MAMBO 12 ya NGUVU kuihusu Tanzania

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
7,121
10,231
NAAM,!NI KUMI NA MATATU

JAMBO LA KWANZA

Tanzania ni miongoni mwa nchi chache sana duniani zenye mti uitwao MPINGO (African Blackwood tree)ambao unashika rekodi kuwa mti mgumu sana na wenye thamani kubwa duniani.


JAMBO LA PILI

Fuvu la kale kuliko, la binadamu, lilivumbuliwa Tanzania katika Bonde la Olduvai Kaskazini mwa Tanzania.

JAMBO LA TATU

Ikiwa na zaidi ya wanyamapori Milioni 4 katika hifadhi zake,Tanzania ina mlundikano mkubwa kuliko ufananisho wowote wa wanyamapori kwa kilomita za mraba duniani.


JAMBO LA NNE

Na unapozungumzia nyika za hifadhi,30% ya eneo lote la Tanzania linachukuliwa na Hifadhi mbalimbali,12 hifadhi za taifa,13 maeneo tengefu,na 38 maeneo yaliyohifadhiwa.


JAMBO LA TANO

Mlima mrefu huria duniani,Ml.Kilimanjaro unapatikana Tanzania.Huu ndio mlima mrefu zaidi Afrika pia.


JAMBO LA SITA

Mataifa hushirikiana chakula,flora na fauna, na mengineyo.Ila kwa Tanzania ala ya wimbo wa Taifa inafanana sana na ile ya Afrika Kusini na Zimbabwe.


JAMBO LA SABA

Katika kisiwa cha Zanzibar kilichopo nchini humo ndilo eneo pekee unaweza kukutana Kaa mkubwa sana coconut crab (na ni mtamu balaa) na Hoteli iliyopo ndani ya maji.


JAMBO LA NANE

Hifadhi ya The Ruaha National Park ni nyumbani kwa idadi kubwa mno ya ndovu kuzidi hifadhi yoyote ya Afrika Mashariki.


JAMBO LA TISA

Tanzania ndiyo nchi pekee Afrika Mashariki yenye kiwango cha chini cha ubaguzi kwa wageni ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika.

JAMBO LA KUMI

Tanzania inayo kreta ya volkano kubwa kuliko zote duniani,Ngorongoro,yenye ukubwa wa kilomita 19 na kina cha Mita 600.


JAMBO LA KUMI NA MOJA
Tangu ijipatie uhuru kutoka mkoloni Mwingereza nchi ya Tanzania imeongozwa na maraisi watano na chama kimoja cha siasa CCM tangu wakati huo.Nchi hiyo inafuata mfumo wa vyama vingi.

JAMBO LA KUMI NA MBILI

Tanzania inabeba heshima ya Afrika kutokana na jitihada zake za ukombozi wa Afrika kutoka ukoloni,huku Mratibu wa kuanzishwa kwa Taifa hilo hayati Mwalimu JK Nyerere akibeba sifa kubwa duniani kama ilivyo kwa Mandela,Nkurumah,nk


LA KUMI NA TATU

Je, uliwahi kukutana na Simba anaepanda mti?labda kwenye runinga,sasa mubashara Simba hao wapo Manyara pekee,huwapati popote duniani.

ONGEZA JINGINE LA NGUVU KUIHUSU NCHI YETU YA NGUVU.WAKENYA MSIKOMENTI
 
Back
Top Bottom