Sheria inapozungumzia swala la leave, inazungumzia siku 28 za mapumziko zenye malipo kwa mwaka, sick leave, maternity leave, partenity leave na compasionate leave (mwajiri amefiwa na mwenza wake, mtoto, mzazi wake, n.k). Haisemi chochote kabisa kuhusiana na "leave allowance". Lakini waajiri katika kujenga uhusiano mzuri na waajiriwa na kuwapo motisha ndio wanakua na "Other Benefits" katika mikataba ya ajira.
Hapo ni kukaa na HR/Mwajiri na kuweka hicho kipengele sawa, ili allowance leave ijumuishe wategemezi (mke, watoto), na iseme ni wategemezi wangapi. Kipengele kichambuliwe vizuri na kuonyesha watu wapi wana haki ya kufaidika na leave allowance.