Mambo haya yataua ndoto za serikali ya awamu ya tano

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Serikali ya JPM inaweza kushindwa kufikia malengo ya ukuaji uchumi!

Sababu kubwa ni mbinu zake za kufufua uchumi ambazo zinabinya mzunguko wa fedha na hivyo kufuta kabisa ubunifu na uthubutu kwa wafanyabiashara nchini na wajasiliamali wengine!

Lakini kukosekana kwa motisha kwa watumishi wa umma pia ni kikwazo kikubwa sana ktk kukuza uchumi!

Trend zinaonesha kuwa pamoja na kufanya kazi kwa woga, hali ya uzalishaji au kujituma kwa watumishi wa umma imeshuka, pamoja na ile morali ya kazi!

Wengi wanachofanya ni kujitetea kwa kufika kazini na kuwepo maeneo ya kazi lkn hawaingii ktk kuwekeza nguvu zao kwenye uzalishaji.

Hili linaonekana hata kwa watendaji wa juu wa mikoa na mawaziri, ambapo wengi wanacheza michezo salama Zaidi kuliko kuwa wabunifu.
 
Kama hauna motisha acha kazi, nani amekulazimisha??

Wakulima na wafugaji siku zote wanapewa motisha na nani??

Tumechoka na vitabia vyenu vya kulialia kila siku.
 
Kama hauna motisha acha kazi, nani amekulazimisha??

Wakulima na wafugaji siku zote wanapewa motisha na nani??

Tumechoka na vitabia vyenu vya kulialia kila siku.
Una akili sana wewe. Wakulima na watumishi wa umma wote wanafanya kazi kwa utaratibu mmoja, chini ya sheria zile zile na mikataba ile ile na mwajiri wao.
 
bandiko lako li mapungufu makubwa. sehemu kubwa ya waajiriwa wa umma wapo kwenye ttowaji huduma. tofautisha na uzalishaji, ambao upo viwandani, shambani na migodini.
 
Mmemrukia Bure mtoa mada, mngejipa muda wa kutafakari alichoandika mngeelewa kitu.

Kwahiyo kufanya kazi za kutoa huduma hutakiwi kuwa mbunifu na kupewa motisha.
 
Serikali ya JPM inaweza kushindwa kufikia malengo ya ukuaji uchumi!
sababu kubwa ni mbinu zake za kufufua uchumi ambazo zinabinya mzunguko wa fedha na hivyo kufuta kabisa ubunifu na uthubutu kwa wafanyabiashara nchini na wajasiliamali wengine!
lakini kukosekana kwa motisha kwa watumishi wa umma pia ni kikwazo kikubwa sana ktk kukuza uchumi! trend zinaonesha kuwa pamoja na kufanya kazi kwa woga, hali ya uzalishaji au kujituma kwa watumishi wa umma imeshuka, pamoja na ile morali ya kazi! wengi wanachofanya ni kujitetea kwa kufika kazini na kuwepo maeneo ya kazi lkn hawaingii ktk kuwekeza nguvu zao kwenye uzalishaji. hili linaonekana hata kwa watendaji wa juu wa mikoa na mawaziri, ambapo wengi wanacheza michezo salama Zaidi kuliko kuwa wabunifu.

Ni vigumu kuainisha bayana ufanisi wa Serikali ya Magufuli kwa sababu kuu mbili:

Kwanza kwa kuwa bado tuna tunategemea mambo yalioanzishwa katika awamu iliyopita. Miradi mingi ukiacha Bombadier kiini chake ni utawala wa JK mfano flyovers, madaraja, barabara, bandari, reli, mifumo ya maji safi, uzalishaji umeme nk. Nakiri uwepo wa viashiria kadhaa vya mabadiliko kwenye makusanyo na uanzishaji wa miradi mipya.. Hata hivyo bado ni mapema kusema kama awamu hii imevuta wawekezaji, watalii, imeboresha huduma nk nk

Pili utamaduni wa kutokuwepo uwazi katika utendaji wa serikali. Hadi sasa hakuna ongezeko lolote la utoaji taarifa na uwazi juu ya huduma za serikali na hakuna mfumo wa kupokea kero na maoni ya wanachi walau katika ngazi ya taasisi. Pengine kanzu data ya Mh. Lukuvi kwenye sekta ya ardhi inaweza kuwa chachu kwa wizara nyingine..

Nashauri tuanze kujenga mfumo wa kupima pia efficiency ya serikali na idara zake, sio tu output. Tufike mahali tujue kipindi hichi inagharimu kiasi gani na muda gani kupata huduma fulani kama kuunganishiwa umeme, maji, kupata hati ya kiwanja, kutoa kontena bandarini, kusajili biashara nk. Tuangalie uwiano na kabla, na nchi zingine na pia tulinganishe na muda/gharama zilizowekwa kisheria na kwa namna ya uwazi.
 
Kama hauna motisha acha kazi, nani amekulazimisha??

Wakulima na wafugaji siku zote wanapewa motisha na nani??

Tumechoka na vitabia vyenu vya kulialia kila siku.
Hizi ndizo akili za makada zinazowapotosha viongozi wenu!
Motisha ni kitu cha msingi ili jambo lolote liweze kutendeka!
kwa akili zako za kijani unadhani motisha ni mpaka upewe pesa / materials za aina yeyote.
Ngoja nikupe mfano mdogo wa motisha!
  • Kama umewahi kuingia darasani, mkuu wa shule anaweza kuwaambia wanafunzi, jamani msituangushe ktk mitihani ya taifa, ufaulu wenu unatuletea heshima sote. maana hii shule ni yetu sote na bila ya nyinyi sisi hatuwezi kuwa na sifa zozote. hii ni kauli yenye motisha, kwanza hapa mtu amepata umiliki wa shule, anayotenda anajua yatawaletea heshima yeye binafsi, walimu wake na shule yake
  • motisha siku zote zimewafanya watoto wadogo waweze kutambaa, kutembea na kukimbia, kuongea etc! just kumu-encourage mtu kunajenga uwezo wa ziada ktk performance yake na this is worldwide.
  • wapo watu wanakuwa motivated na materials, lkn I bet motisha ya cash huwa haizidi motisha ya kauli njema!
kwa maana hiyo hiyo, wakulima waliheshimika na walipewa motisha sana miaka yote. neno kama kilimo kwanza, upatikanaji wa power tila, stakabadhi gharani na upatikanaji wa mbolea na pembejeo nyingine ni sehemu ya motisha ambayo wakulima wali-enjoy!

kwa sasa, watu wanaambiwa watakaokuwa na njaa hawatosaidiwa.
watu wavivu etc.
kazini, mabwege kama nyinyi msio na kazi kutwa kufanya majungu juu ya walimu, madaktari na wauguzi, au maafisa ardhi ambao kutwa wanatishiwa, wanadharirishwa hadharani etc wengi kwa vijimishahara ambavyo havikutani tarehe 30 - 30.
 
Mwanzo mgumu jamani. Tujipe moyo tutashinda
Watumishi wa umma ni sehemu muhimu sana ktk taifa!
lazima wawe sehemu ya serikali.
kwa sasa kuna gap kubwa kati ya watumishi na viongozi wa juu wa serikali!
sio salama kwa uchumi na maendeleo ya taifa!
watu wanahitaji kuwa sehemu ya maendeleo ya taifa lao!
lkn unaweza kukuta shule haina walimu wa kutosha, lkn walimu wanalaumiwa kwa ufaulu mbovu!
Muuguzi anatakiwa azalishe tu hata kama hospitali haina gloves, na haruhusiwi kumwambia mama akanunue gloves mwenyewe maana atasemewa na kudhalilishwa barabarani, lkn hakuna anayetazama side ya nurse
 
Una akili sana wewe. Wakulima na watumishi wa umma wote wanafanya kazi kwa utaratibu mmoja, chini ya sheria zile zile na mikataba ile ile na mwajiri wao.
sio kweli!
Tanzania wakulima karibu wote sio waajiriwa wa serikali!
sehemu ndogo sana wameajiriwa ktk sekta binafsi au mashamba waliyoingia ubia ambapo hali ni mbaya kuliko watumishi wengine!
 
bandiko lako li mapungufu makubwa. sehemu kubwa ya waajiriwa wa umma wapo kwenye ttowaji huduma. tofautisha na uzalishaji, ambao upo viwandani, shambani na migodini.
Tunapolizungumzia taifa ktk ukuaji wa uchumi kila sekta ni muhimu!
taifa ni kama mwili wa binadamu!
raisi na team yake ndio roho, lkn roho iliyohai ktk mwili uliomahututi huwa haina maana yeyote!
lkn kama alivyo mtu, hata ukiumwa kidole unaweza usiende kazini kabisa, ingawa kidole ni sehemu ndogo sana ktk mwili wako!
wakulima, watu wa migodini na viwandani wanahitaji askari kwa ulinzi, lkn watahitaji gereza kwa waharifu ambao watahitaji mahakama pia ili ulinzi uwe imara na wenye kuzingatia haki! kila mmoja wao atahitaji watu wa Bank kwa ajili ya transactions za kila siku, lkn wote wakiumwa watahitaji wataalam wa afya, pia watoto wao watahitaji kusoma! chaos ktk any system ita-upset uchumi tu!
labda unahitaji kufikiri tena!
 
Mmemrukia Bure mtoa mada, mngejipa muda wa kutafakari alichoandika mngeelewa kitu.

Kwahiyo kufanya kazi za kutoa huduma hutakiwi kuwa mbunifu na kupewa motisha.
kuna watu wana matatizo!
wanafikiri mimi nalaumu kama vile ni mpinzani wa CCM!
Mimi nazungumzia concerns zangu kama raia wa Tanzania! mimi nina haki ya kujadili vitu kwa faida ya nchi yangu, binafsi sijaibinafsisha nchi yangu kwa CCM, na wala sitowasusia kina JPM au kufikiri wao ni bora Zaidi kuliko mimi la hasha!
wao nitawaheshimu kama watu waliopewa dhamana na watanzania wote kutuongoza kwa miaka 5 lkn I cant still speak my minds au naweza pia kushauri hata kama itakuwa ni kujifariji mwenyewe lkn I know nimezungumza somewhere vile ninavyohisi napaswa kutendewa kama mwananchi wa taifa hili pekee Mungu alilioona linanifaa kuwa mkazi wake wa kudumu!
 
Hivi Kama Kazi Unayofanya Unaona Haikulipi, Kwanini Usiache Kazi Utafuta Kazi Inayolipa ?
 
Ni rahisi namna hii Mkaruka?
Mkuu Inachosha Kusikia Malalamiko, Mara Mshahara Hautoshi, Mara Hakuna Ongezeko La Mshahara. Sasa Kama Kazi Unayofanya Unaona Malipo Kiduchu, Suluhisho Ni Kuacha Kazi Na Kutafuta Kazi Ambayo Inalipa. Period
 
Mkuu Inachosha Kusikia Malalamiko, Mara Mshahara Hautoshi, Mara Hakuna Ongezeko La Mshahara. Sasa Kama Kazi Unayofanya Unaona Malipo Kiduchu, Suluhisho Ni Kuacha Kazi Na Kutafuta Kazi Ambayo Inalipa. Period
Haya mkuu
 
sio kweli!
Tanzania wakulima karibu wote sio waajiriwa wa serikali!
sehemu ndogo sana wameajiriwa ktk sekta binafsi au mashamba waliyoingia ubia ambapo hali ni mbaya kuliko watumishi wengine!
Hahahahaha. Nilimpa kejeli mkuu. Pole kwa kukupoteza. Pamoja sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom