Mama amchoma mtoto kwa maji moto

Mama amchoma mtoto kwa maji moto

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,607
Mkazi wa kijiji cha ndachi mkoani Dodoma Bi Asha Juma anashutumiwa kwa kosa la kumchoma mwanae mikono kwa maji ya moto kwa kile kilichoelezwa ni udokozi wa nyama
Kaimu mganga mkuu kitengo cha upasuaji hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma Doctor Kato Peleusdr amethibitisha kumpokea Godfrey Banda mwenye umri wa miaka 13 hospitalini hapo.

Awali mashuhuda wa tukio hilo wameelezea namna mama huyo alivyomtendea mwanae kitendo hicho cha kikatli.

Bi.Joyce Juliass ambaye ni mwenyekiti wa ndachi kata ya mnadani ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa serikali pindi wanapoona matuki ya kikatili katika jamii.

Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii Vedastus Matagy kutoka Hospital ya general amesema kuwa Jamii kutokuwa na utayari wa kuripoti matukio ya kikatili na unyanyasaji ndiyo sababu ya kuongezeka kwa vitendo hivyo.

Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 inatamka wajibu wa jamii katika kumlinda na kutunza haki za mtoto ili kuhakikisha analelewa na kuwa ustawi mzuri katika maisha yake ,lakini bado haki za mtoto zinavunjwa.
 
Kupiga au kutoa adhabu kali kwa mtoto sio njia bora ya kumfundisha/kumlea mtoto,kuna mambo mengine watoto huyafanya kwa kutokujua kama hilo alifanyalo ni kosa,mtoto anatakiwa aelimishwe,kipi kizuri na kipi kibaya,yepi madhara ya kufanya jambo baya,

Kupiga mtoto na kumpa adhabu kali ni kumtengenezea mazingira ya kutokujiamini "self confidence" hata anapofika umri mkubwa,ni kumjengea uoga kwa kila alifanyalo akidhani kua pia ni kosa.
 
Huyo Bi Asha unamnunulia nyama KG 20 halafu unampikia vizuri, ale mpaka amalize zote. Ili ajue thamani ya NYAMA au AFYA YA MTOTO ni ipi muhimu.

Hana akili.
 
Mkazi wa kijiji cha ndachi mkoani Dodoma Bi Asha Juma anashutumiwa kwa kosa la kumchoma mwanae mikono kwa maji ya moto kwa kile kilichoelezwa ni udokozi wa nyama
Kaimu mganga mkuu kitengo cha upasuaji hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma Doctor Kato Peleusdr amethibitisha kumpokea Godfrey Banda mwenye umri wa miaka 13 hospitalini hapo.

Awali mashuhuda wa tukio hilo wameelezea namna mama huyo alivyomtendea mwanae kitendo hicho cha kikatli.

Bi.Joyce Juliass ambaye ni mwenyekiti wa ndachi kata ya mnadani ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa serikali pindi wanapoona matuki ya kikatili katika jamii.

Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii Vedastus Matagy kutoka Hospital ya general amesema kuwa Jamii kutokuwa na utayari wa kuripoti matukio ya kikatili na unyanyasaji ndiyo sababu ya kuongezeka kwa vitendo hivyo.

Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 inatamka wajibu wa jamii katika kumlinda na kutunza haki za mtoto ili kuhakikisha analelewa na kuwa ustawi mzuri katika maisha yake ,lakini bado haki za mtoto zinavunjwa.
Wanawake badilikeni acheni ukatili kwa watoto. Sio tabia nzuri hata kidogo mjue kuwa hamuwakosei watoto tu bali mnamkosea Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kupiga au kutoa adhabu kali kwa mtoto sio njia bora ya kumfundisha/kumlea mtoto,kuna mambo mengine watoto huyafanya kwa kutokujua kama hilo alifanyalo ni kosa,mtoto anatakiwa aelimishwe,kipi kizuri na kipi kibaya,yepi madhara ya kufanya jambo baya,

Kupiga mtoto na kumpa adhabu kali ni kumtengenezea mazingira ya kutokujiamini "self confidence" hata anapofika umri mkubwa,ni kumjengea uoga kwa kila alifanyalo akidhani kua pia ni kosa.
Kwanza hilo sio kosa kwa huyo mtoto kwani mtu yeyote akiwa na njaa lazima ale.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom