Balungi
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 234
- 162
Nimesikitishwa sana na kufariki kwa mama mmoja wiki mbili zilizopita, ambaye alikuwa mjamzito katika kijiji cha Nam-bali, Newala mkoani Mtwara baada ya kupata homa iliyopelekea kupelekwa zahanati ya kijijini hapo. Baada ya hali kuendelea kuwa mbaya, alikimbizwa kituo cha afya Chihangu kwa matibabu zaidi lakini alifariki na mtoto aliendelea kucheza tumboni. Ndugu wa mama, waliwaomba marehemu apasuliwe ili kuokoa mtoto aliyekuwa anacheza ila madaktari walikataa kabisa hali iliyopelekea mtoto naye kukosa hewa na kufariki