Mwenyekiti wa NEC amepiga marufuku jitihada za CHADEMA kuhamasisha watu kujiandikisha kupiga kura huko Singida.
CHADEMA walikuwa wanatumia vipeperushi na matangazo ya magari kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi.
Kauli hii ya Mwenyekiti wa NEC inanishangaza kwani kila chama kina haki ya kuhamasisha wafuasi wake kujiandikisha na hiyo ndio kazi ya siasa.
Hii inatupelekea tuhisi Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina agenda ya siri maana katika hali ya kawaida Tume ingefurahi kwa vyama kufanya kazi ya uhamasishaji.
nanukuu maelezo ya Mwenyekiti wa tume DAMIAN LUBUVA aliyoandika katika kitabu alichowaandikia vyama vya siasasa kitabu hicho kinaitwa MAELEKEZO KWA VYAMA VYA SIASA.
UJUMBE WA MWENYEKITI.
"katika uboreahaji wa daftari la kudumu la wapiga kura,ushirikiano mkubwa unahitajika kati ya tume ya taifa ya uchaguzi ,vyama vya siasa na wadau wengine.Vile vile ,ili utekelezaji wa zoezi hili uwe na mafanikio mazuri , ni muhimu kuwepo elimu kwa umma na uhamasishahi wa kutosha juu ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, aidha utaratibu wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura hauna budi ueleweke vizuri"
hapa tena akaendelea kuandika
"maelekezo yaliyomo katika kijitabu hiki yameandaliwa ili kuvisaidia vyama vya siasa viweze kushiriki katika kuelimisha na kuhamasisha wananchi juu ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura"
hapa akaendelea kuandika
"napenda kutoa wito kwa viongozi wa vyama vya siasa kutumia fursa hii kujielimisha juu ya dhana ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ,utaratibu na hatua zitakazotumika katika zoezi hili"
MAELEZO HAYO YOTE JUU YANAPATIKANA KATIKA UKURASA WA (iii).
katika ukurasa wa 1. kuna maelezo mengine kuhusu swala la uhamasishaji.
nanakiri maelezo hayo.
"vyama vya siasa vina wajibu mkubwa wa kuwaelekeza na kuwaelimisha wanachama wao na wananchi kwa ujumla umuhimu wa kuwemo katika daftari la kudumu la wapigakura ,na utaratibu utakaotumika katika uboreshaji wa daftari hilo.Hivyo ni muhimu kwa vyama vya siasa kuhamasisha na kuelimisha wanachama wao pamoja na wananchi kwa ujumla ili waweze kufahamu na kuelewa uboreshaji wa daftari hilo, haki na wajibu wao"
KABLA NA WAKATI WA UBORESHAJI
"kwa kuwa uboreshaji utafanyika katika kipindi cha siku kumi na nne(14) tu, ipo haja kwa vyama vya siasa kabla na wakati wa kipindi hicho , kuwahimiza wananchi wajitokeze kujiandikisha wakati wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura"
WAKATI WA UKAGUZI WA DAFTARI
"ni wajibu wa vyama vya siasa kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kukagua daftari la awali la wapiga kura mara litakapowekwa wazi kwa ukaguzi.
daftari la awali la wapiga kura litakuwa kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura kwa muda usiozidi siku saba.kwa hiyo kuna umuhimu mkubwa wananchi kuhamasishwa kujitokeza bila kuchelewa kukagua daftari hilo.
wananchi pia waelimishwe kuhusu utaratibu mzima wa kuweka pingamizi kama watakuwa na sababu za msingi. vile vile waelimishwe kuwa wana haki ya kukata rufaa kwenye mahakama ya wilaya ,iwapo hawakuridhika na uamuzi uliotolewa kuhusu pingamizi walilowekewa au waliloweka"
baada ya nukuu zote hizo hapo juu ambazo zimetokana na MAELEZO YA TUME YA UCHAGUZI CHINI YA JAJI MASTAAFU DAMIAN LUBUVA.
nitoe masikitiko yangu makubwa kama hili limetokea na kuamrisha CHADEMA ISITISHE UHAMASISHAJI KATIKA HILO ULILOTAJA.
kwa kuwa maelekezo hayo yanaenda kinyume na ujumbe wa jaji huyuhuyu alioutoa kwa vyama vya siasa.
lakini kibaya zaidi yanakiuka taratibu za kanuni na sheria ya uchaguzi.
hivyo vyama vya siasa visitishwe na kauli hiyo ya Lubuva kuzuia uhamasishaji. na badala yake viendelee kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi ili wasipoteze haki yao.
na kwa kuwa hakuna utaratibu uliotolewa ni kwa namna gani uhamasishaji ufanyike. itakuwa si kosa kwa vyama kuandaa na kuchapisha vipeperushi vya kuelimisha na kuhamisha, pia si kosa kutoa matangazo kwa spika, mikutano na hata matangazo kwa njia ya radio na television.
NA:
KATIBU MWENEZI CHADEMA KATA YA MSIGANI(jimbo la ubungo).
Joseph Mshinga.