MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,996
Lowassa aliingia CHADEMA kwa usanii wa kuja na wabunge 50 wa CCM, wenyeviti wa mikoa wa CCM zaidi ya 22, Wenyeviti wa wilaya zaidi ya 80 na wakuu wa wilaya zaidi ya 80 lakini kilichoshangaza baada ya kuondoka CCM, alifuatana na genge la wachumia tumbo wachache wasiozidi kumi ambao wengine wameanza kurudi CCM. Hii ilikuwa ni ishara halisia kuwa Lowassa ni msanii.
Mama Wema na yeye ameingia CHADEMA kwa kutumia gia kama ya Lowassa ambapo wakati akiongea na vyombo vya habari alisema ana watu zaidi ya 5,000 nyuma yake huku familia yake yenye watu zaidi ya 70 wamemwambia wanajiandaa kuingia CHADEMA.
Tunaelewa Lowassa aliingia na gia hii ili aweze kupewa nafasi ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA.
Swali la kujiuliza, Mama Wema ameingia na gia kama ya Lowassa ili yeye na mwanae wapate nini CHADEMA? Ubunge wa Viti Maalum? Mawakili wa bure kutoka CHADEMA?
Kinachoshangaza zaidi, kuna baadhi ya vijana wa CHADEMA katika mkutano huo walikuwa wanamshangilia wakati akielezea uwongo wake.
Mwl. Nyerere aliwahi kusema, ‘’Ukiona mtu anakwambia jambo la kipumbavu na yeye mwenyewe anajua kuwa unajua ni la kipumbavu..ukilikubali ujue atakudharau’’.