Malory 200 ya Tanzania yakamatwa Zambia

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Malori 200 yakamatwa Zambia
Serikali ya Zambia ilipiga marufuku usafirishaji wa magogo nje ya nchi, lakini serikali ya DRC inaruhusu.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (Tatoa), Angelina Ngalula, alisema jana kuwa malori hayo yamekamatwa pamoja na madereva na wasaidizi wao 400.

Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Grace Mujuma, alipopigiwa kuzungumzia suala hilo, simu yake ilipokewa na mmoja wa maofisa ubalozi ambaye alithibitisha kuwapo kwa malori yaliyokamatwa nchini humo.

‘‘Balozi amesafiri, lakini ni kweli kuna malori yanashikiliwa hapa na kumekuwa na mazungumzo.

Tunachosubiri ni uamuzi wa serikali ya Zambia,’’ alisema na kuomba asitajwe jina kwa kuwa si msemaji wa ubalozi huo.

Akifafanua, Ngalula alisema malori hayo yalikuwa yanasafirisha magogo kutoka DRC kupitia Zambia kuingia Tanzania kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

Alisema malori yalipofika katika mpaka wa Congo na Zambia yalikamilisha taratibu zote za kiforodha na kuruhusiwa kuendelea na safari kuingia Zambia, lakini baada ya kufika katika maeneo mbalimbali ya Zambia, ikiwamo Nakonde ulipo mpaka wa Zambia na Tanzania, malori hayo yalizuiwa kuendelea na safari.

‘‘Hali ni mbaya huko Zambia kwa kuwa kuna madereva ambao wametelekeza malori na wengine hawajulikani walipo. Serikali ya Zambia imeshikilia malori hayo kwa sababu wanadhani magogo hayo yametoka Zambia licha ya nyaraka kuonyesha kuwa yanatoka DRC,’’ alisema.

Alisema malori hayo ya Tanzania yalipeleka mizigo kwenda DRC kupitia Zambia na wakati wa kurudi yalipakia magogo.

‘‘Nyaraka zote zinaonyesha magogo yanatoka DRC tunashangaa Serikali ya Zambia kuendelea kuyashikilia malori na mzigo,’’ alisema na kuongeza kuwa hata madereva wengine wa malori ambao wako DRC wakiwa wamepakia magogo, wameshindwa kuondoka wakihofia kukamatwa Zambia.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Tatoa, Rahim Dossa, alisema wametoa taarifa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa pamoja na Ubalozi wa Zambia nchini kuhusiana na malori hayo.

Alisema pia wametoa taarifa kwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia ili afuatilie tatizo hilo.

Naye mmiliki wa kampuni ya D&M Systems, Betson Kiwanga, alisema yeye ameathirika kwa kuwa malori matatu yamezuiwa nchini humo.

‘‘Malori yangu yalibeba mzigo wa magogo kutoka DRC na yana nyaraka zote sasa iweje yazuiwe Zambia?’’ alihoji.

Alisema kama ni kufanya ukaguzi walitakiwa kazi hiyo isichukue muda mrefu, lakini sasa ni mwezi mmoja wanaendelea kuyashikilia malori yetu na usalama wa madereva haujulikani.

Chanzo: Nipashe
 
Kwa kosa gani? Hawa ni ndugu zetu,hata lugha zinaingiliana: Lungu vs Fipa.
 
Back
Top Bottom