Nionavyo moja kati ya mambo yanayotufanya tusipige hatua inayostahili kimaendeleo ni viongozi wetu wa juu kabisa kuchanganya kati ya Malengo na Mikakati ya kufikia malengo hivyo kuhangaika na mikakati bila kuwa na malengo kisha kupelekea kushindwa kujipima au kujitathimini wanapomaliza muda wao wa uongozi (kwa makusudi au kutokujua).
Vile vile ninavyofahamu baadhi ya mikakati ya kiongozi wa juu ni malengo ya kiongozi anayefuata na inaendelea hadi chini kabisa ya utawala. Malengo yapo ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu kutegemea wapi unataka kufika.
Kwa mfano kujenga barabara za lami au changalawe, kujenga maabara, kujenga shule za kata au kuweka miundombinu ya kuvutia utalii n.k haiwezi kuwa malango ya Raisi wa nchi wala wizara husika na hivyo sio mambo ya kupimwa nayo.
Kwa mtazamo huo wizara ya mipango na uchumi haitakiwa iwe ni kitengo ndani ya wizara ya fedha bali iwe ni wizara inayojitegemea au iwe ni wizara iliyo china ya ofisi ya raisi kwa sababu ndiyo inatakiwa kutengeza malengo na mikakati ya nchi ambayo itashushwa kwenye wizara husika kwa ajili ya utekelezaji.
Malengo ya Raisi wa nchi yanatakiwa yawe mapana yanayoelekeza matarajio ya nchi kwa muda fulani (hasa muda mrefu na wa kati).
Kwa mfano malengo ya raisi wa nchi yanaweza kuwa; baada ya miaka kumi nchi inatakiwa iwe na uchumi wa kati (ufafanuzi wa uchumi wa kati unatakiwa utolewe ili iwe rahisi kupima/kujipima) na baada ya miaka mitano serikali ipunguze utegemezi wa bajeti kwa asilimia kadhaa.
Mfano wa mikakati yake ambayo itakuwa malengo ya wizara husika ni kama; (1) kujenga mtandao wa barabara za lami nchi nzima (Wizara ya Ujenzi/Tanroads), (2) Kuwa na watalaam wenye ujuuzi na weledi kwenye sekta muhimu za uchumi na ustawi wa wananchi (wizara ya Elimu & Mafunzi na na wizara ya Serikali za mitaa), (3) kuanzisha miradi ya kilimo cha umwagiliaji nchi nzima (wizara ya Kilimo na wizara ya maji na umwagiliaji), kujenga mtandao wa reli unaounganisha nchi jirani hasa ambazo hazina sehemu bahari "landlocked countries" (wizara ya mawasiliano na uchukuzi), (4) Kulima zao la pamba kwa wingi na kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya kutengeneza nyuzi za pamba na kutengeneza nguo kwa ajili ya soko la ndani badala ya kuagiza nguo toka nje (km. China) kwa ajili ya kupunguza matumizi ya fedha za kigeni bila sababu za msingi ( wizara ya Kilimo, wizara ya viwanda na wizara ya fedha), (5) Badala ya kuhusika na propaganda tu na kupokea wageni, Balozi zetu za nje ziwezeshwe kushughulika na kujenga uchumi kwa kutafuta masoko na kutoa taarifa za ubora na bei halisi za bidhaa zinazoletwa nchini ili kulinda walaji/watumiaji na ili kutoza kodi/ushuru halali unaotakiwa (wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa), nk.
Kwa mantiki hiyo inatakiwa kila wizara iwe na ofisi ndogo kila mkoa ambazo zitakua na wataalaam wa kusimamia mikakati yao ambayo itashushwa toka makao makuu ya wizara badala ya wataalamu kuwa makao makuu kusubiri ripoti tu. Makao makuu ya wizara kuwe na idadi ndogo ya watunga sera na kutafuta fedha na kufuatilia mgawo wao wa fedha toka wizara ya fedha na vyanzo vingine. Kwa mtiririko huo ofisi ndogo za wizara zilizo mikoani zitengeneza mikakati inayotekelezeka kulingana na uwezo wa rasimali fedha na rasilimali watu uliopo.
Mikakati ya ofisi ndogo za wizara itakua ni malengo ya wakurugenzi wa wilaya ambao nao watatengeneza mikakati ya utekelezaji wa malengo yao na kushusha mambo mengine kada za chini (tarafa na kata hatimaye vijiji). Watalaam wengi wanatakiwa kuwa ngazi za chini za utawala badala na kukusanyika wizarani.
Ahadi nyingi za wagombea uraisi zinakua mikakati badala ya malengo. Ni mtazamo wa chini sana kwa raisi kuahidi masuala ya mikakati badala ya malengo hivyo sitegemei rais ajaye awe yule aliyeahidi kujenga maabara, kujenga shule za kata, kujenga kiwanda cha korosho nk.
Kutokana na uelewa wetu ni kweli usiopingika kwamba wapiga kura wengi wanataka kusikia utekelezaji wa muda mfupi wa mambo yanayowasibu, hivyo ili kupata kura, wagombea ni lazima wawambie wananchi kile wanachotaka kusikia, lakini cha kushangaza hata baada ya kuchaguliwa wanakua kama bado wanaendesha kampeni za uchaguzi, badala ya kusimamia malengo wanabaki kuhutubia na kuahidi utekelezaji wa mambo madogo madogo kulinganisha na mamlaka waliyokabidhiwa.
Sitegemei baada ya Raisi kumaliza muda wake wa uongozi ajisifu ati kwa kujenga daraja fulani au kununua kivuko, badala yake atwambie uchumi alioacha unaweza kutengeza kiasi gani cha ajira, kuondokana na utegemezi wa bajeti, kujenga vituo imara vya utafiti wa sekta kuu za uchumi, kuwa na wataalam mahiri katika kila sekta muhimu ya uchumi (badala ya barabara zetu zote kutengenezwa na wachina, ni watanzania wangapi wazalendo amefanikisha kuwawezesha kuwa wakandarasi mahiri), nk.
Kwa maelezo machache "tunataka raisi mwenye mtazamo mpana ambaye anatuahidi kututoe mahali tulipo na kutupeleka mahali pengine bora zaidi na mwisho wa utawala wake tumpime kwa ahadi zake".
Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania ili iwe mahali pa haki, ambapo haki ndio tunda la Amani ya kudumu.