Mama Lowassa jiandae kwa 2020

Mama Lowassa jiandae kwa 2020

chikub

Senior Member
Joined
Oct 15, 2015
Posts
110
Reaction score
28
Nina imani na Mama Lowassa, kumbe ni mwanamke mwerevu, jasiri, anaekubalika kwenye jamii na asiyekuwa na uchu wa madaraka. Haya ameyaonyesha kwa vitendo wakati wa kampeni za mume wake, na sasa hivi amekataa kujaza nafasi aliyopewa ya ubunge wa viti maalum ili kupisha wanawake wanzeke wenye uhitaji huo wachukue nafasi hiyo.

Ukawa kama mna akili zenye maono tafadhalini mkumbatieni huyu mama kuanzia sasa, huenda akawa kete muhimu sana kwa UKAWA kwenye uchaguzi wa 2020 katika ngazi ya urais. Mbembelezeni sana hata kama yeye mwenyewe hana mpango huo. Tumechoka kuona watu wenye ndevu waliovaa suluali katika kila uchaguzi wasioshinda.

Kuanzia leo anzeni mchakato kapambe wa kumpatia mama huyu tume huru ya uchaguzi na katiba inayoruhusu matokeo ya urais kuweza kuhojiwa mahakamani, mtaona maajabu makubwa 2020.
 
chikub una roho mbaya sana wewe..mmetafuna pesa za mzee sasa mnataka kula pesa za mama pia...kuweni na utu, muacheni mama apumzike na familiayake..
 
Last edited by a moderator:
chikub una roho mbaya sana wewe..mmetafuna pesa za mzee sasa mnataka kula pesa za mama pia...kuweni na utu, muacheni mama apumzike na familiayake..
Nani kala pesa za Maalim Seif? Tatizo la Lowassa halikuwa pesa bali wizi wa kura.
 
Mnania mbaya sana familia ya Lowasa. Mshalamba billion 15 mnataka mumkamue na mama pia. Nendeni mkamkamue Mzee Mtei na Ndessamburo mnapenda sana kuwaibia wameru
 
Ukosahihi kabisa,lakini watanzania hawawezi kumchagua mwana mke kuwa rais,
 
Ukosahihi kabisa,lakini watanzania hawawezi kumchagua mwana mke kuwa rais,
Mmmh, huo utafiti uliufanya lini, wapi na kwa watu wangapi?. Lipumba, Dr. Slaa, Mbowe, Mrema, Dovutwa, Rungwe, Limo wote ni wanaume mbona hawakuchaguliwa walipogombea? Mbona Mama Mghwila wa ACT alishika nafasi ya tatu kwa kupata kura na kuwashinda wanaume. Hoja yako inatia shaka.
 
Mnania mbaya sana familia ya Lowasa. Mshalamba billion 15 mnataka mumkamue na mama pia. Nendeni mkamkamue Mzee Mtei na Ndessamburo mnapenda sana kuwaibia wameru
ha ha ha,,
 
Acha unafiki mlitaka kumdanganya na kanafasi ka ubunge ili muendelee kulamba pesa ya familia yake, amestukia dili, Lowassa ameangaika sana kwenye studio za ITV, acha wapumzike!
 
Mnania mbaya sana familia ya Lowasa. Mshalamba billion 15 mnataka mumkamue na mama pia. Nendeni mkamkamue Mzee Mtei na Ndessamburo mnapenda sana kuwaibia wameru

Tuma CV yako PCB unaweza pata kazi nzuri zaidi. Inaonyesha unafahamu account za benki na miamala ya wanasiasa. Umbea mzigo.
 
Acha unafiki mlitaka kumdanganya na kanafasi ka ubunge ili muendelee kulamba pesa ya familia yake, amestukia dili, Lowassa ameangaika sana kwenye studio za ITV, acha wapumzike!
CCM wakisikia jina la Lowassa mioyo yao inageuka mishale ya sekunde kwenye saa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom