Malengo Makuu ya Maisha

Malengo Makuu ya Maisha

Chipsi yaipembeni

Senior Member
Joined
Jan 8, 2015
Posts
128
Reaction score
93
Katika dunia ya sayansi na technolojia, vijana hatuwezi kutoka kimaisha kama hatuna malengo,yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo tunapaswa kuyawekea malengo.

1) Imani kwa Mungu wako, ukiwa kijana mwenye nguvu panga kumtumikia mungu wako ktk maisha yako.

2) Elimu, kila kijana anapaswa kuwa na elimu,si kwamba namaanisha elimu ya darasani tu,kijana anaweza kuwa na maujuzi kwa kusoma kupitia mitandao na hata kutoka kwa wakubwa na ukatoka.

3) Afya, Leo hii vijana wengi tunakula bila kufuata kanuni za afya,yaani si ajabu Kijana kafariki kwa presha wakati kuna mzee kikongwe tena ananguvu.

4) Uchumi, vijana tuache utegemezi,kijana hadi miaka 25 cha ajabu bado anategemea wazazi sasa atafanya lini maendeleo yake ,weka malengo na upambane kuyatimiza, Mf-nikifikisha miaka18 niwe na tsh1,000,000, kitendo cha kuweka lengo kitakufanya utafute mbinu halali za kuyafikia.

5) Kazi ya maisha, kijana akiwa na uchumi mapema hatakiwi kubweteka,anatakiwa awe na ujuzi zaidi na achague kazi ya kuifanya maisha yote.

6) Familia, sasa kijana unaanzisha familia yako,na tayari utakuwa umejipanga vizuri,ajabu kijana anaingia katika maisha ya familia hata kianzio hana,amka.

7) Huduma kwa wengine, sasa kijana wasaidie wazazi,ndugu na hata wenye shida,panga kwa siku lazima umfanye mtu afurahie uwepo wako,nawe ndivyo utakavyobarikiwa na Alla au Mwenyezi Mungu.
 
If we die afterall, what is the essence of living.
 
Vijana wa siku hizi hata uwashauri vipi lakini vichwa vyao ni kama vinavitobo akili zikiingilia huku zinatokea huku wenyewe ni usharobalo tu
 
Utafutaji wa maisha mazuri unategemea sana na waliokutangulia yaani wazazi.

Miaka 18 katika familia zingine kijana hata F 4 anakuwa hajamaliza.

Cha msingi hapa kila kijana anatakiwa kuanza maandalizi ya maisha yake anapofikisha miaka 12.

Hapa namaanisha, kijana anatakiwa kuelekezwa namna ya kuandaa maisha yake katika umri huu, kama vile kusoma kwa bidii, ku-save pesa za matumizi yake, kutoa sadaka,kuwatembelea wagonjwa mahospitalini, kushiriki katika kazi za kijamii Na mengine mengi.
 
Back
Top Bottom