Mambo 14 ambayo unapaswa kuyafahamu kuhusu hizi smartphones

mugumu11

Senior Member
Jun 22, 2016
113
56
Utakubaliana na mimi kwamba kila siku tunatumia simu , simu zimekuwa kama sehemu ya maisha yetu ya kila siku ambapo zimebadilisha kila namna katika biashara na shughuri zetu kiujumla

Ukitafakari kwa makini utagundua kuwa hizi kompyuta katika mifuko yetu zina guvu zaid kuliko hata zile ziwapelekazo watu mwezini...rockets

mambo 15 ambayo kwa namna moja ama nyingine haukuweza kuyafahamu kuhusu hiyo smart phone katika kiganja chako.



ukweli ni kwamba....

1 99% ya virusi vya simu (malware) hutengenezwa kwaajili ya simu zinazotumia mfumo wa android


2 47% ya watumiaji wa simu za mkononi huko marekani wanadai hawawezi kuishi bila ya simu zao

3 Viwanda ya simu za mkononi ni moja ya viwanda vinavyo kua kwa kasi kubwa hapa duniani




4. 70% ya simu za mkononi zinatengenezwa china

5 Kwa kawaida smart phones zina idadi ya bacteria ambayo ni mara 18 zaid ya vifaa vya chooni/ vyooni

6 Wanasayansi wamegundua namna ya kuchaji simu kwa kutumia mkojo (Bristol Robotics Laboratory)

7 Watumiaji wengi wa internet huko china hawana computer binafsi (PC) isipokuwa hutumia smart phones

8 Simu ya kwanza iliuzwa huko marekani kwa gharama ya dola 4000 za kimarekani

9 Mwaka 2012, kampuni ya Apple iliweza kuuza iphones 340,000 iPhones karibia kila siku.

10 Martin Cooper, Mgunduzi wa kwanza wa motorola alitengeneza simu ya kwanza mnamo mwaka 1973

11 Nokia wameuza simu zaidi ya milioni 250000 , hii imewafanya wavunje rekodi ya mauzo ya vifaa vya umeme katika historia

12 Hakuna ushahidi kwamba mionzi inayotokana na simu za mkononi ni hatari

13 Idadi ya watu wenye smart phones ni kubwa kuliko wenye vyoo hapa duniani

14 65% ya watumiaji wa smart phones hawadownlod application zozote .

Imeandaliwa na jm classic
 
Back
Top Bottom