Mama Kanumba asema Lulu alimuua mwanae kwenye kipindi cha ‘Cook with Wema Sepetu’; Lulu amblock Wema Instagram. Sababu yatajwa ni kuchangia mabwana

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
776
1,330
Jamani mji haukosi issue huu..



Katika episode latest ya shoo ya Miss Tanzania 2006, Mlezi wa Wana Originali (akina Shishi wanacopy tu), Wema Abraham Sepetu iitwayo Cook with Wema Sepetu mgeni alikuwa Mama wa Steve Kanumba.

Katika Mahojiano kati ya Wema na Mama Kanumba wakiwa wanapika ndizi, mama Kanumba alisema mwanae aliuawa.

Wema akauliza swali ambalo limempatia lawama kibao. Swali lilikuwa “nani alimuua? Leo nataka ufunguke mama”.

Mama naye hakuwa na kukopesha wala kupindisha akamtaja Lulu kwa jina lake la Serikali - Elizabeth Michael.

Katika inayoonesha ni kuendeleza chokochoko, Wema akaenda kupost clip ambapo Mama Kanumba anasema yeye ndo binti pekee aliyewahi kupelekewa na mwanaye huku akitamba kwamba hajawahi kuchukiwa na mkwe hata siku moja. Yani waja wengine mnaweza kumchukia ila anashukuru alhamdulillah hajawahi kuchukiwa ukweni.

7F3E8A71-2304-4E10-816F-05D3078FEB74.jpeg


Hii imechukuliwa kama dongo kwa Lulu ambaye maneno mtaani yanadai ndoa yake imepigwa breki na wakwe ambao hawataki kumsikia kwa tuhuma za kuwa mchawi.

Kwakweli jamii ya Instagram haijafurahishwa kabisa na Wema. Amechambwa kushoto, kulia na katikati.

Wananzengo walivyo wachokozi wakaenda kwenye comments za post za Lulu na kumdokeza yaliyojiri.

Majibu ya Lulu ni kama ifuatavyo:

0772CF97-9115-49C9-A80C-F7B5F08A67E7.jpeg


FA6469BA-21CB-478E-A62C-11199350E0B0.jpeg



Inaelezwa kuwa Lulu ameshamblock “shosti” wake huyo ambaye juzi kati tu walikuwa wanaitana “babe” kwenye kipindi hicho hicho cha Wema.

Taarifa zisizo rasmi zinadai kamwe Lulu na Wema hawawezi kupatana kwani wameshapita sehemu hizo hizo ikiwemo kwa Kanumba, Mr. Blue, Idris na Majizo.
 
Pale wote hamnazo si huyo Wema wala mama Kanumba, huyu wema kabla hajaanza kurusha hicho kipindi angalau angejifunza kitu kuhusu kuhoji sio anakurupuka kuuliza maswali ya kijinga halafu na huyo mama Kanumba mkubwa hovyo kamganda mtoto wa ke mwenzie utadhani Luba, huyu mama kama sio mchawi uzeeni ataroga mtu. Hebu wamuache mtoto wa watu atulie kapitia magumu mengi sana sasa ni muda wa kupimzika.
 
Huyo mama pia nadhani kuna kitu hakipo sawa kwake.
Mbona mumewe katulia.
Utu uzima dawa ila huyu mama kakosa busara japo tunajua ana maumivu lakini bado hatumii busara .
Muda mwingine kuna mambo ni bora ukae kimya tu.
 
Mwacheni Wema, kukonda hizo surgery zinasaidia kukonda lakini ukitaka kurudi kuwa mnene unaweza sana tu, mfano ni Mbunifu wa mavazi Hasanali alifanya surgery ila sasa hivi ni mnene, mwacheni lifestyle yake km kaamua kuwa mwembamba na kujiongezea umri wa kuishi 😏😏😏😏
 
Mwacheni Wema, kukonda hizo surgery zinasaidia kukonda lakini ukitaka kurudi kuwa mnene unaweza sana tu, mfano ni Mbunifu wa mavazi Hasanali alifanya surgery ila sasa hivi ni mnene, mwacheni lifestyle yake km kaamua kuwa mwembamba na kujiongezea umri wa kuishi 😏😏😏😏
 
Back
Top Bottom