๐— ๐—ฎ๐—บ๐—ฏ๐—ผ ๐Ÿฑ ๐˜†๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐˜ƒ๐˜‚๐˜๐—ถ๐—ฎ ๐—ธ๐˜„๐—ฒ๐—ป๐˜†๐—ฒ ๐˜€๐—ถ๐—บ๐˜‚ ๐˜†๐—ฎ ๐—œ๐—ป๐—ณ๐—ถ๐—ป๐—ถ๐˜… ๐—ก๐—ผ๐˜๐—ฒ ๐Ÿฑ๐Ÿฌ ๐—ฆ๐—ฒ๐—ฟ๐—ถ๐—ฒ๐˜€'

๐— ๐—ฎ๐—บ๐—ฏ๐—ผ ๐Ÿฑ ๐˜†๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐˜ƒ๐˜‚๐˜๐—ถ๐—ฎ ๐—ธ๐˜„๐—ฒ๐—ป๐˜†๐—ฒ ๐˜€๐—ถ๐—บ๐˜‚ ๐˜†๐—ฎ ๐—œ๐—ป๐—ณ๐—ถ๐—ป๐—ถ๐˜… ๐—ก๐—ผ๐˜๐—ฒ ๐Ÿฑ๐Ÿฌ ๐—ฆ๐—ฒ๐—ฟ๐—ถ๐—ฒ๐˜€'

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,221
Reaction score
2,425
1_20250623_194507_0000.png


Baada ya Infinix kutangaza toleo jipya la simu zao ambayo ni Infinix Note 50 Series' , kwa kweli wameboresha mambo mengi sana kwenye hii toleo jipya kikubwa zaidi ni kuhusu ujio mpya wa AKILI bandia inayokusaidia kufanya mambo Mbalimbali kwa haraka na urahisi.

๐Ÿ’ก Kioo chake ni chembamba
Hii simu imekuja ikiwa na AMOLED flat display yenye inchi 6.7 ikiwa na muundo wa STB skrini to body ni nyembamba wallah , inapendeza machoni mwa watu ukishika una enjoy pamoja na kutumia refresh rate yake ni 144Hz iko very smoothly.

3_20250623_194507_0002.png
4_20250623_194507_0003.png


๐Ÿ”‹ Battery ni Super
Battery lake ni 5200mah ndani ya dakika 30 utaweza kuchaji simu yako na kujaa faster ikiwa na 90W + fast charger 3.0 support. Pia unaweza chaji simu yako kwa mfumo wa wireless kwa kukuletea Mag Pad Wireless charging pad yenye 20W.

6_20250623_194507_0005.png
5_20250623_194507_0004.png


๐Ÿ“ธ Camera
Hii simu kamera yake ni nzuri mnoo asikuambie mtu aiseeh, inatoa picha nzuri za kuvutia unaweza sema umetumia kamera mbugani. Ina 50mp ikiwa na sensor ya Samsung ya ISOCELL GN 5 inayotoa picha Kali balaa.

Nakuambia tena picha zake ni Kali balaaa๐Ÿ“ธ.

8_20250623_194507_0007.png
9_20250623_194507_0008.png
11_20250623_194507_0010.png


๐Ÿ’ก Infinix Ai
Kwa kweli kwenye Ai siwezi kuwadai Chochote kwa hapa wametisha kwanza Wana Ai Eraser yenye uwezo wa kuondoa kitu usichotaka kwenye picha yako bila kuharibu uhalisia wa picha tofauti na AKILI bandia ya Apple kwenye iphone.



Utaweza ku double tap kwenye batani ya pendeni utaweza kumuwasha AI anaitwa Folax akiwa na muingiliano na Deepseek Chochote unachomuuliza basi anakusaidia chap bila shida yoyote.




โšก Processor yake
Imekuja ikiwa na Processor yenye nguvu MediaTek Helio G100 ultimate yenye uwezo wa kucheza game yoyote bila kuganda Ganda, kuanzia call of duty, Bright memory infinity yani simu kupata Joto sahau, Wala kuisha chaji unatumia bila wasiwasi.

15_20250623_194507_0013.png
14_20250623_194507_0012.png
 

Attachments

  • 10_20250623_194507_0009.png
    10_20250623_194507_0009.png
    1.1 MB · Views: 23
  • 13_20250623_194507_0011.png
    13_20250623_194507_0011.png
    1.3 MB · Views: 23
Sawa.

Samsung A3 core nadhani imeanguka kamamara Mia na hii NI kwasababu Mimi NI mlevi na bado iko vzr.


Je hiyo ikianguka chini damage yake inaweza kuwa kubwa Sana au nayo NI robot
 
Tunatoka mbali sana, enzi hizo hakuna utitiri wa simu kama sasa.
Kuna blaza alikuaga na Tecno M6, aisee nilikua namuona mwamba sana, simu kali, kioo kikubwa, camera kali, kitu HD.

Kadri siku zinavyozidi kwenda AI feature inazidi kuboreshwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom