Mama Samia na Mama Salma Kikwete waitikisa lindi

Mama Samia na Mama Salma Kikwete waitikisa lindi

Robethn

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2015
Posts
2,103
Reaction score
354
[h=2]MAMA SAMIA, NAPE NA MAMA SALMA KIKWETE WAITIKISA LINDI MKUTANO WA KAMPENI[/h] Maelfu ya wanainchi mkoa wa Lindi wamejitokeza kwa wingi katika kampeni za mgombea mwenza wa urais CCM.

Aliyekuwa Katibu wa wilaya ya Lindi mjini wa Chadema, AbdallaMadebe ambaye alikuwa ndiye mpigadebe mkubwa wa Mbunge anayemaliza mda wake wa Lindi mjini, maarufu kwa jina la -----, akibebwa na wananchi baada ya kutangaza kuhamia CCM, katika mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea wenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika eneo la Mnazi Mmoja, mkoani Lindi leo. Pamoja na Katibu huyo wanachama wengine 38 walihamia CCM.
Wananchi akishangilia wakati wa mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan leo katika eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi
Katibu wa NEC, Itkadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akimkaribisha jukwaani, Aliyekuwa Katibu wa wilaya ya Lindi mjini wa Chadema, AbdallaMadebe ambaye alikuwa ndiye mpigadebe mkubwa wa Mbunge anayemaliza mda wake wa Lindi mjini, Maarufu kwa jina la -----, wakati alipoamua kutangaza kuhamia CCM, katika mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea wenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika eneo la Mnazi Mmoja, mkoani Lindi leo. Pamoja na Katibu huyo wanachama wengine 38 walihamia CCM.
Shamrashamra zikirindima wakati Nape akimtangaza Aliyekuwa Katibu wa wilaya ya Lindi mjini wa Chadema, AbdallaMadebe ambaye alikuwa ndiye mpigadebe mkubwa wa Mbunge anayemaliza mda wake wa Lindi mjini, maarufu kwa jina la ----- baada ya kutangaza kuhamia CCM, katika mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea wenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika eneo la Mnazi Mmoja, mkoani Lindi leo. Pamoja na Katibu huyo wanachama wengine 38 walihamia CCM.
Mgombea wenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni za CCM aliofanya katika eneo la Mnazi Mmoja, mkoani Lindi leo
Mgombea wenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan na Mjumbe wa NEC, Lindi Mjini Mama Salma Kikwete wakiwasalimia wananchi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika eneo la Mnazi Mmoja, mkoani Lindi
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsikiliza kwa makini, aliyekuwa Mpigadebe Mkuu wa CUF, Lindi Mjini, Mohammed Omari baada ya kutangaza kuhamia CCM leo katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi
Mke wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi
Wananchi wakiwa na bango la kufagilia uamuzi wa CCM kumpatia nafasi mwanamke Mama Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo eneo la Mnazi Mmoja, mkoani Lindi.
Mgombea Mwwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwa na Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Mtopa, baada ya kuwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi
Mgombea Mwwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Mtopa, baada ya kuwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi
Wasanii wa Bongo Movie kina Wema Sepetu wakiwa kwenye mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi leo
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasili meza kuu wakati wa mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi leo
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu akiwasili meza Kuu wakati wa mkuano wa kampeni uliofanyika leo katika eneo la Mnazi Mmoja mkoani Lindi
Msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu, ukipokewa na waendesha bodaboda ulipowasili Lindi Mjini leo ukitokea jimbo la Mchinga mkoani Lindi
Wananchi wakiwa katika shamrashamra wakati wa mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea Mwenza w Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika jimbo la Mchinga mkoani Lindi leo
Mwananchi akiwa na bango la Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Katika mkutano wa kampeni za CCM uliohutubiwa na Mgombea Mwenza wa Urais Mama samia Suluhu Hassan katika jimbo la Mchinga mkoani Lindi leo
Mbunge wa zamani wa Mchinga,Muhdhihir Mudhihir akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Mtopa katika mkuano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo leo
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akishauriana jambo na Mgombea Ubunge jimbo la Mtera Said Mtanda, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Mchinga, Mudhihir Mudhihir akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo mkoani Lindi
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Mchinga mkoani Lindi
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia suluhu Hassan akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Mchinga Said Mtanda, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo mkoani Lindi.
 
Hawa ndiyo watu maskini kabisa tanzania pamoja na viongozi wengi maarufu kutoka huko kwa akiwa mzee nkapa,bernad membe,na wengine lakini bado wanaishabikia ccm,hawajui ccm ndiyo inapenda waendelee kuwa maskini na wajinga ili ndiyo wachaguliwe tena,mtaji mkubwa wa ccm ni watu wajinga na maskini
 
Kijana baada kupata ki certificate cha journalism ushaanza nyodo na kudharau wanannchi, lofa sana wewe
 
Hawa ndiyo watu maskini kabisa tanzania pamoja na viongozi wengi maarufu kutoka huko kwa akiwa mzee nkapa,bernad membe,na wengine lakini bado wanaishabikia ccm,hawajui ccm ndiyo inapenda waendelee kuwa maskini na wajinga ili ndiyo wachaguliwe tena,mtaji mkubwa wa ccm ni watu wajinga na maskini
Mtaji wa UKAWA ni vijana wajinga wajinga wanaokunywa viroba kuanzia asubuhi mpaka jioni. Kuna vijana wengi tu wapo CCM na wanajitambua kwa kujishughulisha na maisha yamewanyookea. Ndio maana hata Wabunge wenu wa CHADEMA waliwahi kukaririwa wakisema "wanao mshabikia Lowassa, wakapimwe akili."
 
#HapaKaziTu. Safi sana Wana Lindi mpaka kieleweke. Safari ya Magufuli ni moja kwa moja mpaka IKULU. MUNGU ibariki Tanzania, MUNGU mbariki John Pombe Magufuli.
 
Hawa ndiyo watu maskini kabisa tanzania pamoja na viongozi wengi maarufu kutoka huko kwa akiwa mzee nkapa,bernad membe,na wengine lakini bado wanaishabikia ccm,hawajui ccm ndiyo inapenda waendelee kuwa maskini na wajinga ili ndiyo wachaguliwe tena,mtaji mkubwa wa ccm ni watu wajinga na maskini

Hayo sasa ni matusi na dharau zisizokuwa na mashiko.Bunge lililo maliza muda wake liliwa na majimbo 238 kati ya malimbo ccm ikipata majimbo 178 unamaana hayo yote yapo kusini?
 
Hawa ndiyo watu maskini kabisa tanzania pamoja na viongozi wengi maarufu kutoka huko kwa akiwa mzee nkapa,bernad membe,na wengine lakini bado wanaishabikia ccm,hawajui ccm ndiyo inapenda waendelee kuwa maskini na wajinga ili ndiyo wachaguliwe tena,mtaji mkubwa wa ccm ni watu wajinga na maskini

Una mawazo ya kimaskini sana.
 
Lowassa na Sumaye ni sehemu ya Hayo matatizo.Kama Sifa ya Rais ni Ufisadi, Rushwa na Uroho wa Mamlaka basi Lowassa angepita bila Kupingwa
 
Hawa ndiyo watu maskini kabisa tanzania pamoja na viongozi wengi maarufu kutoka huko kwa akiwa mzee nkapa,bernad membe,na wengine lakini bado wanaishabikia ccm,hawajui ccm ndiyo inapenda waendelee kuwa maskini na wajinga ili ndiyo wachaguliwe tena,mtaji mkubwa wa ccm ni watu wajinga na maskini

Siyo maarufu tu, viongozi wa juu kabisa wa serikali na chama na usisahau hadi first lady. Kusini imetoa raisi, waziri mkuu, makamu wa pili wa raisi, mwenyekiti wa ccm, katibu mkuu wa ccm, waziri wa ujenzi nk, nk lakini kimaendeleo ni shiiiiida. Mwisho wa siku wakistaafu hawarudi makwao.

Wanasifia tu fulani kapata Unyerere lakini kimaendeleo ni mwendo wa kinyumenyume. Juzijuzi walikuwa wanalalamikia gas yao, leo vitenge, t-shirts na kapelo ambazo zitachuja baada ya mfuo mmoja zimewasahaulisha yote.

Sitaki kuamini kuwa Mkapa aliongea kimafumbo aliposema kuwa wanaotaka mabadiliko ni wapumbavu na malofa.
 
Hawa wa mama wasijifanye kama vile hawafahamu kwamba serikali ya CCM iliamua kuterekeza mikoa hii ya kusini. Leo hii wanajifanya kupeleka sura zao mbaya huko kwa sera zipi ngeni? Huko ni kwenda kuwakejeli wakaazi wa maeneo hayo.
 
Ni haki yao hao wamama kuchagua wanakotaka sio kila mtu apende ww unapopenda
 
Hivi hiyo ni mkutano wa halmashauri kuu ya ccm au mkutano wa kampeni, mbona wote wamevaa kijani/njano??
 
Back
Top Bottom