ndoto unaipuuzia kama mfalme Nebukadreza? Je, unaweza ukapewa taarifa na Mungu kwa njia ya ndoto ukaielewa na kuitii?
Mtu mmoja aliyenisikiliza kwa njia ya redio tarehe 6 Nov, 2015, nikifundisha juu ya ndoto kwa kutumia biblia, alinitumia ujumbe ufuatao kwa njia ya simu:
“Bwana Yesu asifiwe – mwalimu! Mafundisho uliyotupa leo yamegusa maisha yangu, kwa sababu kuna ndoto niliota tarehe 24.12.2013 – sitaisahau siku hii! Niliota niko kijijini kwetu huko….napambana na nyoka. Huyo nyoka alikuwa amesimama usawa wangu – na akawa ananitishia kuning’ata. Na mimi nilikuwa namkemea kwa jina la Yesu. Lakini ghafla nikaona amenigonga, na kuniuma kwenye kidole cha pili cha mguu.
Ghafla nikashtuka toka usingizini. Nikakuta kidole kile alichonigonga na kuniuma yule nyoka katika ndoto, kinatoka damu na kinauma sana! Kulipokucha nikaenda kanisani kwetu, ambako siku hiyo kulikuwa na maombi ya kufunga. Mchungaji akawa anaombea wagonjwa. Akaniuliza unaumwa nini? Nikamjibu hivi: nimeota ndoto usiku …na kabla sijamaliza kujieleza nikaanguka.
Kuja kushtuka na kuamka, nikaambiwa nilikuwa na pepo mauti, ambaye waliweza kumkemea, na akaondoka toka mwilini mwangu.
Lakini tangu hapo maisha yangu yakayumba sana. Ijapokuwa nimeokoka…lakini sisongi mbele! Maisha yamekuwa magumu sana, na uchumi wangu umeyumba!Tena tangu siku hiyo niliyoota ndoto hii nilifukuzwa kwenye nyumba niliyokuwa nimepanga.Nikapanga nyumba nyingine – nayo pia tumefukuzwa mwezi wa sita mwaka huu”.
Huo ni ujumbe nilioandikiwa na mmoja wa wasikilizaji wa mafundisho yetu. Ni dhahiri ya kwamba maombi aliyopata yalimfungua kwa sehemu fulani, na kuna sehemu alikuwa bado hajafunguliwa!
Usiache kufuatilia somo hili kila wiki hapa hapa. Mungu aendelee kukubariki sana!

[4/30, 8:32 AM] Principal Focus: Bwana Yesu asifiwe!
Jambo la 2 tunalojifunza juu ya: “Mambo unayohitaji kuyajua kuhusu ndoto unazoota ili iwe vyepesi kufanikiwa kimaisha” ni hili:
“Ndoto ni mlango wa kiroho ndani ya mtu, unaomwingizia vitu maishani mwake kutoka vyanzo tofauti vya ndoto”
Ndoto ambazo mtu anaota, huwa hazina vyanzo vinavyofanana. Utofauti wa vyanzo vyake, unasababisha ufuatiliaji wake usifanane pia! Ukikosea kukijua chanzo cha ndoto uliyoota, uwe na uhakika wa kukosea pia namna ya kuishughulikia!
Kibiblia – ndoto ambazo mtu anaota, zinaweza kutokana na chanzo kimojawapo kati ya vyanzo vifuatavyo:
1. Ndoto zinazotoka kwa Mungu:
Biblia inasema kwenye kitabu cha Ayubu 33:14, 15 ya kuwa: “Mungu huwa anasema na mtu “mara moja”, na wakati mwingine hata mara mbili, kwa njia ya “ndoto”…usingizi mzito uwajiliapo watu”.
Njia mojawapo ambayo mfalme Sauli alitegemea Mungu angeitumia kujibu maombi yake, ilikuwa ni njia ya “ndoto” (1 Samweli 28:6). Asingetegemea Mungu amjibu maombi yake kwa njia ya ndoto, ikiwa huko nyuma alikuwa hajawahi kuona wala kusikia Mungu akifanya hivyo.
Na tunajulishwa ya kuwa, njia mojawapo ambayo Mungu atakuwa anaitumia kuwaongoza watu, akimtumia Roho Mtakatifu, ni kwa njia ya “ndoto” (Matendo ya Mitume 2:17).
2. Ndoto zinazotoka kwa shetani:
Ndoto hii inayotajwa katika Kumbukumbu ya Torati 13:1 – 4, ni wazi kwamba chanzo chake ni “shetani”. Hii ni kwa sababu maelekezo ya ndoto hiyo, ni kutaka mtu aache kumwabudu Mungu, na badala yake afuate miungu mingine. Hii inatudhihirishia ya kuwa, shetani anaweza akaingiza kitu ndani ya mtu, kwa kutumia njia ya ndoto.
3. Ndoto zinazotokana na mtu kuwa na shughuli nyingi:
Tunalijua hili kwa sababu ya kile tukisomacho kwenye kitabu cha Mhubiri 5:3 ya kuwa: “…ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi….!
Ndoto za namna hii zinaweza kumjia mtu, kwa sababu ya kujikuta amefanya “shughuli” zingine, ambazo hazipo kwenye ratiba ya Mungu – kwa ajili yake siku hiyo!
4. Ndoto zinazotokana na hali ya kiroho ya mahali ambapo mtu amelala:
Ndoto inayokuja kwa namna hii, tunaiona tunaposoma kitabu cha Mwanzo 28:10 – 17. Yakobo aliota ndoto ile, kwa sababu ya hali ya Kiroho ya ardhi ya eneo alilolala usiku ule!
Ndoto ile ilimpa ufahamu Yakobo kujua hali ya kiroho ya eneo lile, na ya ardhi ile. Ndiyo maana alisema: “Kweli Bwana yupo mahali hapa, wala mimi sikujua….hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni” (Mwanzo 28:16,17).
Utofauti huu wa vyanzo vya ndoto ambazo mtu anaweza kuota, unanisukuma moyoni kukushauri na kukuhimiza kujiombea mambo yafuatayo:
Jambo la 1: Jiombee ili Mungu akupe kujua chanzo cha ndoto unazoota ni kipi. Soma Danieli 2:27, 28.
Jambo la 2: Jiombee ili Mungu akiamua kukusemesha kwa njia ya ndoto, upate kusikia na kuelewa ujumbe uliomo ndani yake. Soma Ayubu 33:14, 15
Jambo la 3: Jiombee na “kuziba” kwa kutumia damu ya Yesu, lango la ndoto ndani yako, ili lisipitishe ndoto za shetani kuja kwako. Kumbuka Mungu aliwaambia wana wa Israeli wanaweza kutumia “damu” kumzuia Shetani asipite kwenye “milango” yao. Soma Kutoka 12:21 – 23
Jambo la 4: Kabla ya kulala jizoeze kuomba toba kwa Mungu, ikiwa umefanya “shughuli” zingine ambazo zilikuwa nje ya yale ambayo Mungu alikupangia kwa siku hiyo. Soma Luka 8:5 – 7,14.
Jambo la 5: Jizoeze kuombea mazingira ya Kiroho ya mahali unapolala usingizi – iwe ni mchana au iwe ni usiku. Hii ni muhimu kwa kuwa ikibidi uote ndoto, basi ziwe ni zile ambazo Mungu anataka kukujulisha jambo.
Mungu aendelee kukufafanulia na kukupa uelewa, wakati tukiendelea kujifunza somo hili.

[4/30, 8:33 AM] Principal Focus: Bwana Yesu asifiwe sana!
Leo tuangalie jambo la 3, katika yale ambayo ni vyema ukayafahamu juu ya ndoto, ili uweze kufanikiwa kimaisha.
Jambo hilo la 3 ni hili: “Zijue Ishara zitakazokuonyesha ya kuwa ni ndoto ipi uliyoota inayohitaji ufuatiliaji wa haraka”
Hizi zifuatazo ni baadhi ya ishara, nilizoweza kukukusanyia toka katika biblia, zitakazokusaidia kujua ikiwa ndoto uliyoota, inahitaji ufuatiliaji wa haraka, na wa makini.
Ishara ya 1: Kuiota ndoto ile ile zaidi ya mara moja! Yusufu alimwambia Farao hivi: “Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi”. (Mwanzo 41:32).
Hii haina maana yaliyomo katika ndoto huwezi kuyabadilisha – la hasha! Ukiota ndoto ile ile au zinazofana zaidi ya mara moja, ni ili ujue umuhimu wa kuyafuatilia yaliyomo kwenye ndoto hizo – kwa haraka na kwa makini. Wazo hili unalipata ukisoma Ayubu 33:14,15.
Ishara ya 2: Ndoto kukutia hofu – ambayo hata baada ya kuamka hofu hiyo unajikuta bado unaisikia! Mfalme Nebukadreza aliwahi kusema hivi juu ya ndoto aliyoota: “Nikaota ndoto iliyonitia hofu ….” (Danieli 4:5).
Kabla ya kuota ndoto ile, hakuwa na hofu. Ndoto aliyoota ilibeba roho ya hofu – iliyomwingia Nebukadreza wakati akiiota ndoto ile! Na alipoamka – alijikuta amejaa hofu kutokana na ndoto aliyoota.
Ishara ya 3: Kujisikia umefadhaika moyoni baada ya kuota ndoto! Tunasoma katika Danieli 2:1 ya kuwa: “Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, usingizi wake ukamwacha”.
Je, umewahi kusikia hali ya namna hii, mara tu baada ya kuzinduka usingizini baada ya kuota ndoto? Ikiwa hali ya namna hii imewahi kukupata – basi ujue ndoto hiyo ina ujumbe wa muhimu unaohitaji kuufahamu! Soma Danieli 2:28.
Ishara ya 4: Hali ya kufadhaika iliyoambatana na kitu kingine! Nebukadreza katika Danieli 2:1 – aliposikia kufadhaika baada ya kuota ndoto aliyoota – kuna hali nyingine zaidi iliyojitokeza kwake! Biblia inasema ya kwamba: “ na roho yake ilifadhaika, usingizi wake ukamwacha”!
“Mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri waliofungwa gerezani” na Yusufu, waliota “ndoto wote wawili, kila mtu ndoto yake usiku mmoja, kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake” (Mwanzo 40:5).
Biblia inasema, si tu kwamba Yusufu “akawaona wamefadhaika” (Mwanzo 40:6); lakini pia akawaona mfadhaiko ule waliokuwa nao, uliambatana na “nyuso” zao kukunjamana (Mwanzo 40:7).
Farao alipoota ndoto mbili mfululizo katika usiku mmoja, asubuhi yake “roho yake ilifadhaika” (Mwanzo 41:8). Ule mfadhaiko uliambatana na mahangaiko ya kutaka kupata tafsiri ya ndoto zile, bila kujali hali za kiroho za wale aliokuwa anawaulizia tafsiri zake (Mwanzo 41:8).
Mahangaiko ya Farao yalipokwama kupata tafsiri, ndipo Mungu alipomkumbusha mkuu wa wanyweshaji wake juu ya Yusufu, na akamkutanisha Farao na Yusufu. Yusufu akampa Farao tafsiri za ndoto zake, na maelekezo ya kufanya.
Ishara ya 5: Ndoto zinazosababisha jambo uliloota lijitokeze katika mwili wako! Unaposoma Ayubu 4:12 – 16, utatambua ya kwamba, Elifazi aliota ndoto iliyomtia hofu, na mifupa yake yote ilitetemeka. Unapolitafakari jambo hili, unaona uwezekano mkubwa wa Elifazi kusikia maumivu ya mifupa yake alipoamka, baada ya kuota ile ndoto.
Kuna mtu aliyeniandikia ujumbe wa simu mwaka 2016 akiomba nimwombee, ambaye alikuwa na maumivu katika mwili wake, yalisababishwa na ndoto aliyokuwa ameota. Mwaka 2009 aliota amepigwa risasi kwenye paja lake, na katika ndoto alipokuwa anaota, alijua risasi ilikuwa imebaki kwenye paja na ilihitaji kutolewa. Lakini aliamka toka usingizini kabla risasi haijatolewa!
Mwaka 2013 mguu wake ukaanza kuuma, na kuwa na maumivu makali kwenye eneo lile la paja palipopigwa risasi! Kwa nini? Kwa sababu ile “risasi ya kiroho” iliyompiga katika ndoto ilikuwa haijaondolewa!
Pia kuna dada mmoja ambaye alinisimulia ya kuwa aliota akicheza mpira wa miguu na wenzake. Na alipoupiga mpira kwa mguu wake, mara ule mguu ukaanza kumuuma. Na mara akaamka toka usingizini.
Lakini alishangaa alipoona ya kuwa, baada ya kuamka toka usingizini – mguu ule uliokuwa unauma kwenye ndoto ulikuwa bado unamuuma! Na tokea usiku ule alikuwa hawezi kutembea bila kuchechemea, kwa kuwa mguu ule uliendelea kumuuma.
Tulipokutana alipotoka hospitali na aliponieleza shida ile, nilijua tatizo lililompata. Nikamwombea na akapona muda ule ule nilipomwombea!
Ishara ya 6: Imani yako kwa Mungu katika Kristo Yesu au/na utumishi wako kwake kuanza kuyumba na kuhangaika na kupoa – baada ya kuota ndoto!
Tukisoma Kumbukumbu ya Totati 13: 1 – 4, tutaona ya kuwa, kuna ndoto ambazo lengo lake, ni kumwondoa mtu kwenye imani aliyonayo, kwa Mungu huyu tunayemwabudu katika Kristo Yesu.
Tena – tunaposoma Yeremia 23:25 – 17, tunajulishwa ya kuwa, kuna ndoto ambazo lengo lake ni kutaka kumsahaulisha mtu jina la Bwana Yesu!
Kwa hiyo – ukiona baada ya kuota ndoto imani yako, na utumishi wako kwa Mungu katika Kristo Yesu, vinaanza kupoa na kuyumba – ni ishara ya kuwa unahitaji kuifuatilia hiyo ndoto kwa haraka, na kwa umakini mkubwa kwa njia ya maombi.
Wengine waotao ndoto zenye malengo kama hayo; wanajikuta au hawaendi kanisani bila maelezo yanayoeleweka, au nguvu za maombi zinapotea, au wanajikuta hawana msukukumo tena hata wa kusoma biblia.
Ushauri wangu kwako kuhusu ishara hizi:
1. Hizi ishara zikiwa kubwa (“Strong”), au nzito (“heavy”) moyoni mwako – ina maana ufuatiliaji ufanyike kwa haraka – maana muda umekaribia wa kutimia yote uliyoyaona kwenye ndoto, ikiwa utayanyamazia! Labda kama unataka yatimie kama ulivyoyaona kwenye ndoto uliyoota.
2. Iandike ndoto unayoona ishara nilizokushirikisha, zinakupa kujua inahitaji kufuatiliwa. Iandike hiyo ndoto hata kama bado hujui tafsiri yake, wala ujumbe wake. Soma Habakuki 2:2 na Danieli 7:1
3. Anza kuiombea hiyo ndoto, na usiache kuiombea, hadi hizo “ishara” zilizokusukuma kuanza kuomba zimeondoka moyoni mwako au mwilini mwako!
Ni maombi yangu ya kuwa Mungu atasikia kuomba kwako!
Na Mungu azidi kukubariki!

[4/30, 8:33 AM] Principal Focus: Bwana Yesu asifiwe milele!
Jambo la 4 kati ya “Mambo unayohitaji kuyajua kuhusu ndoto unazoota ili iwe vyepesi kufanikiwa kimaisha” ni hili:
“Ikiwa umeota ndoto ambayo tafsiri yake huijui ufanyeje?”
1. OMBA MUNGU AKUPE UFAHAMU JUU YA NDOTO! UFAHAMU HUU JUU YA NDOTO, UKIUPATA TOKA KWA MUNGU KATIKA KRISTO YESU, UTAKUSAIDIA WEWE NA WATU WENGINE PIA!
Biblia inatueleza ya kuwa: “Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto” (Daniel 1:17).
Kufuatana na Wakolosai 1:9, Mtume Paulo akiongozwa na Roho Mtakatifu aliwaombea wakristo waliokuwepo Kolosai wakati ule, wajazwe “maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni”.
Naamini hata katika nyakati za sasa, Roho Mtakatifu yupo tayari kutuongoza tujazwe “ufahamu wa rohoni”. Naamini ufahamu huu wa rohoni unahusu pia ufahamu juu ya ndoto!
2. USITAFUTE TAFSIRI YA NDOTO TOKA KWA MTU YE YOTE TU UNAYEDHANI ANAWEZA KUKUSAIDIA!
Kitabu cha Mwanzo 40:8 tunasoma swali hili: “Kufasiri si kazi ya Mungu” Hayo yalikuwa maneno ya Yusufu akiwahakikishia “Mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri”, juu ya upatikanaji wa tafsiri juu ya ndoto walizokuwa wameota!
Farao alipoota ndoto zake mbili mfululizo zilizofanana, tena kwa usiku mmoja (Mwanzo 41:1 – 7), alitafuta tafsiri ya ndoto zile mahali ambapo hakutakiwa kutafuta!
Farao alitafuta wapi kwanza juu ya tafsiri zake za ndoto alizoota usiku ule? Biblia inasema: “Farao akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko…akawahadithia ndoto zake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria…” (Mwanzo 41:8).
Ni mpaka alipotafutwa Yusufu aliyekuwa gerezani wakati ule, ili amtafsirie Farao ndoto zake. Yusufu akamwambia Farao: “Si mimi, Mungu atampa Farao majibu ya amani” (Mwanzo 41:16).
Ni wazi ufahamu aliokuwa nao Yusufu juu ya ndoto, ulikuwa mkubwa kuliko wa waganga na wachawi wote waliokuwa nchini Misri wakati ule!
Mfalme Nebukadreza aliona jambo kama hili kwa Danieli, alipomlinganisha na waganga na wachawi waliokuwa kwenye himaya yake alipokuwa anatawala.
Biblia inatueleza ya kuwa: “Danieli…alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto” na alifaa “mara kumi zaidi ya waganga na wachawi waliokuwa katika ufalme wake” (Danieli 1:17,20).
Ni kweli kuna mtu ambaye anaweza kukupa tafsiri ya ndoto yako, lakini asiweze kukupa ujumbe uliomo katika ndoto hiyo! Kupewa tafsiri ya ndoto, bila kupewa ujumbe unaoambatana na ndoto hiyo; ni sawa na kula chakula na ukashiba huku hakina virutubisho kwa afya yako.
3. OMBA MUNGU AKUPE KUJUA UJUMBE ULIOMO KWENYE NDOTO ULIYOOTA, ILI USIISHIE KUPATA TAFSIRI YA NDOTO BILA KUJUA UJUMBE WAKE!
Ukisoma kitabu cha Danieli 4:4 – 18, utaona ya kuwa kiu aliyokuwa nayo mfalme Nebukadreza, ilikuwa ni kujua tafsiri ya ndoto aliyoota, na si ujumbe uliokuwa ndani ya ndoto kwa ajili yake!
Lakini Danieli alimpa mfalme Nebukadreza vyote viwili – tafsiri ya ndoto (Danieli 4:20 – 26), na ujumbe uliokuwemo kwenye ndoto ile kwa ajili yake (Danieli 4:27).
Na kwa sababu mfalme Nebukadreza alitaka tafsiri ya ndoto, na si ujumbe wa ndoto, alijikuta akipuuzia na kutokutilia maanani ujumbe wa ndoto aliopewa, wala hakuufuatilia! Na matokeo yake ni maisha ya mateso ya miaka saba, kwa ajili yake, na kwa ajili ya familia yake, na kwa ajili ya serikali ya ufalme wake.
Unapoendelea kutafakari juu ya jambo hili, ni vizuri nikujulishe pia yafuatayo:
(i) Kuna ndoto ambazo zimebeba vitu vinavyohitaji tafsiri ili uweze kupata ujumbe uliomo ndani yake. Mfano wa ndoto kama hizi tunaupata katika Mwanzo 40:5 – 23
(ii) Kuna ndoto ambazo zimebeba vitu ambavyo maana yake iko wazi, na kwa ajili hiyo havihitaji tafsiri yake, ili kuupata ujumbe uliomo ndani yake. Soma mfano wake katika Mathayo 1:18 – 24.
(iii) Kuna ndoto ambazo zina ujumbe peke yake, bila kubeba vitu vyovyote zaidi ndani yake. Soma mfano wake katika Mathayo 2:12,22 na Mwanzo 31:24,29.
(iv) Mfasiri sahihi wa ndoto na ujumbe uliomo ndani yake ni Mungu tunayemwabudu katika Kristo Yesu; bila kujali chanzo cha ndoto uliyoota!
4. UWE NA NENO LA BIBLIA LA KUTOSHA NDANI YAKO – TENA KATIKA HEKIMA YOTE!
Wakolosai 3:16 inasema hivi: “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana…”
Kwa nini jambo hili ni la muhimu katika kutafsiri ndoto na kupata ujumbe uliomo ndani yake? Hii ni kwa sababu kufuatana na Ayubu 33:14,15 – ndoto ni neno katika picha!
Na kwa kuwa “kusikia huja kwa neno la Kristo” (Warumi 10:17), basi ujue bila neno la Kristo ndani yako huwezi “kusikia” ujumbe uliomo ndani ya ndoto – hata kama unajua tafsiri ya ndoto hiyo!
Hebu tuangalie mfano juu ya Biblia inasema nini kuhusu tafsiri ya ndoto zinazohusu madarasa, au kusoma, au kufanya mitihani; na ujumbe uliomo ndani yake.
Ukisoma kitabu cha Danieli 1: 3 – 20 unaweza kujifunza yafuatayo juu ya ndoto hizo:
(i) Maandalizi yanahitajika kwa ajili ya hatua iliyo mbele yako, au hatua unayotaka Mungu akupe unapoomba katika maombi yako.
(ii) Kuota “shule” au “chuo” maana yake maandalizi ya hatua fulani iliyo mbele yako yanahitaji utaratibu maalumu.
(iii) Kuota “shule” au “chuo” ulichowahi kusoma zamani, ina maana kwamba kuna jambo lililotokea hapo ulilotakiwa “kuvuka” – lakini hukuweza kuvuka, na kwa hiyo kuna eneo limekwama kwenye maisha yako.
(iv) Watu mlio nao darasani katika ndoto ina maana watu mlio ngazi moja ya kimaandalizi
(v) Kuota ndoto uko darasani na watu uliowahi kusoma nao zamani au unaota unarudia darasa, au unarudia mtihani – ina maana umekwama mahali kimaisha na unahitaji maandalizi ili kuvuka hapo.
(vi) Ukiota hukai darasani wakati wengine wako darasani; au hukai kwenye mtihani wakati wengine wanafanya mitihani – ina maana huna utulivu unaotakiwa uwe nao ili uweze kujiandaa vyema kwa hatua iliyo mbele yako
(vii) Ukiota unafanya mtihani – ujue: au unapita mahali kimaisha ambapo unapimwa kiwango chako ulichofikia kimaandalizi; au mbele yako kuna kuja kipimo kwa ajili ya kujua ikiwa umefikia kiwango kinachotakiwa kwa wewe kuingizwa hatua nyingine ya maisha
(viii) Ukiota unaota unasoma, na ukaona na somo unalosoma, au ukaota unafanya mtihani na ukaona somo la mtihani huo – ina maana unaonyeshwa aina ya, au eneo la – maandalizi unalotakiwa kulifuatilia kimaandalizi
Kumbuka – huu ni mfano tu wa kutafsiri ndoto na kupata ujumbe uliomo ndani yake kwa kutumia neno la biblia.
Mungu aendelee kukubariki unapoendelea kujifunza somo hili la ndoto.

[4/30, 8:35 AM] Principal Focus: Bwana Yesu asifiwe milele!
Ndani ya somo lililotangulia kabla ya hili, nilikuwa najibu swali hili: “Ikiwa umeota ndoto ambayo tafsiri yake huijui ufanyeje?”
Nilipokuwa nakupa majibu ya swali hilo, nilikufundisha vipengele vinne muhimu, katika kutafsiri ndoto. Leo – nataka nikufundishe kipengele cha tano, kitakachoweza kukusaidia katika kutafsiri ndoto unazoota, kipengele hicho ni hiki: “ANGALIA ULICHOKUWA UNAWAZA KUKIFANYA KABLA YA KUOTA NDOTO ULIYOOTA”
Waefeso 3:20 inatukumbusha ya kuwa, Mungu anaweza “kufanya mambo ya ajabu mno, kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo…”Kwa hiyo – ikiwa Mungu anatumia “ndoto” kama njia mojawapo ya kuwasiliana na watu (Ayubu 33:14,15) ina maana Mungu anaweza kutumia “ndoto” kujibu mawazo ya mtu, au kufikiri kwa mtu, au maombi ya mtu!
Ndiyo maana kwenye kipengele hiki cha tano, juu ya kutafsiri ndoto, nasisitizia umuhimu wa kuangalia ulichokuwa unawaza kukifanya kabla ya kuota ndoto uliyoota!
Hebu tujifunze jambo hili kwa mifano ifuatayo:
MFANO WA 1: YUSUFU ALIPOTAKA KUMKIMBIA MARIAMU.
Ukisoma habari iliyoandikwa katika Mathayo 1:18 – 20, utaona ya kwamba, kulikuwa na uhusiano wa kile ambacho Yusufu alikuwa anafikiria kukifanya, na ndoto aliyoota!Wakati huo Yusufu ambaye alikuwa anajiandaa kumwoa Mariamu – “akaazimu kumwacha kwa siri”, baada ya kusikia kwamba alikuwa mja mzito.
Biblia inasema; “Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema…usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu”.Ni dhahiri ndoto ile aliyoota Yusufu ilikuja ili kujibu alichokuwa anafikiri kukifanya – kumwonyesha ya kuwa hakikuwa sahihi!
Yusufu aliamua au aliazimu kumwacha Mariamu, kwa kuwa hakuwa na ufahamu wa kutosha juu ya mimba ya Mariamu. Ndoto ile ilimpa ufahamu, uliomsaidia kubadili kile alichokuwa anafikiria kukifanya.
MFANO WA 2: MAMAJUSI
Mamajusi waliombwa na Mfalme Herode, wampe taarifa ikiwa watajua Yesu alipozaliwa, ili naye aende kumsujudia
Ukisoma Mathayo 2:1 – 18 utajua ya kuwa si kweli kwamba Herode alitaka kujua Yesu alipozaliwa ili amsujudie – bali apate kumwua! Lakini Mamajusi hawakujua hila hizo za Herode! Kwa hiyo – walipomaliza kumsujudia Yesu na kumpa zawadi walizompelekea, wakawa wanajiandaa kurudi kwa Herode kumpa taarifa ya mahali Yesu alipokuwepo.
Ndipo biblia inasema; “Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine’ (Mathayo 2:12). Mungu aliingilia kati kwa njia ya ndoto, kuwazuia Mamajusi wasifanye kile walichokuwa wanafikiria kukufanya!
Tunaona tena katika mfano huu wa pili, umuhimu wa kufuatilia ulichokuwa unawaza – kama njia mojawapo ya kukusaidia kujua tafsiri ya ndoto uliyoota!
MFANO WA 3: KUHAMIA KANISA LINGINE
Kuna mtu aliyenishirikisha ndoto hii ifuatayo, baada ya kuamua moyoni mwake, kutaka kuhama toka Kanisa alilokuwa anasali, na kuhamia kanisa lingine – ambalo yeye aliona ni bora kuliko lile alilokuwa anasali wakati huo. Aliota ndoto ambayo ndani yake alimwona mchungaji wa Kanisa alilotaka kuhamia. Mchungaji huyo alikuwa anawaongoza waumini wake kuelekea porini – huku na yeye aliyeota ndoto hiyo akiwemo kwenye kundi hilo.
Na huko porini wakapotea njia na hawakujua pa kutokea – mchungaji wao na waumini wake. Na akaamka toka usingizini wakiwa wamepotea porini!
Mtu huyo alipoamka toka usingizini, na kuitafakari ndoto aliyoota – alijua Mungu alikuwa amemtumia ujumbe kwa njia ya ndoto aliyoota, ya kuwa uamuzi wa kuhamia kanisa alilotaka kuhamia, haukuwa sahihi! Na ikiwa ataamua kupuuza onyo lile, basi, angejikuta amepotea kiroho na kimaisha!
Yule mtu aliyeota ndoto ile, akanieleza ya kuwa aliamua kusitisha uamuzi wake wa kuhama kanisa kama alivyokuwa anataka kufanya!
Kumbuka: Njia mojawapo itakayokusaidia kutafsiri ndoto uliyoota, ni wewe kutathmini mawazo uliyokuwa unawaza kabla ya kuota ndoto uliyoota. Hii ni muhimu kwa sababu, ndoto hiyo inawezekana imeletwa kwako ili kujibu, au kurekebisha, au kuonya, au kuthibitisha - misimamo ya mawazo uliyokuwa unawaza, kabla ya kuota ndoto hiyo uliyoota!
Mungu aendelee kukubariki unapoendelea kujifunza somo hili pamoja nasi!

[4/30, 8:35 AM] Principal Focus: Jina la Yesu litukuzwe milele!
Jambo la 5 kati ya “Mambo unayohitaji kuyajua kuhusu ndoto unazoota ili iwe vyepesi kufanikiwa kimaisha” ni hili hapa:
“Omba Mungu akupe kujua muda uliomo katika ndoto, unaokupa kuomba na kujiandaa, au kubadili kuhusu uliyoota”.
Si ndoto zote zina kipengele cha “muda” wa namna hii, ingawa nyingi zinao, lakini wengi wanashindwa kuufuatilia!
Hebu tujifunze jambo hili kwa mifano ifuatayo:
Mfano wa 1: NDOTO ZA FARAO
Habari za ndoto hizi tunazipata tunaposoma Mwanzo 41:1 – 36. Ndoto zote mbili alizoota Farao katika usiku mmoja, zilikuwa na msisitizo mkubwa uliowekwa kwenye “muda”!
• Ndoto zote zilikuwa na matukio ya jumla ya “muda” wa miaka 14.
• Miaka 7 ya shibe ilihitajika kwa ajili ya kujiandaa, kwa ajili ya miaka 7 ya njaa.
• Sehemu ya 5 ya mavuno ya mwaka mmoja (1) wa shibe, ilihitajika kwa ajili ya mahitaji ya chakula ya mwaka mmoja (1) mzima wa njaa
• Maarifa yalihitajika kwa ajili ya kukusanya mavuno ya kila mwaka katika miaka 7 ya shibe; ili kupata na kutenga, na kulinda sehemu ya 5 kama akiba katika miji.
• Yusufu aliamua kutokuwa “mvivu” wa kuweka akiba kila mwaka. Kwa hiyo akaweka akiba ya chakula, kwa miaka 7 mfululizo, kwa ajili ya miaka 7 ya njaa iliyofuata.
• Wananchi wa Misri hawakuweka akiba ya nafaka bali waliweka akiba ya fedha na wanyama pekee – tena ya kutosha mwaka mmoja (1) tu. Mwaka wa 2 wa njaa walijiuza wao na ardhi yao kwa Farao ili kupata msaada ili wasife njaa.
Kumbuka: Ndoto zote mbili za Farao zilikuwa na msisitizo uliowekwa kwenye “muda”! Bila msisitizo huo wa muda, ujumbe uliokuwa kwenye ndoto zile, usingekuwa wa msaada kwa aliyeoteshwa ndoto!
Mfano wa 2: NDOTO ZA WAFANYAKAZI WA FARAO
Wafanyakazi hawa wawili wa Farao – mmoja alikuwa mkuu wa wanyweshaji na mwingine alikuwa mkuu wa waokaji. Biblia inasema "wakaota ndoto wote wawili kila mtu ndoto yake usiku mmoja, kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake…"(Mwanzo 40:5).
Yusufu aliyekuwa amefungwa nao gerezani – aliwapa tafsiri za ndoto zao…na kukuta zilikuwa na kipengele cha “muda”, kilichofanana katika ndoto zote mbili – za wale wafanyakazi wawili wa Farao!
Muda uliokuwepo kwenye ndoto zao ni “siku tatu” (Mwanzo 40:12,18) – zilikuwa na matukio mawili yaliyokuwa yatokee kwao “siku tatu” baada ya kuota ndoto zao!
Biblia inatupa habari ya kuwa “Ikawa siku ya tatu …Farao…akampandisha mkuu wa wanyweshaji katika kazi yake….Bali akamtundika mkuu wa waokaji, kama Yusufu alivyowafasiria” (Mwanzo 40:20 – 22).
Ndoto zile ziliwapa wahusika ujumbe wa kuwa kila mmoja wao alikuwa na “siku tatu” kabla ya matukio yaliyokuwa kwenye ndoto zile kutokea katika maisha yao!
Swali la msingi la kujiuliza ni kwa nini walipewa muda huo – ikiwa si kwamba walitakiwa kuzitumia kuhusiana na ujumbe uliokuwemo kwenye ndoto zile?
Mfano wa 3: NDOTO YA MKE WA PILATO
Kufuatana na Mathayo 28:19 – ndoto aliyoota mke wa Pilato, ilikuwa imebeba “muda” uliokuwa wa “usiku mmoja”, kama onyo na angalizo kwa mume wake, juu ya ushiriki wake katika maamuzi ya hukumu juu ya Yesu, iliyokuwa ifanyike kesho yake
Ni dhahiri familia ile ya Pilato ilishindwa kuutumia vizuri ule “muda” waliopewa katika ndoto ile!
Mfano wa 4: NDOTO YA NEBUKADREZA.
Hii ni ndoto tunayoipata katika Danieli 4:1 – 37. Ndani ya ndoto hii kulikuwa na “muda” wa aina mbili – na wenye kazi mbili tofauti.
“Muda” wa kwanza – na uliokuwa wazi, ni ule wa kipindi cha “adhabu” ya “nyakati 7” (Danieli 4:16, 23, 24), uliokuwa umekusudiwa kwa Nebukadreza – ikiwa hatabadili tabia zake.
“Muda” wa pili – na ambao haukuwa dhahiri sana, ni ule wa kipindi cha kuangalia ikiwa atafuata ushauri aliopewa – ili adhabu aliyopangiwa isimpate!
Danieli alimpa Nebukadreza ushauri huu: “Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kuwahurumia maskini, huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha” (Danieli 4:27).
Kufuatana na Danieli 4:28, mfalme Nebukadreza alipewa “miezi kumi na miwili” ili kufuata na kutekeleza ushauri wa Danieli. Lakini hakuufuata – na matokeo yake ni kuipata adhabu aliyoona imepangwa kwa ajili yake kwenye ndoto!
Pamoja na kwamba ndani ya ndoto hatujaona miezi 12 hiyo moja kwa moja – lakini ina maana ndoto ile iliendelea kukaa mawazoni mwake kwa mfululizo wa miezi kumi na mbili …ili asiipuuzie – lakini akaipuuzia!
Nakuombea ili Mungu akusaidie, ili ikiwa utaota ndoto yenye “muda” ndani yake – usije ukafanya kosa kama la mfalme Nebukadreza la kutojali ushauri ambao angeutekeleza – angeepuka adhabu iliyokuwa kwenye ndoto ile!
Mungu aendelee kukupa nafasi ya kulifuatilia somo hili kwa umakini kwa kadri ninavyokufundisha!

[4/30, 8:39 AM] Principal Focus: Bwana Yesu asifiwe sana sana!
Leo nataka nikushirikishe jambo la 6 kati ya “Mambo unayohitaji kuyajua kuhusu ndoto unazoota ili iwe vyepesi kufanikiwa kimaisha”.
Jambo hilo la 6 ni hili: “Ng’oa kilichopandikizwa na shetani ndani yako kwa njia ya ndoto, na kuondoa madhara yake!”
Ndoto ambazo chanzo chake ni shetani, huwa zina tabia ya “kupandikiza” mambo mabaya kwenye maisha ya mtu aliyeoteshwa ndoto hizo!
Ukisoma kitabu cha Ayubu 4:12 – 16, utaona ya kuwa, Elifazi aliota ndoto iliyopandikiza vitu vifuatavyo kwenye maisha yake:
• Mawazo yake yalipokea neno ambalo kabla ya kuota ndoto ile halikuwemo mawazoni mwake;
• Alisikia “Sauti” kwenye masikio yake;
• Hofu “ilimwangukia” katika mwili wake;
• Mifupa yake ilianza kutetemeka
Ukiyaangalia maandiko hayo kwa mtazamo huu, utajua ya kuwa ndoto ile “ilipandikiza” katika maisha ya Elifazi vitu visivyopungua vinne!
Na vitu hivyo vinne vilimsumbua Elifazi na kwa sababu hiyo angetamani viondoke katika maisha yake, kama angekuwa anajua la kufanya ili kuving’oa!
Ningekuwa katika mazingira ya kumwombea Elifazi juu ya kilichomtokea baada ya kuota ndoto aliyoota – ningemwombea mambo yafuatayo:
(i) Toba kwa kile kilichosababisha “lango” lake la ndoto kufunguka na kupitisha ndoto na vile vilivyobebwa na ndoto ile.
Toba hii ni muhimu ili kwa kupitia msamaha wa Mungu, shetani apoteze uhalali wa kuendelea kumshambulia Elifazi kwa kutumia “lango” lake la ndoto
Na pia toba hiyo inatengeneza “uhalali” katika ulimwengu wa roho, wa Mungu kumsaidia Elifazi apate kushinda “vita” iliyopitia kwenye “ndoto” aliyoota!
(ii) Kung’oa “neno” lisilokuwa la Ki – Mungu lililoingia kwenye mawazo yake kwa kupitia kwenye ndoto aliyoota;
(iii) Kunyamazisha kwa kutumia Damu ya Yesu – “sauti” za kigeni ambazo Elifazi anazisikia “ndani yake” tangu alipoota ndoto ile;
(iv) Kukemea roho ya hofu iliyomwangukia ili iondoke katika maisha yake;
(v) Kumuombea uponyaji wa mifupa yake ili iache kutetemeka, au ili mifupa yake ipone “ugonjwa” wa kutetemeka alioupata tangu siku ile aliyoota ile ndoto!
(vi) Kuziba kwa Damu ya Yesu “lango” lake la ndoto, ili asiote tena ndoto zenye kumletea mashambulizi ya kipepo katika maisha yake!
Ufahamu huu umenisaidia kuwaombea watu wengi ambao walipata mashambulizi ya shetani kwa kupitia kwenye ndoto walizoota.
Kwa – mfano niliwahi kukutana na dada mmoja akitokea hospitali huku mguu wake mmoja akitembea kwa kuchechemea
Nilipomuuliza chanzo cha kuchechemea kwake, akanijibu ya kuwa ilikuwa ni matokeo ya ndoto aliyoota usiku
Ndoto aliyoota alimhusisha yeye akicheza mpira na wenzake, na alipoupiga mpira yeye, mguu wake ukaanza kuuma kwenye ndoto hiyo! Na baada ya hapo akaamka toka usingizini!
Na hata baada ya kuamka toka usingizini akaona mguu alioumia kwenye ndoto akicheza mpira, unaendelea kuuma. Na alipojaribu kutembea alijikuta akichechemea kwa sababu ya maumivu aliyokuwa – nayo kwenye mguu wake, ulioumia alipoupiga mpira kwenye ndoto aliyoota.
Nikamwombea pale pale njiani tulipokutana naye – na maumivu ya mguu yakapona wakati ule ule, na akaweza kuondoka pale huku akitembea bila kuchechemea!
Mfano mwingine ni huu: Mama mmoja aliniandikia kwa ujumbe wa simu ya kuwa aliwahi kuota ndoto ambayo ndani yake nyoka alimuuma yeye kwenye kidole alichokuwa na pete ya ndoa.
Na tangu wakati ule alioota hiyo ndoto, alijikuta akimchukia na kumkinai mume wake.
Lakini alipokuwa anasikiliza kwa njia ya redio mafundisho ya ndoto niliyokuwa nafundisha, na kushiriki maombi ya kung’oa kilichopandwa na shetani kwa njia ya ndoto, alijikuta akitapika povu jeupe!
Na baada ya maombi hayo, hali ya kumchukia na kumkinai mume wake iliisha, na badala yake, hali ya kumpenda ilirudi ndani yake kwa upya!
Je, kuna ndoto uliyoota unayoona ya kuwa “imepandikiza” kitu kibaya kwenye mawazo yako, au katika mwili wako, au katika nafsi yako, au katika roho yako, au katika maisha yako?
Pitia kwa upya hatua za kimaombi, nilizoziweka katika somo la leo, nilipokuwa natoa mfano wa kumwombea Elifazi wa Ayubu 4:12 – 16.
Hatua hizi zitakupa mwongozo wa kujiombea na wa kuwaombea wengine waliopata matatizo kwa njia ya ndoto.
Mungu akubariki sana!

[4/30, 8:39 AM] Principal Focus: Bwana Yesu asifiwe milele!
Wakati huu nataka nikuletee na kukushirikisha jambo la 7, kati ya “Mambo unayohitaji kuyajua kuhusu ndoto unazoota ili iwe vyepesi kufanikiwa kimaisha”

Jambo hilo la 7 ni hili: “Imarisha imani yako inayohusu kutumia Damu ya Yesu ili ikusaidie kuombea ndoto kwa mafanikio zaidi”
Kuna dada mmoja aliyeokoka, aliyekuja kwangu kuhitaji maombi, juu ya ndoto iliyokuwa inamsumbua mara kwa mara.
Huyo dada alinisimulia ya kuwa kuna mwanaume aliyemkataa asimwoe, lakini alikuwa anamjia kwenye ndoto mara kwa mara na kuzini naye. Na alipokuwa akizinduka usingizini baada ya kuota ndoto hiyo, alikuwa anaona kwenye mwili wake dalili zilizokuwa zikimwonyesha kuwa ametoka kuzini na mtu.
Na kilichomsumbua zaidi ni kule kuona ya kuwa maombi aliyokuwa anajiombea kabla ya kulala, hayakuweza kuizuia ile ndoto! Na mtu yule mwanaume aliendelea kumjia kwenye ndoto na kuzini naye!
Mimi nilimwombea ulinzi wa damu ya Yesu juu yake, na kuizuia ile ndoto isiendelee kumrudia. Na tulipoonana siku nyingine, akanisimulia ya kuwa tangu siku ile niliyomwombea, ile ndoto ilikoma na hakuiota tena!
Halafu akaniuliza swali hili: “Mbona mimi nilipoomba ulinzi kwa damu ya Yesu ile ndoto ikome,sikufanikiwa, lakini wewe ulipoomba ulinzi kwa damu ya Yesu, ulifanikiwa na ndoto ikakoma? Je, tofauti ya kuomba kwangu na kule kuomba kwako ilikuwa ni nini?
Mimi nikamjibu ya kuwa: “tofauti ya kuomba kwetu – yaani kati ya mimi na yeye, ilikuwa ni imani tulizokuwa nazo juu ya damu ya Yesu”
Ukifuatilia maeneo yafuatayo ya neno la Mungu juu ya damu ya Yesu, uwe na uhakika ya kuwa imani yako juu ya damu ya Yesu itaimarika, na utaweza kuitumia kwa mafanikio zaidi.
Maelekezo nitakayokupa hapa leo, yasome na uyatafakari, na yafanyie kazi! Hii ni kwa sababu: “Imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo” (Warumi 10:17).
Lakini kuwa na imani peke yake hakutoshi! Hii ni kwa sababu “imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake;…haizai;..imekufa”(Yakobo 2:17,20,26).
Eneo la 1: “Ikiwa unamwamini Yesu, basi iamini na Damu yake pia!”
Yesu aliwahi kuwambia wanafunzi wake maneno haya: “Mnamwamini Mungu, niaminini na mimi” (Yohana 14:1). Kwa nini Yesu aliwaambia maneno haya?
Yesu aliona ya kuwa – wanafunzi wake walikuwa na imani na Baba yake, lakini hawakuwa na imani na yeye! Na kwa kutokuwa na imani na yeye, kulikuwa na vitu ambavyo wasingeweza kuvipata (Yohana 6:40); na wasingeweza kuvifanya (Yohana 14:12)!
Yesu alitaka wanafunzi wake, wawe na imani na Baba yake, na wawe pia na imani na yeye!
Vivyo hivyo ni muhimu ujue ya kuwa, ile kwamba unamwamini Yesu, haina maana unaiamini na Damu yake pia! La sivyo Warumi 3:25 isingetuhimiza tuwe na “imani katika Damu yake” Yesu! Hii ni kwa sababu, kuna vitu ambavyo Mungu na Yesu hawawezi kuvifanya bila ya imani yetu juu ya Damu ya Yesu kuhusika!
Imani hii juu ya Damu ya Yesu unaipataje? Kufuatana na Warumi 10:17 inakubidi usome na usikie neno la Mungu la biblia linavyosema juu ya Damu ya Yesu!
Eneo la 2: “Zijue na uzipate aina zote za imani zinazohusu Damu ya Yesu!”
Zipo aina mbalimbali zinazohusu Damu ya Yesu, lakini ngoja nikupe mifano ya aina mbili tu za aina ya hizi za imani juu ya damu ya Yesu
Aina ya kwanza: Ni imani juu ya uwezo uliomo katika Damu ya Yesu; na aina ya pili ni imani inayokuwezesha wewe uitumie Damu ya Yesu!
Ili uweze kulielewa jambo hili vizuri, tafakari mfano huu: Kuna tofauti kati ya imani uliyonayo juu ya uwezo uliomo katika gari; na imani uliyonayo katika kuitumia hiyo gari!
Imani juu ya uwezo wa gari unakufanya iwe rahisi kwako kukubali uwe abiria wa gari hilo, lakini unaweza usiwe na uwezo wala imani ya kuliendesha wewe mwenyewe!
Imani inayokuwezesha uiendeshe gari, inakusukuma “ujifunze” kuiendesha gari hilo “kihalali”, badala ya kutaka tu uwe abiria wakati mtu mwingine anaendesha!
Je unajua ya kuwa Mungu haitumii damu ya Yesu ambayo huitumii? God does not use the blood of Jesus you have stored somewhere without using it! You have to use it, or apply it - for God to use it in order for Him to help you!
Hii ninaipata katika Kutoka 12:1 – 23! Wana wa Israeli wasingepata msaada wa Mungu, kama wangeiacha damu ya Kondoo aliyekuwa pasaka wao, kwenye bakuli bila kuitumia baada ya kumchinja!
Mungu aliwambia ya kuwa ataitumia ile damu katika kuwakomboa na kuwalinda, ikiwa tu wao wataitumia kuiweka kwenye miimo miwili ya milango, na kwenye kizingiti cha juu ya milango yao!
Kwa nini? Kwa sababu kwa kufanya vile walikuwa waonyesha aina za imani walizokuwa nazo juu ya "damu ya pasaka", kwa kukifanya kile walichoelekezwa wakifanye!
Ni muhimu ukaimarisha imani yako juu ya Damu ya Yesu – si tu kwenye uwezo uliomo ndani yake peke yake, lakini pia uweze kuwa na imani ya kuitumia!
Hii itakusaidia sana hasa wakati una gari, lakini huna dreva wa kukuendesha! Kwa sababu kama dreva hayupo na gari lipo – na unajua kuendesha – unaweza ukaendesha na ukasafiri!
Vivyo hivyo – ikiwa unajua kuitumia Damu ya Yesu kwa imani unaweza ukaitumia kwenye maombi yako mwenyewe kwa mafanikio, hata kama hakuna mtu wa kukuombea!
Tunakutakia pasaka njema – unapoendelea kutafakari habari za Damu ya Yesu – aliye “Pasaka wetu” (1 Wakorintho 5:7). Katika kukusaidia dhidi ya ndoto zinazokuletea mambo mabaya kwenye maisha yako!
Na Mungu aendelee kukubariki zaidi kwa kukusaidia imani yako iimarike katika kuitumia Damu ya Yesu!

[4/30, 8:40 AM] Principal Focus: Jina la Yesu litukuzwe milele na milele!
Tunaendelea tena na somo hili la: “Mambo unayohitaji kuyajua kuhusu ndoto unazoota ili iwe vyepesi kufanikiwa kimaisha”
Leo nataka nikujulishe kimafundisho juu ya jambo la 8 katika mfululizo wa somo hili ya kwamba “Usisahau kutumia Damu ya Yesu ili kuondoa sumu iliyoingia maishani mwako kwa kupitia kwenye ndoto”.
Yesu Kristo alipokuwa anashiriki “chakula cha Bwana na wanafunzi wake- siku ya pasaka -alisema: “Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi” (Mathayo 26:28)
Hii inatupa kujua ya kuwa, ikiwa damu ya Yesu ina uwezo wa “Kuondoa” dhambi: ina maana basi ya kuwa – ina uwezo pia wa kuondoa chochote kinachokuja kikiwa kimeambatana na dhambi!Kufuatana na Warumi 5:12, 17 – shetani alipata nafasi ya kuingia, na kuingiza vitu vyake – katika maisha ya mwanadamu, kupitia kwenye mlango wa dhambi, pale kwenye bustani ya Edeni.Ikiwa ni hivyo – inakuwa ni sahihi kabisa tukiamini ya kuwa, damu ya Yesu inaweza kutumika kuondoa dhambi, pamoja na chochote kile ambacho shetani anakiingiza katika maisha ya mwanadamu!
Tunapojifunza somo la leo – nataka tuangalie jinsi ambavyo unaweza kuitumia damu ya Yesu, kuondoa sumu yoyote ambayo shetani anaingiza kwenye maisha ya mtu, kwa njia ya ndoto.
Mtu mmoja aliniandikia akitaka nimwombee baada ya kuota ndoto ifuatayo: Aliota ameumwa na nyoka kidole cha pili cha mguu wake. Na alipoamka toka usingizini alikuta kidole kile alichoumwa na nyoka katika ndoto aliyoota, kilikuwa kinauma na kinatoa damu.Mtu yule alienda kanisani kwao kwa ajili ya maombi, na alipoombewa walikemea pepo la mauti toka ndani yake. Lakini, hata baada ya maombi yale, maisha yake na uchumi wake viliyumba sana, na kujikuta mara kwa mara, akifukuzwa toka kwenye nyumba alizokuwa anapanga kwa ajili ya kuishi.
Swali la msingi alilojiuliza, na ambalo lilimfanya ahitaji maombi zaidi, ni kutaka kujua ni kwa nini hata baada ya pepo la mauti kukemewa na kutolewa toka ndani yake, bado maisha yake yalikuwa magumu sana!
Nikikupa maelezo kwa kutumia mfano huu ufuatao utaelewa vizuri: Mtu akiumwa na mbu na akimwambukiza ugonjwa wa malaria, hatapata uponyaji kwa kumuua mbu aliyemuuma! Ni lazima pia “aondoe” mwilini mwake “vijidudu” vilivyowekwa na mbu yule kwenye damu yake, na pia “kuondoa” ugonjwa wa malaria alioupata kwa kutokana na vijidudu vile!
Nyoka aliyemuuma mtu yule kwenye ndoto aliyoota, aliacha “sumu” kwenye “maisha” yake! Alipoamka toka usingizini – yule nyoka hakuwepo – ila maumivu yalikuwepo, na damu ilikuwa inatoka kutoka kwenye kidole alichoumwa! Kwa hiyo – nyoka aliondoka – lakini “sumu” ilibaki ndani ya mtu yule! Na unaweza kuona ya kuwa sumu ile ilibeba “mauti” iliyofanya uchumi wake ufe: na ilibeba “hali ya kukataliwa”, iliyofanya awe anafukuzwa kwenye nyumba alizokuwa anapanga!
Bila kuondoa sumu ile ya nyoka na madhara yake kwenye maisha yake, hali mbaya ya uchumi wake isingeondoka; na hali ya kukataliwa isingeondoka!Nilipomwombea mtu huyu – nilitumia damu ya Yesu kuondoa “sumu” ya nyoka aliyemuua – na madhara yake kwenye uchumi wake, na madhara yake kwenye eneo la yeye kuishi.
Kumbuka: Kufuatana na Mathayo 26:28 – “damu ya agano” – yaani damu ya Yesu – ina uwezo wa “kuondoa” dhambi, na kile ambacho shetani anakileta katika maisha ya watu!
Mtu mwingine aliomba nimwombee baada ya kuota ndoto hii: Aliota ndoto ya kuwa kuna mtu anakata kwa kisu kidole gumba cha mguu wake wa kulia. Akaamka toka usingizini kwa mshtuko na akauombea mguu wake usiku ule ule – maana alipoamka alisikia maumivu makali toka kwenye kidole alichoota kuwa kinakatwa na kisu!
Mtu yule alishangaa sana kuona ya kwamba, baada ya miezi mitatu tangu aote ndoto ile, lile eneo la kidole kilichokuwa kinakatwa na kisu kwenye ndoto – pametokea alama nyeusi iliyokuwa inamwasha sana.Ni dhahiri ya kuwa aliombea kidole chake baada ya kuamka toka usingizini, lakini maombi yake hayakugusa “sumu” iliyoingizwa kwenye maisha yake kwa njia ya “kisu” kilichotumika kwenye ndoto aliyoota!
Mimi aliponishirikisha juu ya ndoto hiyo – nilimwombea kwa kutumia damu ya Yesu kuondoa ile “sumu” iliyosababisha kidole kiwe cheusi na kuwasha. Kumbuka: “pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo” (Waebrani 9:22). Lakini kufuatana na Mambo ya Walawi 8:23,24 – “kidole gumba cha kulia” kinasimama kama eneo linaloguswa wakati ulimwengu wa roho unapofuatilia hatua za mtu katika kumtumikia Mungu.
Ni dhahiri kwa kutumia ndoto ile, shetani alitaka “kukata” na “kuzuia” hatua za mtu yule katika kumtumikia Mungu. Nilimwombea pia jambo hilo kwa damu ya Yesu!Na maombi hayo niliyoomba kwa kutumia damu ya Yesu yalimsaidia kuponya kidole cha mtu yule; na kuponya, na kuutunza utumishi aliokuwa nao katika Kristo Yesu.
Unaposhughulika na ndoto za namna hii, ambazo zinaweka na kuacha “sumu” kwenye maisha yako, au ya mtu mwingine – kumbuka hatua zifuatazo:
1. Omba toba kwa ajili ya jambo lolote lililosababisha mtu aote ndoto ya jinsi hii;
2. Kemea pepo la shetani lolote litakalokuwa limeingia kwenye maisha ya mwota ndoto ile, ili liondoke kwenye maisha yake;
3. Weka mkono wako juu ya eneo lililopata madhara kwenye ndoto (kama vile – kidole), huku ukisema “Namwaga damu ya Yesu ya agano jipya kwenye eneo hili (huku ukilitaja hilo eneo), ili kuondoa sumu na madhara yake vilivyopitia hapo kwa njia ya ndoto aliyoota;
4. Ikiwa kumetokea “ugonjwa” au “madhara” ambayo uliyaondoa kwenye hatua ya 3 hapo juu, kumbuka kuomba “mbadala” wake ili utokee hapo. Kwa mfano ikiwa “sumu” ilileta ugonjwa – omba damu ya Yesu iweke uponyaji! Ikiwa “sumu” iliharibu uchumi – basi omba damu ya Yesu itengeneze uchumi ulioharibika!
Hii ni kwa sababu, kwa damu ya Yesu ya agano jipya, Biblia inasema;” aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili” (Waebrania 10:9)!
Mungu azidi kukubariki tunapoendelea kushiriki pamoja katika somo hili.

[5/1, 12:21 PM] Principal Focus: Jina la Yesu libarikiwe milele!
Namshukuru Mungu kwa kutupa nafasi hii tena, ya kujifunza juu ya jambo la 9, kati ya “Mambo unayohitaji kuyajua kuhusu ndoto unazoota ili iwe vyepesi kufanikiwa kimaisha”.
Jambo hilo la 9 ni hili: “Tumia Damu ya Yesu kulithibiti lango la muda ili lisitumiwe na ndoto kukwamisha maisha yako”.
Neno hili “muda” lilivyotumika kibiblia linahusisha maneno kama: saa, siku, wiki, mwezi, nyakati, zamu, na majira. Matumizi ya maneno hayo yanategemea ni “muda” upi, au ni muda wa aina ipi unaozungumzwa.
Ninachotaka ujifunze leo, ni kule kujua ya kuwa Damu ya Yesu inaweza kutumika kulithibiti lango la “muda”, ili lisitumiwe na ndoto kuvuruga maisha yako.
Mwanzo 40: 16 – 22 inatupa maelezo ya ndoto aliyoota mkuu wa waokaji wa Farao. Aliota ziko nyungo tatu za mikate myeupe juu ya kichwa chake. Na katika ungo wa juu, mlikuwa na kila namna ya chakula kwa Farao, kilichokuwa kimeandaliwa na mwokaji.
Ndege wakavila vile vyakula vilivyokuwa kwenye ungo, juu ya kichwa cha yule mkuu wa waokaji.
Yusufu alipokuwa anampa tafsiri ya ndoto ile alimwambia hivi: “Nyungo tatu ni siku tatu. Baada ya siku tatu Farao atakiinua na kukuondolea kichwa chako, na kukutundika juu ya mti, na ndege watakula nyama yako” (Mwanzo 40:18, 19). “Ikawa siku ya tatu …Farao…akamtundika mkuu wa waokaji, kama Yusufu” alivyomfasiria!
Swali ninalotaka tujiulize kwa pamoja, ni kama kifo cha mkuu wa waokaji kingeweza kuzuiliwa!
Ukisoma biblia katika “mapana” yake, au katika undani wake, utajua ya kuwa kifo cha mkuu wa waokaji kingeweza kuzuiliwa! Hii ni kwa sababu “lango” lililokuwa linatakiwa litumiwe ili kuyatimiza yaliyokuwa ndani ya ile ndoto, ni lango la muda!
Muda huo ulikuwa ni ule wa “siku tatu”, tangu usiku ule alioota ile ndoto. Kufuatana na ile ndoto, kifo chake kilipangwa kitokee “siku ya tatu”, kama adhabu kutoka kwa Farao! Ile adhabu haikupangwa itokee siku ya kwanza, wala siku ya pili, wala siku ya nne – bali itekelezwe “siku ya tatu”. Ndoto ile haikutoa sababu ya kwa nini adhabu ije “siku ya tatu”.
Kwa hiyo, ukiweza “kuzuia” hiyo ndoto isipate nafasi ya kutekelezwa katika siku hiyo ya tatu, basi, na mkuu wa waokaji atapona ili asichinjwe kichwa! Lakini ili apone ni sharti ushughulike na adhabu, na pia ushughulike na siku iliyopangwa kutekelezwa.
Nalipata jambo hili kwa kusoma habari iliyopo katika kitabu cha Kutoka 12:1 – 42.
Mungu alimpa taarifa Musa ya kuwa, kuna pigo alilopanga litokee nchini Misri, usiku wa siku ya 24 ya mwezi. Pigo hilo lilikuwa linalenga kuwapiga, na kuwaua wazaliwa wa kwanza wa wanadamu, na wazaliwa wa kwanza wa wanyama.
Kutoka 12:3 inasema “Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana Kondoo kwa hesabu ya nyumba ya baba zao…”
Na Kutoka 12:6 inasema: “Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule…”
Siku 10 ukijumlisha na siku 14 unapata siku 24. Kwa hiyo pigo lilipangwa litokee, au litekelezwe “tarehe” 24 ya mwezi huo! Lakini pia siku hiyo ya 24 ya mwezi huo – si siku yote ilikuwa inahusika, bali “muda” wake wa “usiku” ndiyo uliopangwa “pigo” lile litekelezwe!
Hili la muda wa “usiku” tunalipata tunaposoma mistari hii ya Kutoka 12:12,22. Na tunaona pigo hilo likitekelezwa juu ya nchi ya Misri “usiku wa manane” (Kutoka 12:29). Usiku wa manane kibiblia ina maana ya muda uliopo kati ya saa 6 usiku hadi saa 9 usiku!
Ninachotaka uone ni kwamba ile “damu” ya “Pasaka”, waliyoelekezwa wana wa Israeli kuiweka kwenye kizingiti cha juu, na kwenye miimo miwili ya milango yao, ilipewa “kufanya kazi” ya kuwalinda usiku ule tu wa siku hiyo ya 24 ya mwezi ule!
Ndiyo maana waliambiwa hivi: “na mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi” (Kutoka 12:22). Hii ikiwa na maana baada ya “asubuhi”inayotajwa hapa, kusingekuwa na tishio la lile pigo!
Kwa hiyo – Damu ya Pasaka ilitumika kuthibiti muda wa usiku, au “lango” la muda wa usiku, ili lisipitishe pigo, lililokuwa limekusudiwa kutokea usiku ule katika nchi yote ya Misri!
Kumbuka: “Usiku” ni muda unaoanza giza linapoingia, na unamalizika asubuhi au alfajiri wakati giza linapoondoka!
Ukisoma habari hii kwa “jicho” la agano jipya, utaona ya kuwa damu ya Yesu ina uwezo wa kufanya kazi kama hii, ya kuthibiti lango la muda, lisipitishe pigo lililokusudiwa kupitia hapo, ili kumpata mtu mhusika!
Kitabu cha 1 Wakorintho 5:7 kinasema: “Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo”. Hii inatupa kujua na kuamini ya kuwa, damu ya Yesu ina uwezo wa kufanya yale yaliyofanywa na damu ya Pasaka ya Kutoka 12:1 – 42.... Lakini katika hali ya ubora zaidi (Waebrania 8:6).
Hivi ndivyo ninavyowaombea wale ambao huwa wanahitaji maombi, juu ya ndoto zinazopitisha “mashambulizi” katika muda maalumu, na pia katika muda wanaoota ndoto ya kimashambulizi kwa kujirudia kwenye muda ule ule mara kwa mara!
Huwa ninaomba hivi:
1. Ninatubu kwa ajili ya mhusika, kwa chochote kilichosababisha “pigo” au mashambulizi ya kwenye ndoto yawe yanautumia muda fulani kwa kujirudia; Au kwa ajili ya muda maalum uliopangwa kutekeleza shambulizi hilo linalopitia kwenye ndoto, kama vile ilivyokuwa kwenye ndoto ya “mkuu wa waokaji” wa Farao. Toba hii inasaidia kupata pia msamaha toka kwa Mungu ikiwa “pigo” la kwenye ndoto ni taarifa ya adhabu toka kwa Mungu.
2. Ninaomba hivi: “Naweka damu ya Yesu aliye pasaka wetu juu ya muda huu (huku nikitaja muda unaotumiwa na shambulizi la kupitia kwenye ndoto), ili kuthibiti na kuzuia lango hilo la muda lisiruhusu shambulizi hilo kupita hapo, na kumfikia fulani (huku nikitaja jina la mhusika kama ndoto ilivyoonyesha).
3. Ninaomba damu ya Yesu hiyo inene mema kwa ajili ya mhusika kwenye muda husika (Waebrania 12:24), ili maneno hayo yawe badala ya mabaya yaliyokusudiwa kwa njia ya ndoto.
4. Ikiwa ndoto inatoa taarifa ya shambulizi toka kwa shetani: Nakemea kwa jina la Yesu na kwa damu ya Yesu, roho yo yote ya kipepo iliyotumwa kutekeleza shambulizi lile la kwenye ndoto – ili liondoke na kuacha kutekeleza shambulizi lile kwa mhusika
5. Na pia: Nakemea kwa jina la Yesu na kwa damu ya Yesu, roho yo yote ya kipepo iliyowekwa “kulinda” lango la muda uliolengwa na ndoto, ili liondoke, na badala yake malaika wa Mungu wahusike kulinda lango hilo la muda sawa na Kutoka 12:23.
Mungu aendelee kukutunza na kukupa uelewa mpana juu ya somo hili tunaloendelea kujifunza.

[5/19, 5:35 AM] Principal Focus: Bwana Yesu Asifiwe!
Leo nataka tuangalie sehemu ya 10 ya somo letu la ndoto, inayohusu;"uhusiano wa jina la Yesu na damu ya Yesu, ili uwe unapata ushindi juu ya mashambulizi ya shetani anayopitisha katika ndoto."
Hebu soma na kutafakari ndoto zifuatazo, halafu tuone tunajifunza nini ndani yake, juu ya mambo mawili hayo hapo juu.
Ndoto ya mtu wa 1: Mtu mmoja aliniandikia kuwa aliota yuko nyumbani kwao alikozaliwa. Na alipofika nyumbani kwao kwa wazazi wake, akatokea nyoka mbele akitaka kumuuma. Huyo mtu aliyeota ndoto hiyo, kwa kuwa alikuwa ameokoka, akamkemea yule nyoka mbele yake kwa jina la Yesu. Yule nyoka hakuondoka, badala yake akamrukia na kumuuma kwenye kidole cha mguu wake. Na alipoamka au alipozinduka toka usingizini, alikuta kile kidole alichoumwa na nyoka kwenye ndoto, kinauma na kutoa damu.
Ndoto za mtu wa 2: Mtu mwingine aliniandikia kuhusu ndoto zifuatazo alizoota: " Niliota kijana ameajiriwa kuniua na aliponiambia - nilikemea kwa jina la Yesu kwa nguvu zote - lakini alinizidi nguvu! Aliposogeza kisu ( kutaka kunichoma nacho), nikasema damu ya Yesu inenayo mema inishindie, aliniacha. Nikashtuka toka usingizini".
"Wiki iliyofuata nikatoka ndoto nyingine ya kuwa; niko msituni nimeshikwa na walinzi, halafu akaja mdada na kisu ili anichinje. Nikakumbuka kilichotokea kwenye ndoto ya wiki iliyopita, nikaita damu ya Yesu dhidi ya kile kisu, ghafla kikadondoka, na yule dada akaondoka hapo huku akikimbia. Nikashtuka toka usingizini".
Huyu mtu aliyeota ndoto hizo mbili kufuatana katika wiki mbili, alimalizia ujumbe huo alioniandikia kwa maneno yafuatayo:"Tangu kipindi hicho natafuta sana kujua juu ya damu ya Yesu. Asante kwa somo"
Ndani ya ndoto hizo za watu wawilu, tunajiuliza maswali ya msingi yafuatayo:
1. Kwa nini yule mtu wa kwanza alipotimia jina la Yesu kumkemea nyoka, hakuon ushindi, na badala yake akaumwa na yule nyoka?
2. Kwa nini yule mtu wa kwanza alishindwa kupata ushindi dhidi ya shetani, alipomshambulia kwenye ndoto, ingawa alikuwa ameokaka?
3. Kwa nini yule mtu wa pili aliona ushindi dhidi ya mashambulizi ya adui kwenye ndoto, kwa kutumia damu ya Yesu na si kwa kutumia jina la Yesu?
Je kuna uhusiano gani wa kimamlaka na wa kimatumizi, kati ya damu ya Yesu na jina la Yesu?
Kuna mambo ya msingi unayohitaji kuyafahamu, ikiwa unataka kupata majibu ya maswali hayo hapo juu.
Jina la Yesu ni jina lililofunuliwa na Mungu kwa wanadamu katika mazingira ya agano jipya. Hili tunalipata tunaposoma vitabu vya Waebrania 1:1 – 4, na Wafilipi 2:5 – 11, na Luka 1:30 – 35.
Kufuatana na maneno ya Waebrania 9:15 – 18, msingi na uhalali wa kutumika kwa agano jipya, ni kule kutumika kwa “damu” katika kuwepo kwake.
Na Yesu alipokuwa anashiriki chakula cha pasaka na wanafunzi wake kwa misingi ya agano alisema: “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu inayomwagika kwa ajili yenu” (Luka 22:20).
Kwa mantiki hii uhalali wa matumizi ya jina la Yesu, unategemea uhalali wa kimatumizi wa damu ya Yesu kwa mtumiaji wa jina la Yesu!
Ndiyo maana mahali ambapo damu ya Yesu inatakiwa itumike kwanza kabla ya kutumia jina la Yesu, utakuta jina la Yesu likitumika linakosa nguvu ya kimamlaka!
Ikitokea namna hii haina maana jina la Yesu halina nguvu – la hasha! Bali ina maana ya kuwa, mazingira ya kiroho ya jambo hilo, yanadai damu ya Yesu itumike kwanza kabla ya kutumia jina la Yesu! Kwa hiyo, ukiona kuna jambo unaloliombea kwa jina la Yesu, na huoni matokeo uliyotarajia – basi tumia damu ya Yesu, na utaona matokeo mazuri na ya ushindi.
Hili ndilo lililoweka tofauti ya kimatokeo katika matumizi ya jina la Yesu na damu ya Yesu kwenye ndoto nilizokushirikisha kwenye somo hili la leo.
Mazingira ya kiroho yanayodai matumizi ya jina la Yesu kwa msingi huu, ndiyo yaliyowafanya wana wa Skewa wasifanikiwe kutoa pepo kwa kutumia jina la Yesu.
Habari hii utaipata ukisoma Matendo ya Mitume 19:11 – 17. Jina la Yesu halikuwa na matokeo waliyoyataka, kwa sababu walikuwa hawajaitumia damu ya Yesu maishani mwao!
Kumbuka ya kuwa Damu ya Yesu ukiiamini na kuitumia kibiblia maishani mwako, inakupa uhalali wa kutumia jina la Yesu kwa mafanikio zaidi.
Ni vigumu kulitumia jina la Yesu kwa mafanikio, ikiwa kuna “lango” katika maisha yako ambalo shetani anatumia, au anaweza kulitumia kukushambulia.
Ni muhimu utumie damu ya Yesu KWANZA kuziba, au kulifunga hilo “lango” kwa damu ya Yesu, ndipo utaweza kuona matokeo mazuri hata utakapolitumia jina la Yesu!
Jambo jingine la kukumbuka kujiombea katika vita vinavyokujia kupitia kwenye ndoto – ni hili la kwamba Mungu akupe uwezo wa kushinda hivyo vita wakati unaota ndoto hiyo – ili kuondoa kwako madhara ya ndoto za vita vya kiroho katika maisha yako!
Nami nakuombea katika hilo wewe uliyesoma somo hili leo! Mungu azidi kukubariki sana!

Bwana Yesu asifiwe sana! …tena sana!
Hii ni sehemu ya 11 ya mfululizo wa somo la ndoto, ninaloendelea kukuletea mara kwa mara kwenye ukurasa huu.
Ndani ya sehemu ya 11 – nataka nikufundishe jambo la II unalohitaji juu ya ndoto – nalo ni hili: “Kiashiria Kilichomo katika ndoto kinavyosaidia unapoiombea ndoto”.Lengo kubwa la somo la leo, ni kukuhimiza ili umpe nafasi Roho Mtakatifu akusaidie kuiombea ndoto, kwa kutumia viashiria vinavyokuja na ndoto.
Neno ‘Kiashiria’ nimelitumia katika somo hili, kumaanisha juu ya “ishara” inayoambatana na ndoto, ili kukuarifu na kukujulisha kuwa usiipuuzie hiyo ndoto husika!Viashiria vinavyokuja na ndoto, huwa vinatofautiana na havifanani kati ya ndoto na ndoto, lakini kufuatana na kitabu cha Kutoka 4:8, ishara huwa zina ujumbe ndani yake.
Tukitazama baadhi ya ishara, au viashiria vinavyokuja na ndoto, utaona mifano ifuatayo:
• “Hasira” au “chuki” Soma Mwanzo 37:5,9 – 11.
• “Kufadhaika” au “mahangaiko moyoni”. Soma Mwanzo 40:5,6
• “Huzuni” au “kukunjamana uso” Soma Mwanzo 40:7
• “Hamu moyoni ya kutaka kujua tafsiri ya ndoto uliyoota” Soma Mwanzo 40:8
• “Hofu” au “Kuingiwa na woga” Soma Ayubu 4:12 – 14.
• “Uliloota kuwa kinyume na matarajio yako, au mipango yako, au makusudio yako” Soma Ayubu 33:14 – 18.
• “Uliloota kujitokeza katika mwili Soma Ayubu 4:12 – 14.
• “Uliloota kuwa kinyume na neno la Mungu”. Soma Kumbukumbu ya Torati 13:1 – 4.
Hivyo ni baadhi tu ya “viashiria” vinavyoweza kuja na ndoto – vikiwa na lengo la kukuarifu na kukujulisha kuwa usiipuuzie hiyo ndoto – husika.
Kumbuka “ndoto” ni njia mojawapo ya Kiroho inayotumika kukupa taarifa ya ujumbe unaokujulisha juu ya:
(i) Jibu la swali moyoni mwako au …
(ii) Jibu la maombi yako kwa Mungu; au ….
(iii) Kukujulisha yajayo; au …
(iv) Kukujulisha yaliyopita ambayo bado yanagusa maisha yako ya sasa na ya baadae; au …
(v) Kukujulisha yanayotokea katika ulimwengu wa Kiroho, au kimwili, wakati huo unapoota ndoto.
Ni vizuri pia ujue, ya kuwa – si lazima yale yote uliyoota katika ndoto yatokee kama ulivyoota kwa kuwa yanaweza kubadilishwa na maombi!Tena – si lazima yale yote uliyoota kwenye ndoto, na yakatokea kama ulivyoota – yaendelee kukudhuru (yaani ikiwa mabaya), maana unaweza kuyaondoa madhara yake kwa maombi!
Na ikiwa ndoto hiyo imebeba ujumbe wenye taarifa ya mambo ambayo huwezi kuyabadilisha, basi ina maana unahitaji kujiandaa ipasavyo juu ya “kutokea” kwake!
La msingi – ni wewe kujua “umuhimu” wa kuombea ndoto, zilizobeba kiashiria kinachokujulisha ya kuwa usiipuuzie hiyo ndoto!Kujua “umuhimu” wa kuombea ndoto za namna hiyo, kunatakiwa kuambatane na kujua namna ya kuziombea kwa mafanikio ndoto hizo!
Ndani ya somo la leo, nataka nikujulishe ya kuwa njia mojawapo, au aina majawapo ya kuombea ndoto, ni kule kuomba huku unafuatilia kwa karibu “kiashiria” kilichokuja na ndoto; na mabadiliko yanayotokea kwenye “kiashiria” hicho wakati unaendelea kuiombea ndoto husika.
Mfalme Nebukadreza aliwahi kuota ndoto, ambayo ingawa alisahau alichoota, lakini hata hivyo viashiria vilivyokuwa vimeambatana na ndoto ile havikumwachia!Ndoto hiyo inapatikana katika kitabu cha Danieli 2:1 – 12. Ndani ya ndoto hiyo tunaona viashiria vinne, vilivyokuwa vinaambatana na ndoto hiyo!Ingawa Mfalme Nebukadreza alisahau ndoto ile, baada ya kuamka toka usingizini (Danieli 2:5,6), lakini viashiria vilivyokuja na ile ndoto, havikumwachia mfalme asahau kuota kwa ile ndoto!
Kiashiria cha 1: Kilikuwa ni “roho yake kufadhaika” (Danieli 2:1). Kiashiria cha 2: Kilikuwa ni “usingizi wake kumwacha” (Danieli 2:1). Kiashiria cha 3: Kilikuwa ni kuwa na hamu ya kujua tafsiri ya ndoto ile – ingawa alikuwa haikumbuki” (Danieli 2:3). Kiashiria cha 4: Kilikuwa ni “ghadhabu kubwa na hasira nyingi (Danieli 2:5, 12 – 15).
Kumbuka ya kuwa kazi ya viashiria vinavyokuja pamoja na ndoto, ni kumkumbusha na kumtaarifu aliyeota ndoto ya kwamba asiipuuzie ile ndoto, bali anahitaji kuifuatilia!
Fahamu hili pia – ya kuwa – ishara inapokuwa “nzito”, au imejitokeza kwa “nguvu” au ikiwa zimejitokeza ishara zaidi ya moja kwenye ndoto moja, ujue ina maana – ndoto hiyo ni (i) ya muhimu kwako na (ii) unatakiwa ufuatilie kwa haraka na (iii) ina vitu zaidi ya kimoja ndani yake unavyohitaji kuvifuatilia!
Jambo lingine ninalotaka ulione hapa ni kwamba, kile kiashiria cha 4 kilipojitokeza na kumfikia Danieli – ndipo msukumo wa “kuiombea ile ndoto ulipojitokeza ndani yake”!
Kwa hiyo, ni vizuri ujue ya kuwa, kazi mojawapo ya kiashiria kinachokuja na ndoto, ni kule kuusukuma moyo wa mtu, ili umkaribie Mungu katika maombi, au kwa njia ya maombi!Jinsi kiashiria kilichoambatana na ndoto ya Nebukadreza, kilivyomsaidia Danieli kuiombea ndoto hiyo, vivyo hivyo ndivyo unavyoweza kusaidika na wewe katika kuiombea ndoto yako, au ndoto ya mtu mwingine!
Kiashiria kile kilimsaidia Danieli kuiombea ndoto ya mfalme Nebukadreza kwenye maeneo yafuatayo:
1: Kiashiria kiliweka moyoni mwa Danieli msukumo wa “kutambua” ya kuwa, maombi yanayohitajika ili ndoto aliyoota mfalme Nebukadreza na kuisahau, ifahamike na aikumbuke, na tafsiri yake ijulikane! Soma Danieli 2:12 – 16 Kwa hiyo – hata kwako – kiashiria kinachokuja na ndoto, kinakupa kutambua umuhimu wa kuiombea ndoto, ili uikumbuke kama umeisahau, au ujue tafsiri yake sahihi, na upokee ujumbe unaokuja ndani yake.
2: Kiashiria kile kilimsukuma Danieli kujua ya kuwa, ndoto inahitaji utengewe “muda” wa kutosha, ili uweze kuiombea ipasavyo!
Msukumo huu ulimfanya Danieli kwenda kwa Nebukadreza kuomba apewe “muda”, ili apate nafasi ya kumwomba Mungu wake juu ya hilo! Soma Danieli 2:16.Kwa hiyo – hata wewe – jizoeze kutenga “muda”, utakaokuwezesha kuombea ipasavyo, ndoto iliyokuletea kiashiria hicho – iwe ni ndoto yako, au iwe ni ndoto ya mtu mwingine!
3: Kiashiria kile kilimpa kujua kuwa, alihitaji “msaada” wa maombi, toka kwa wenzake aliowaamini! Soma Danieli 2:17,18.Si kila ndoto utahitaji msaada kama huo. Ndoto zingine kiashiria kitakuwekea moyoni mwako, msukumo wa kuiombea hiyo ndoto wewe mwenyewe – na kujikuta unasita kuwashirikisha watu wengine!
4: Kiashiria kilimjulisha Danieli, kupitia moyoni mwake ya kuwa, Mungu amesikia maombi yake – baada ya kuona utisho wa hasira umeondoka moyoni mwake, alipooteshwa ndoto na Mungu – kama ile aliyoota mfalme Nebukadreza!Na alipomjulisha mfalme Nebukadreza ndoto ile , “hasira” ya Nebukadreza juu ya wenye hekima ikaondoka! Soma Danieli 2:17 – 19,24. Kwa hiyo – jizoeze kuangalia kiashiria kama bado kipo moyoni mwako, au kimeondoka kila unapoendelea kuiombea ndoto!
5: Kiashiria kile kilimsukuma Danieli, kuomba maombi ya shukrani, mara tu baada ya kujua moyoni mwake, ya kuwa Mungu amejibu maombi yao, kuhusu ile ndoto ya mfalme Nebukadreza! Soma Danieli 2:19 – 23.Kwa hiyo – na wewe usisahau kumshukuru Mungu pindi ujuapo ya kuwa, Mungu amekujibu juu ya ndoto uliyokuwa unaiombea!
Mungu aendelee kukupa maarifa, tunapoendelea kujifunza pamoja somo hili linalohusu ndoto!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom